Tanzania tuna taasisi za umma Goigoi au tunawasimamizi wa taasisi za umma Goigoi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Nimeona viongozi wa kisiasa wakizilalamikia taasisi za umma Goigoi kwamba zinakwamisha ukuaji wa uchumi kati ya asilimia 1 hadi 5 kwa mwaka. Lakini ninavyojua mimi hakuna taasisi Goigoi ila kuna wanadamu waliopewa dhamana za umma ambao watumishi hao ni Goigoi

1. Ufanisi wa hizi taasisi utapatikana pale tu taifa litakubali kuachana na wakurugenzi na wakuu wa taasisi Goigoi na kuweka watu wenye uwezo

2. Ufanisi wa taasisi hizi utapatikana pale ambapo wakuu wa taasisi hizi wataanza kuomba kazi kwa kushindanishwa katika usahili wa wazi. Wapewe KPI na waondolewe kwa kushindwa kufikia malengo

3. Taasisi hizi zitaongeza ufanisi pale ambapo serikali itaacha kufanya nazo siasa za magawio na vitu kama hivyo ambavyo havina uhalisia.

4. Ufanisi utaongezeka endapo taasisi hizi zitalazimishwa kupewa ruzuku kwa kuzingatia ufanisi; kuongezwa kwa maslahi ya watumishi kulingana na ufanisi. Ila kama anayefanya vizuri na asiyefanya vizuri wataonekana sawa basi hakutakuwa na ushindani.

Tupambane na wakuu wa taasisi goigoi
 
Back
Top Bottom