Wazungu wanasema .. Shortcut is the longest way you were not going... Na Waswahel wanasema unaweza kuruka ndogo(haja) ukadhani umesalimika kumbe unaenda kukutana na kubwa
Na shida ya kubwa ni moja haichomi, haiumizi lakini ukiikanyaga lazima uchecheme kama aliyekanyaga mwiba ukamchoma akiwa peku ama ukiwa umevaa kiatu ama kobazi lisilo na soli imara!
Na shida ya kubwa ni moja ukishaikanyaga umeitibua uvundo wake wote
Utanuka wewe na wengine watakukwepa kutokana na harufu hiyo wasijue kutofautisha kama ni yako ama ni ya mwingine umeipitia tuu..!
Tunaaswa na wahenga tukiwa kwenye taharuki tusiwe watu wa kuchukua maamuzi ya haraka! Lakini kubwa kuliko yote kuepuka kuchukua maamuzi yanayotokana na ushauri wa kunguni na papasi
Chama kimeyakanyaga! Kinatoa uvundo mkali.. Wenye pua ambazo silika za kunusa bado zinafanya kazi wataanza kukikimbia
View attachment 2789168View attachment 2789169
Sent using
Jamii Forums mobile app