Pengine serikali ya CCM imechanganyikiwa

Pengine serikali ya CCM imechanganyikiwa

Wazungu wanasema .. Shortcut is the longest way you were not going... Na Waswahel wanasema unaweza kuruka ndogo(haja) ukadhani umesalimika kumbe unaenda kukutana na kubwa

Na shida ya kubwa ni moja haichomi, haiumizi lakini ukiikanyaga lazima uchecheme kama aliyekanyaga mwiba ukamchoma akiwa peku ama ukiwa umevaa kiatu ama kobazi lisilo na soli imara!

Na shida ya kubwa ni moja ukishaikanyaga umeitibua uvundo wake wote
Utanuka wewe na wengine watakukwepa kutokana na harufu hiyo wasijue kutofautisha kama ni yako ama ni ya mwingine umeipitia tuu..!

Tunaaswa na wahenga tukiwa kwenye taharuki tusiwe watu wa kuchukua maamuzi ya haraka! Lakini kubwa kuliko yote kuepuka kuchukua maamuzi yanayotokana na ushauri wa kunguni na papasi
Chama kimeyakanyaga! Kinatoa uvundo mkali.. Wenye pua ambazo silika za kunusa bado zinafanya kazi wataanza kukikimbiaView attachment 2789168View attachment 2789169

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamechanganyikiwa kutoka Kihongosi hadi Sofia Mjema mpaka Makonda😆😆😆
 
Mkuu alihitajika mtu kama Makonda kufufua chama maana Chama kililoose popularity na wanachama walipungua kwa 30%
So lazma warudishe watu kama makonda kwenye system
Very myopic argument...
 
Hiyo nafasi sio uwaziri Ndugu kwamba unahitaji usomi..Inahitaji mtu anayejua kuongea na kutetea hoja za chama ili kujipatia au kuongeza popularity ya chama nisingeshangaa hata kama angapewa Steve nyerere au kama angepewa shilole kwa sababu sio lazma uwe msomi kushika nafasi hiyo mbona NAPE ALIWAHI KUSHIKA
Kwa hiyo watanzania wanachukuliwa kuwa ni watu wajinga wajinga ambao hawahitaji wasomi na watu intelligent kwenye hiyo nafasi siyo??
 
Daudi hajui kuongea, ni heri hata Haji Manara, yaani Manara angeisaidia CCM ila si huyu Daudi.

Ktk kuongea tu Manara peke yake ni sawa na kina Daudi hamsa
Umenena vema kabisa... Yaani hamfikii hata robo pia Steve Nyerere... Anachoweza ni ubabe, ambao ulikuwa unabebwa na nafasi yake ya u RC enzi hizo...
 
Kwa hiyo watanzania wanachukuliwa kuwa ni watu wajinga wajinga ambao hawahitaji wasomi na watu intelligent kwenye hiyo nafasi siyo??
Katiba yetu pamoja na katiba ya chama ndo inavyoelekeza kuhusu Nafasi za kisiasa....mkiambiwa katiba mpya si mnasema Haileti ugali 😅😅
 
Ilo najua mkuu na ndo maana makonda kawekwa ili kurudisha kidgo heshima..watu wamerudisha sana kadi...Zaidi ya kadi 20k zimerudishwa...
Hiyo heshima asiirudishe pole pole mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja ndiyo ije kurudishwa na huyu??
 
Hiyo heshima asiirudishe pole pole mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja ndiyo ije kurudishwa na huyu??
Pole pole Hawezi kurudishwa tena cuz Wanachoangalia ni mpasuko kwenye chama Pole pole hapendi aina ya uongozi Huu wa Msoga style...
Na ni Sukuma Gang Damu so hawezi kurudishwa nchini kabisa ataleta mpasuko kwenye chama...
 
Katika hili Gwajma amefeli sana. Aliwaaminisha waumini wake kua amemfuta kabisaa bashite kwenye historia ya siasa za nchi hii. Kumbe ni nabii wa uongo
 
Mshana jr kumbuka CCM ni chama cha siasa!they are here for winning elections alafu kuna local ele 2014 ,kweny CCM kuna watu wa propaganda na wafia chama ni hao akina makonda,pia huenda wametoa mambo yote mawil kuweaken mitazam ya watu..yote kwa yote makonda nazan ni mbwatukaj mzuri na ni popularity CHADEMA 2014 watatumia muda kumtukana makonda kuliko sera.
2014!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana ndugu. Hata kama mimi ningekuwa CHADEMA hii siku ya leo ingekuwa mbaya sana kwangu. Yaani wakati nafikiria kuzimwa kwa agenda ya bandari mara ghafla naletewa katibu mwenezi Makonda. Yaani huu ni msiba huko Ufipa. Mzee Mshana usijali utarudi kawaida na kuweza kuandika uzi bila kuchanganyikiwa. Huu uzi wako ni ishara kuwa hauko sawa. Tafuta uzi wa Lucas mwashambwa uusome itakusaidia kupunguza maumivu.
Huu uzi wako ni ishara kuwa hauko sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hili Gwajma amefeli sana. Aliwaaminisha waumini wake kua amemfuta kabisaa bashite kwenye historia ya siasa za nchi hii. Kumbe ni nabii wa uongo
IMG-20231022-WA0190.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom