PCCB: Tuna manufaa nayo?

Bandugu,

Kuhusu mtu kulipa $800 na kuendelea hata hapa nyumbani zipo nyumba za bei hiyo tena na zaidi mpaka $2500 hata zingine $3000.....hapa hap bongo zipo hizi nyumba!! na watu wanaishi humo.

Scholarship ya PhD mara nyingi humuwezesha/humruhusu Candidate kuwa na familia yake.........sasa kama Hosea alikuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi na pia akapata Scholarship nir ahisi kwake ku-rent numba US hata kuanzia huko $800 na kuendelea. ukichanganya na marupu rupu yake ya ukurugenzi + vikao + safari za ndani na nje

Mwenye data zake za uhakika atumwagie hapa hili tuzichambue zaidi..........binafsi so far sijaona
 
njuavyo mie kinyozi hajinyoi..labda kwa serikali yeeetu hii ya kishikaji..mambo hayo yatawezekan..ha haha jk amchunguze el..nasie tukae subiri report yake
 
*Nagu, Mwanyika wasema hakuna aliye juu ya sheria
*Wenye kinga ni Rais, Makamu, Waziri Mkuu, mawaziri

Na John Daniel, Dodoma

SERIKALI imesema hakuna aliye juu ya Sheria na kwamba hata Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Bw. Edward Hosea, anaweza kuchunguzwa na Polisi kuhusu tuhuma za rushwa.

Hata hivyo imesisitiza kuwa suala hilo linapaswa kuangaliwa kwa umakini wa hali ya juu na uangalifu mkubwa, kwa kuwa watu wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa wanaweza kumpaka matope kiongozi huyo wa TAKUKURU kwa kuwa ameonekana kuwa mwiba kwao.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Mary Nagu, wakati akizungumza na Majira nje ya ukumbi wa Bunge kuhusu tuhuma zilitolewa kupitia mtandao wa intaneti kuwa Bw. Hosea anakabiliwa na tuhuma za rushwa.

"Mimi ninachojua ni kwamba hakuna aliye juu ya sheria, mtu yeyote akifanya kosa anaweza kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua kisheria, mimi sijui kama kuna tuhuma zozote kuhusu Mkurugenzi wa TAKUKURU, lakini hata kama yapo, suala hilo linapaswa kuchukuliwa kwa umakini na kwa uangalifu sana.

"Mtu anaweza kuona huyu anafanya kazi vizuri, akaamua kuweka uwongo wake ili kutuharibia tusishinde vita ya rushwa, kwanza kama ni kweli kwa nini wasipeleke barua au malalamiko panapohusika? Intaneti imekuwa ofisi ya kupeka barua? Hili suala ni zito na linapaswa hata ninyi waandishi kuwa makini sana," alionya Dkt. Nagu.

Alipoulizwa kama Mkurugenzi huyo ana kinga kikatiba alisema "Kikatiba hajatajwa, waliopo ni Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu na mawaziri, ila mahitaji ya yeye kutajwa moja kwa moja yalijitokeza ili kuweka ulinzi fulani, lakini bado halijawekwa," alisema Dkt. Nagu

Alisema kwa kuwa Katiba ni sheria mama na imeandikwa kijumlajumla, ataendelea kuangalia kama kuna kifungu kinachomzungumza moja kwa moja.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, alisema yeye kama anavyojua, sheria hakuna mtu ambaye hawezi kuchunguzwa kwa kosa lolote na kusisitiza kuwa polisi wanaweza kumchunguza Bw. Hosea, iwapo kuna ulazima wa kufanya hivyo.

"Kwanza mimi sijui kama kuna tuhuma zinazomkabili Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU lakini ninachojua, hakuna aliye juu ya sheria, wote sisi ni raia wa Tanzania, polisi wana uwezo wa kumchunguza Mkurugenzi wa TAKUKURU," alisema Bw. Mwanyika.

Alipoulizwa sheria inasema nini kwa kiongozi kama huyo anapochunguzwa kama anaweza kuendelea kufanya kazi au kupumzika mpaka uchunguzi ukamilike, alisema suala hilo ni la Waziri katika Ofisi ya Rais Utawala Bora, Bw. Philip Marmo.

"Kama nilivyokwambia, sijui kama unayemzungumza ana tuhuma zozote, pia swali hilo muulize Bw. Marmo ndiye anaweza kukujibu vizuri," alisema Bw. Mwanyika.

Alipoulizwa kuhusu kanuni za maadili ya uongozi kwa ujumla kwa mujibu wa sheria, alisema Bw. Marmo anaweza kujibu hilo vizuri zaidi kwa kuwa yeye anawajibika kwa masuala yote ya Utawala Bora.

Naye Grace Michael alisema wanasheria mbalimbali Dar es Salaam nao walisema Mkurugenzi wa TAKUKURU anaweza akachunguzwa tuhuma zozote zinazohusiana na rushwa na vyombo mbalimbali vya Dola kama Idara ya Usalama wa Taifa au kuundiwa Tume.

Wakizungumza jana na Majira kwa njia ya simu kwa masharti ya kutotajwa majina, wanasheria hao walisema hakuna mtu aliye juu ya sheria, hivyo kama ana tuhuma anaweza akachunguzwa na vyombo vingine na tuhuma zake zikabainika.

Aidha, walisema hata watendaji wake wanaweza wakamchunguza endapo atakuwa amejiuzulu ili waweze kutoa taarifa yenye ukweli, kwani kuchunguzwa akiwa bado kazini ni lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi na hawataweza kutoa taarifa sahihi.

"Kuna vyombo kama Usalama wa Taifa ambao wanaweza wakamchunguza, lakini pia maofisa wengine wa taasisi hiyo nao wanaweza wakamchunguza endapo atakuwa amejiuzlu ili kufanikisha uchunguzi huo na kuepuka mgongano wa maslahi," alisema mmoja wa wanasheria hao

Aidha, walisema kutokana na yeye kuwa ni wa kuteuliwa inatakiwa aliyemteua kushika nafasi hiyo aunde Tume ichunguze madai yake na Tume hiyo inaweza ikaundwa kwa kuwekwa watu mbalimbali wakiwamo majaji, wapelelezi, Usalama wa Taifa ili waweze kukusanya taarifa na kisha kutoa ripoti ya tuhuma anazokabiliwa nazo.

Kauli za wanasheria hao zimekuja kama ufafanuzi kuhusiana na kauli nyingine aliyoitoa hivi karibuni Waziri Marmo kuhusiana na tuhuma ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kompyuta dhidi ya Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Hosea.

Akizungumza na gazeti moja kwa simu akiwa nje ya nchi, Bw. Marmo alisema Serikali inachunguza tuhuma hizo ili kuona ukweli na uhalali wake, huku aliyetuhumiwa akikanusha madai yaliyotolewa katika mtandao.
 
Hosea angekuwa kweli ni mkristo tena msabato wa kweli bora angeamua kukaa pembeni ili aruhusu uchunguzi,ila kama atakuwa msafi.

Ndugu yangu Mpakakieleweke, naona usabato umekuingia kweli kweli. Kwani wasabato wana ubora gani kuliko sisi wakatoloki au ndugu zangu waangalikana, wamorovian, waluteri au waislamu?

Nimeipatapata kuwa ni wasabato wenzake wahariri wa magazeti na wanasheria walio na mahusiano ya karibu na watuhumiwa waliopelekwa mahakamani na PCCB ndio waliomvalia njuga bwana Hosea. Na hata waziri wa sheria ameashiria kitu kama hicho!

Mimi naamini hakuna mtu asiye na walakini, lakini kule kuingiza na kutumia imani ya mtu kama kigezo cha uadilifu wa kazi sikubaliani nawe; kwa vile watu hawapewi uongozi kwa vile ni wa imani fulani. Sisi tuogelee accountability based upon ones position NOT their spirituality.

Kwa kumalizia mimi naamini kuwa tuhuma against Hosea should be substantiated with facts, na kwa kusema hilo siyo kumtetea Hosea au kuutetea "ufisadi", ni common sense . Tuhuma hizo zipelekwe rasmi kwenye vyombo vya malalamishi ili zishughulikiwe rasmi. Malalamiko JF siyo official ila JF inaweza kutumiwa ku-initiate an investigation au inaweza ku-influence kuanzishwa kwa probe.

Kwa mfano kesi ya Mahalu (ambaye ni msukuma na Hosea ni msukuma sijui nalo utaitafsiri vipi)kutokana na "facts" zilizopatikana ni kesi ya wizi kwa kughushi nyaraka na ni waazi kabisa kutokana na tunayoyasoma magazetini. Lakini huko mahamani tunasikia kuwa sivyo. Sasa siwezi ku-conlude Mahalu ni mwizi kwa vile tu ana kesi ingawa wakati anafanya kazi wizara ya elimu pia inasemekana alikuwa analipisha scholarships hewa kibao huko ulaya hadi BM aliposhika usukani na kusitisha hayo malipo. Nasikia hata binti yake aliyekuwa na GPA ya 1.6 alikuwa ana sponsorship ya serikali kwa zaidi ya miaka 8. Na kuna tuhuma kuwa hizo pesa ndizo zilitumiwa kununua Ubungo Garments na kuanzisha Law firm na marehemu Nyalali na JSW. All of these are allegations they could be true or not but unless they are substantiated with facts. Na ndiyo maana nimei-underline. Ni tuhuma na zitabaki tuhuma. Ukweli wake ni hadi hapo wale ambao wanatuhumu waweze ku-provide hizo information then yule anaye fanya uchunguzi kazi yake itakuwa rahisi. Haiwezekani kuwa bora limedikwa kwenye "Citizen" au lipo JF basi lazima lichunguzwe. Lazima lichambuliwe lieleweke then ndipo uamuzi wa kuchunguza ufikiwe. Ama sivyo tutabaki kulaumu kwa misingi ya kusema tunaogopa kujulikana.

ZALENDOHALISI
 
huyo aliyesema kuwa hakuna aliyeko juu ya sheria...halafu hapo hapo anatutajia kuna list ya wenye kinga juu ya kufunguliwa mashtaka tumueleweje sasa?
(nilikwenda nikamkuta hayupo) ndo sawa na asemacho
and abt no one kuwa above sheria its true n i support ilo ila only if we are talkin abt theoretical thingy and when it comes to reality hell no it aint true
 
Hosea akipona hapa, akatoe zaka kwa mizimu. naona amepaniwa haswa. na kama kuna ushahidi kwa nini asichunguzwe? yeye ni mtu na ana hisia zake hivyo ni lazima tujiridhishe kuwa ni msafi, si kwa nadharia bali kivitendo.
 
...duh huo msururu wa wenye kinga mbona wengi sana,yaani hawa wote kuna umuhimu gani wa kuwapa kinga kwa faida ya nchi yetu...hata raisi naye kuwe kuna namna ya kumshitaki ili kumweka sawa,sio haki dunia ya leo mtu kuwa na kinga kama hizo 100%
 
Bandugu,

Kuhusu mtu kulipa $800 na kuendelea hata hapa nyumbani zipo nyumba za bei hiyo tena na zaidi mpaka $2500 hata zingine $3000.....hapa hap bongo zipo hizi nyumba!! na watu wanaishi humo.

Scholarship ya PhD mara nyingi humuwezesha/humruhusu Candidate kuwa na familia yake.........sasa kama Hosea alikuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi na pia akapata Scholarship nir ahisi kwake ku-rent numba US hata kuanzia huko $800 na kuendelea. ukichanganya na marupu rupu yake ya ukurugenzi + vikao + safari za ndani na nje

Mwenye data zake za uhakika atumwagie hapa hili tuzichambue zaidi..........binafsi so far sijaona


Give me a brake. Nyumba ya dolla $800 iko state gani? Most of universities locations cost more than that. Labda aseme kwamba ana condo minium lakini sio nyumba kwa hiyo price. Kingine changanya marupu rupu and everything still he will not afford normal life in US because cost living are way higher, and TSH haina nguvu unapoiconvert to dollar. I wanna know what scholarship amabayo anayo.
 
Mtoto ana GPA 1.6 na bado anasoma, shule gani hazina probation period kwa vilaza kama hawa. Damn, this is so sad
 
Hii haiwezekani, awafichie madhambi yao bure, ni lazima naye akandamize rushwa. Kwani hiyo Benzi anayoendesha kaipataje kama sio TAKRIMA?
 
Yaani nchi hii mtu akiwa waziri basi anakuwa na kinga?

No way huyu mwanasheria mkuu hajui kitu anachosema hata kidogo.

Sitaki kuamini kuwa kila waziri anakuwa na kinga ya kujilinda na ufisadi ,jamani hapa kuna haja ya kuangalia hili kwa kina.
 
Na iwe hivyo......

TAKUKURU noma!
2007-12-04 15:43:55
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuipa ruksa ya kufanya chochote kilicho ndani ya uwezo wake kughughulikia mafisadi nchini, sasa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, TAKUKURU, ni noma kweli kweli.

Chini ya mikakati yake mipya, TAKUKURU imeapa kuyakomba mapesa yote yaliyotwaliwa kwa njia za rushwa na baadhi ya vigogo Serikalini na watu wengineo nchini kabla ya kwenda kuyaficha kwenye akaunti za mabenki yaliyo nje ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa chanzo chetu ndani ya TAKUKURU, ni kwamba chini ya mkakati huo, baadhi ya vigogo wenye tabia za ulafi wa mali za umma wataipata freshi.

Kimesema chanzo hicho kuwa hadi sasa, mkakati huo uko katika hatua muhimu inayoweza kuzaa matunda katika kipindi kisichokuwa kirefu kuanzia sasa.

Chanzo hicho kimeihabarisha Alasiri kuwa hatua hiyo, ni sehemu ya mbinu za kisasa zinazoendelea kubuniwa na TAKUKURU katika kukomesha vitendo vya rushwa kubwa kubwa (grand corruption), ambayo hurudisha nyuma nia njema ya Serikali katika kuwaletea maisha bora wananchi wake.

`Mara zote, wala rushwa kubwa kubwa hukimbizia mapesa yao katika akaunti za nje ya nchi� sasa TAKUKURU iko katika mchakato wa kuhakikisha kuwa mapesa hayo yanarejea nyumbani ili yatumike kwa maendeleo ya nchi,`kikasema chanzo chetu.

`Mkono wa TAKUKURU utafika Uingereza, Ufaransa, Italia, Uswis na kokote kule duniani� pia wahusika watachukuliwa hatua za kisheria, tena bila kujali nafasi zao katika jamii,` kikaongeza chanzo hicho.

Aidha, katika kuthibitisha kuwa sasa TAKUKURU imepania hasa kuwaletea noma wala rushwa vigogo almaarufu kama mapapa, jana Mkurugenzi wake mkuu Dk. Edward Hosea alizungumzia suala hilo la kurejeshwa kwa fedha na mali zilizosafirishwa nje ya nchi kwa njia ya rushwa jana.

Dk. Hosea alizungumzia suala hilo wakati akiwa kwenye semina ya masuala ya rushwa iliyofanyika katika hoteli moja Jijini ambapo mwezeshaji mmojawapo katika semina hiyo alikuwa Bw. Alan Bacarese.

SOURCE: Alasiri

Source link: IppMedia.

SteveD.
 
TAKUKURU imejidhalilisha sana!!

Kama kweli huyu Hosea na wenzake wana moyo wa kizalendo ni bora wakawajibika mapema na ningependa wafahamu kwamba hii issue haiishii bungeni itapelekwa mahakamani na hizo mali walizozipata kwa njia hii ya ufisadi tutawafilisi.....

Mpaka kieleweke hapa....
 
Ofisi ya mwanasheria mkuu na PCCB ndio idara mbili ambazo kama tunataka mabadiliko basi lazima zisafishwe kweli kweli. Hawa wakiwa effective mambo mengine yote yataenda inavyotakiwa.

Inatakiwa wakurugenzi wote waende na maji na hizi idara zianze upya kabisa.
 
Waheshimiwa wana JF naomba radhi kwanza kwa kutumia lugha ya kigeni katika kuomba mwoongozo huu, Na Pili kuna sheria ya fedha haramu ililiyo pitishwa na bunge mwaka juzi (THE ANTI-MONEY LAUNDERING ACT, 2006) ambayo inapitaka hata kwenye tovuti ya bunge au hata Google, Part III (PROHIBITION OF MONEY LAUNDERING) na part IV (ANTI-MONEY LAUNDERING SUPERVISION, Section 17) na Part VI (MISCELLANEOUS PROVISIONS, Section 28)
Nimechambua hili jambo Kwa upeo wangu mdogo wa sheria (kumradhi) na kusikiliza manung’uniko wa waheshimiwa waliojiengua jana eti WAMEONEWA! Sijui kama wanajua hili........

Proving that proceeds are the benefit of "criminal conduct" will usually be done by circumstantial evidence. Where money laundering offences are proceeded with on the same indictment as the underlying crimes, the underlying criminal conduct will be proved as part of the proceedings to the requisite standard.
Where the money laundering proceedings are "stand alone" it is necessary to prove the underlying criminal conduct in the money laundering prosecution.
It is not necessary in "stand alone" money laundering prosecutions to wait for a conviction in relation to the "criminal conduct" (i.e. the underlying or predicate offences giving rise to the criminal property).
Prosecutors are not required to prove that the property in question is the benefit of a particular or a specific act of criminal conduct; as such an interpretation would restrict the operation of the legislation. The prosecution need to be in a position, as a minimum, to be able to produce sufficient circumstantial evidence or other evidence from which inferences can be drawn to the required criminal standard that the property in question has a criminal origin.
Typically evidence of the criminal origin of proceeds may be provided in money laundering proceedings by:
Accomplice evidence;
Circumstantial evidence and/or other evidence;
Evidence of complex audit trails, from which an accountancy expert may be able to conclude that the complexity of the transactions indicate that the property was the proceeds of crime by analogy, it would seem permissible for a witness to give expert evidence that the facts lead him to the conclusion that the property was the proceeds of crime);
Criminals often attempt to launder proceeds through a cash intensive business. Where the cash flows appear too large or the profit margins too high this may be capable of giving rise to expert evidence that the business will usually give rise to a particular level of profit and the profits are clearly excessive which together with other available evidence can be sufficient to prove the underlying criminality.

Naomba mwongozo wenu tafadhali.....
 
Tumekuwa tukiandika mara nyingi lakini watu wanatupuuza wakifikiri sisi ni wachonganishi lakini ukweli ni kwamba TAKUKURU inaenda pabaya, morale ya wafanya kazi ipo chini.
sasa twende kwenye hoja yenyewe.

1.Kuhusu uchunguzi wa Richmond na TAKUKURU Mambo yafuatayo yafahamike.
• Taarifa iliyosomwa kwa vyombo vya habari ni taarifa ya Hoseah na wala siyo ya TAKUKURU. Kwani taarifa ya kweli ya uchunguzi Hosea aliiweka kando ikaandikwa taarifa nyingine ya kuvipa vyombo vya habari na kuwalinda marafiki zake.
• Matokeo yake wachunguzi wote waliohusika na uchunguzi wa Richmond wakaamishwa makao makuu mara moja kuwaziba midomo. Jk afanye uchunguzi atabaini haya.
• Mbaya zaidi wakati kamati ya Richmond ikiwahoji wahusika wote Hoseah kwa woga akamtuma mkurugenzi wake wa uchunguzi ndiye ahojiwe na badala yake, yeye akadanganya kwamba amekwenda kutibiwa India wakati alikuwa likizo chikago marekani kwa familia yake. Kamati ya bunge ya uchunguzi wa Richmond imebaini hilo.



Matumizi mabaya ya pesa.
Hoseah ana matumizi mabaya ya pesa , na ufisadi sasa anaufanya ndani ya TAKUKURU. Kwanza alitumia Tsh Mil 170 kukarabati nyumba ya mkurugenzi mkuu, na ukarabati huu haukuwa na tender yeye ndiye aliyechagua mtu wa kufanya kazi hii, sasa kituko ni kwamba baada ya hapo alimpatia rafiki yake huyo tender ya kuzunguka katika ofisi zote za TAKUKURU mikoani na kupiga rangi bila tender kupita , kwa kumwagiza mhasibu mkuu afanye malipo hayo. Sasa inakuja ajabu ni kwamba rafiki yake huyo ndiye anamjengea hekalu huko maswa –Mwanza. Hapo hakuna rushwa kweli, haya mambo ni ya kweli na uchunguzi ukifanyika yapo wazi.
Kama Ikulu inataka iangalia manunuzi yote yaliyofanya na Hoseah tangu aingie madarakani itagundua ukiukwaji wa tarataibu usio mfano na ukijaribu kuoji au kushauri tofauti anakupa adhabu ya kukuamisha.
Kama alivyosema Mwakiembe, watanzania wengi ni waoga, watu waliopo makao makuu wanayajua mengi kuliko sisi tulioko mikoani, lakini wanakaa kimya kwa kuogopa kuamishwa, sijuhi wanafikiri huku mioani tunaishi ndege tu.?


Mambo yanayomlinda Hoseah.
• Kwa sababu kabla ya hapa alikuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi kwa miaka 10, anajua madhambi yote ya viongonzi waliopo madarakani kiasi kwamba anaitumia hiyo kama insurance kwani wakimtoa atawalipua.
• Baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu na Lilian Mashaka kuteuliwa kuwa naibu Mkurugenzi Mkuu kulitokea pengo la nafasi mbili za mkurugenzi wa uchunguzi na mkurugenzi wa elimu kwa umma, hivyo Hoseah alitumia nafasi hiyo kuteua watu wadhaifu katika nafasi hizo, watu ambao hawawezi kumbishia kwa jambo lolote. Hii ina implication nyingi, kwanza kwa kumteua mtu dhaifu kuiongoza idara ya uchunguzi ambayo ndiyo kiini cha TAKUKURU inampa yeye nafasi ya moja kwa moja kuingilia shughuli zake. Na kwa kuwa mkurugenzi wa uchunguzi wa sasa (alex mfungo) siyo mwanasheria ni raisi kwake kumzidi ujanja. Pili nafikiri watu mmeishona vipindi vya TV ambavyo mkurugenzi wa sasa wa elimu kwa umma amewakilisha PCCB, hata maswali yanamshinda kujibu huyu kweli ni mtu wa kuchagulia wakati PCCB ina watu makini wengi tu, wana TAKUKURU tuona aibu kweli kweli.
Ipo haja kwa bunge kuteua kamati kama ya Mwakyembe kwa ajili ya kuchunguza manunuzi na matumizi ya pesa yaliyofanyika TAKUKURU tokea Hoseah achaguliwe kuwa mkurugenzi mkuu kama yanafuata taratibu za PPRA.
 
Jamani kuhusu swala la mwanasheria mkuu, dont you think its time hizi post wapewe watu waliosoma currently, nikimaanisha kuna watu wengi competent waliosoma sheria miaka hii na wanakosa ajira kwa kubaniwa na hawa wazee waloisoma miaka ile na wanaongozwa na mawazo ya wakati ule kiasi kamba hawajui kinachoendelea duniani maana wengi ya hawa wazee hawana hata culture ya kujisomea,hivyo kuleta tabu. Mbaya zaidi hawa hawa watu ambao ni competent wanaojua current issues wanachukuliwa na mafisadi against their own goverment. Ifike wakati wazee wakapumzike walee wajukuu ili watu wanaochipukia wenye uwezo mkubwa wapewe nafasi kufanya mambo. Na hii iwe kila sector.
 
Jamani tuwe macho na hawa Wanasiasa na wasioitakia mema Takukuru,msitake kupindisha mjadala kwa kuandika masuala yanayomuhusu Dk. Hoseah,ninafahamu kwamba;
Uchunguzi walioufanya Takukuru kama ilivyokuwa kwenye sheria yao ya zamani ulihusu rushwa,na Dk Mwakyembe ktk taarifa yake hakuna sehemu aliyozungumzia kwamba kuna rushwa fulani waliyoiona ambayo Takukuru hawakuifanyia kazi
Na hata ripoti waliyotoa hawakuzuia vyombo vingine kama PPRA visifanyie kazi,nikiikumbuka ile taarifa yao walisema kuwa serikali haikupata hasara hadi wakati ule kwa sababu hakukuwepo pesa iliyolipwa,sasa ulitaka Takukuru wawe wanasiasa kwa kusema wananchi walikuwa gizani hivyo Serikali ilipata hasara na ushahidi huo wapeleke mahakamani?
Tusiwaonee Takukuru na Dk Hoseah,kwa uelewa wangu mdogo wa utumishi wa umma Dk Hoseah siyo ngazi ya uteuzi wa Wakurugenzi,wanateuliwa na Rais,usipotoshe umma kwa kuwadanganya Wananchi kuwa yeye aliteua Wakurugenzi dhaifu,ninachofahamu mimi hao Wakurugenzi wana uzoefu wa muda mrefu kwenye utumishi wa umma,udhaifu wao upo wapi? Kwenye kujibu maswali?
Umedai Dk Hoseah aliikimbia kamati ya Richmond,ulitaka aende nani kama siye Mkurugenzi wa uchunguzi anayesimamia masuala yote ya uchunguzi Takukuru?
Mwacheni Dk Hoseah aitengeneze Takukuru vizuri,kwani hatujui kwamba wakati wa Gen Kamazima wewe Alex Kuhanda na Awadh Mohamed mlikuwa miungu watu? Marupurupu mangapi mlikuwa mkiyapata ambayo watumishi wenzenu walikuwa hawayapati? Ninafahamu kuwa Dk Hoseah kaifanya Takukuru imekuwa ya wote, kawadhibiti kisawasawa,suala la wewe Awadh kushindwa hata kunyoa ndevu,nalo ni la Dk Hoseah? Nani alikutuma uoe wake zaidi ya wawili? nyie endeleeni na juhudi zenu za kupeleka maneno huko na huko ya majungu,hamuwezi kuupotosha umma.Wabunge mliokamatwa na Rushwa tunawajua,tumewaona mnavyochangia kwa kuonyesha chuki zenu,mlitaka msikamatwe? ITENDEENI HAKI TAKUKURU,MTENDEENI HAKI DR HOSEAH.
 
Jamani tuwe macho na hawa Wanasiasa na wasioitakia mema Takukuru,msitake kupindisha mjadala kwa kuandika masuala yanayomuhusu Dk. Hoseah,ninafahamu kwamba;
Uchunguzi walioufanya Takukuru kama ilivyokuwa kwenye sheria yao ya zamani ulihusu rushwa,na Dk Mwakyembe ktk taarifa yake hakuna sehemu aliyozungumzia kwamba kuna rushwa fulani waliyoiona ambayo Takukuru hawakuifanyia kazi
Na hata ripoti waliyotoa hawakuzuia vyombo vingine kama PPRA visifanyie kazi,nikiikumbuka ile taarifa yao walisema kuwa serikali haikupata hasara hadi wakati ule kwa sababu hakukuwepo pesa iliyolipwa,sasa ulitaka Takukuru wawe wanasiasa kwa kusema wananchi walikuwa gizani hivyo Serikali ilipata hasara na ushahidi huo wapeleke mahakamani?
Tusiwaonee Takukuru na Dk Hoseah,kwa uelewa wangu mdogo wa utumishi wa umma Dk Hoseah siyo ngazi ya uteuzi wa Wakurugenzi,wanateuliwa na Rais,usipotoshe umma kwa kuwadanganya Wananchi kuwa yeye aliteua Wakurugenzi dhaifu,ninachofahamu mimi hao Wakurugenzi wana uzoefu wa muda mrefu kwenye utumishi wa umma,udhaifu wao upo wapi? Kwenye kujibu maswali?
Umedai Dk Hoseah aliikimbia kamati ya Richmond,ulitaka aende nani kama siye Mkurugenzi wa uchunguzi anayesimamia masuala yote ya uchunguzi Takukuru?
Mwacheni Dk Hoseah aitengeneze Takukuru vizuri,kwani hatujui kwamba wakati wa Gen Kamazima wewe Alex Kuhanda na Awadh Mohamed mlikuwa miungu watu? Marupurupu mangapi mlikuwa mkiyapata ambayo watumishi wenzenu walikuwa hawayapati? Ninafahamu kuwa Dk Hoseah kaifanya Takukuru imekuwa ya wote, kawadhibiti kisawasawa,suala la wewe Awadh kushindwa hata kunyoa ndevu,nalo ni la Dk Hoseah? Nani alikutuma uoe wake zaidi ya wawili? nyie endeleeni na juhudi zenu za kupeleka maneno huko na huko ya majungu,hamuwezi kuupotosha umma.Wabunge mliokamatwa na Rushwa tunawajua,tumewaona mnavyochangia kwa kuonyesha chuki zenu,mlitaka msikamatwe? ITENDEENI HAKI TAKUKURU,MTENDEENI HAKI DR HOSEAH.

Wambili,

Kweli hata Mamba ana mpenzi wake. Hii ya Hosea na PCCB management yaani inatakiwa hata leo ivunjwe kabisa.

Hakuna wanachofanya zaidi ya ubabaishaji na rushwa. Hivi unahitaji kweli kwenda kusoma PhD ya corruption kujua yanayotendwa na wanasiasa TZ?

PCCB na ofisi ya Mwansheria mkuu inatakiwa zisafishwe hasa, tena yasiishie kwa Hosea peke yake bali hata Wakurugenzi wake, maana kama walichunguza
na kuwa na taarifa tofauti kwanini hawakwenda kuiona tume ya Mwakyembe?

Ingelikuwa uamuzi wangu, hizo idara mbili ni kupitisha mafuriko na wala sio fagio la chuma, inatakiwa kusafisha kila kitu.

Vijana kuna ajira PCCB na ofisi ya Mwanasheria mkuu, jiandaeni tu.
 
u deserve asante hakuna kitu kizuri kuongea with authorities of law i never new this Act b4 despite that i`m a legal practitioner let all the consequenses be upon them concenrned under arm of law and for this in case they are taken to courts of law i pray that judges may dispense justice for the public interest,dont expect them to abuse their noble proffession like those of AG`s chamber its shame
 
Back
Top Bottom