PCCB: Tuna manufaa nayo?

PCCB: Tuna manufaa nayo?

hii gestapo ya kikwete na lowassa ivunjwe na chombo kipya kiundwe kiwe independent ki report kwenye judicial na sio executive branch
 
Jamani kuna taarifa zilizoenea kwamba eti ripoti aliyoisoma Bw. Hosea kwenye vyombo vya Habari wakati PCCB walipofanya uchunguzi wa Richmond sio ambayo iliwasilishwa mezani kwake na wafanyakazi wake....! taarifa zinasema aliifanyia marekebisho na kutoa ripoti mpya aliyioiandika yeye binafsi.

Hivi bado yuko ofisini? Anasubiri nini huyu mtu, au kashaomba kuachia ngazi...? mi nashauri kikwete amfanyie kama Balali, asipokee kujiuzulu kwake, amfukuze...!

Kuna tuhuma za kwamba alimpikia majungu mwandishi wa habari wa Gazeti la THE FAMILY MIRROR akahakikisha kijana amekwenda jela, eti kwa sababu alimuandika vibaya kwenye gazeti hilo la FAMILY MIRROR...! Mwandishi huyo yuko jela mpaka hivi sasa nnapoandika hii email, hii ni habari ya ukweli kabisaaaa...!
 
Mkuu Kalamu,

1. inaonekana rushwa imekuwa tatizo kubwa hata kudhoofidha sana uchumi wa Tanzania. Kwa utajiri wa rasilmali tulizonazo, na jinsi zinavyotumika, inawezekana tungekuwa matajiri miongoni mwa nchi za kusini mwa Afrika. Unadhani pengine kwa kutambua uzito wa tatizo, na kwa sababu rushwa mbaya zaidi ni ile kubwa (grand corruption, tuunde chombo cha maafisa wa uwezo wa juu sana kama The Scorpions, wa South Africa?

2. Vinginevyo, tubadilishe muundo wa PCCB kwa kuiweka chini ya wananchi, yaani iwajibike kwa bunge. Hii nayo nadhani ni effective, kwa kuwa hawa watakuwa wanafanya kazi without fear or favour.

Lakini hizi njia zote mbili zinahitaji political willingeness ya serikali, je itakuwa tayari? What do you think?

Ninakubaliana na Na.2,yako hapo chini. Labda itasaidia kidogo.
 
kaka hivi kweli chombo cha kudeal na rushwa una kiona ni sawa na uraisi? ingawa sikubali hili la kueleta hao experts. lakini kama watakuja kwa kufanya uchunguzi wa 'damu' ili kutibu majipu kama alivyosema wangwe, chacha naona itakuwa vizuri! si umesikia mambo mazuri yaliyofantwa na delloite na ernest and young? hawa wote sio makampuni ya ndani! ni wataalum kutoka 'nnje'. na wametuletea matunda mazuri tu. mimi nadhani tunawahitaji kuja kutuonyesha wabaya wetu then watuachie wenyewe tuendelee sasa na kina mwakiembe wetu.

Humble S

Ukisoma vizuri ( Btw the lines ) post yangu utajua kitu gani nina maanisha....
 
Jamani kuna taarifa zilizoenea kwamba eti ripoti aliyoisoma Bw. Hosea kwenye vyombo vya Habari wakati PCCB walipofanya uchunguzi wa Richmond sio ambayo iliwasilishwa mezani kwake na wafanyakazi wake....! taarifa zinasema aliifanyia marekebisho na kutoa ripoti mpya aliyioiandika yeye binafsi.

Hivi bado yuko ofisini? Anasubiri nini huyu mtu, au kashaomba kuachia ngazi...? mi nashauri kikwete amfanyie kama Balali, asipokee kujiuzulu kwake, amfukuze...!

Kuna tuhuma za kwamba alimpikia majungu mwandishi wa habari wa Gazeti la THE FAMILY MIRROR akahakikisha kijana amekwenda jela, eti kwa sababu alimuandika vibaya kwenye gazeti hilo la FAMILY MIRROR...! Mwandishi huyo yuko jela mpaka hivi sasa nnapoandika hii email, hii ni habari ya ukweli kabisaaaa...!

Mwandishi huyo anaitwa Zephania Musendo...alipandikiziwa rushwa na Hosea kwa kuwashirikisha waandishi fulani wa serikali, akakamatwa na kufungwa. Lengo la kumkomoa likawa limetimia.
 
Tukitaka kuwa wakweli, hatuhitaji chombo kama hiki kwa ajili ya kupambana na rushwa. Haijawahi kuwa na mafanikio na kwa muundo wake haitatokea iwe na mafanikio hata kama atawekwa mwana JF pale! Kama tukitumia vizuri vyombo tulivyo navyo vya kutekekeleza sheria hatuna haja ya kuwaongezea walipa kodi limzigo la kitu kama hiki ambacho sanasana ni kichaka cha wahujumu uchumi tu. Sababu pekee ya kulibakisha dubwana kama hili labda ni hao watu walioajiriwa maana ni wengi na kuvunjwa kwake familia nyingi zitateseka sana! So kubaki kwake it is purely on humanitarian grounds, nothing to do with rushwa!
 
PCCB, POLISI, USALAMA WA TAIFA, FFU ni vyombo vya CCM na vipo kwa ajili ya kulinda, kutetea na kuendeleza masilahi ya CCM. Hivi si vyombo vya Tanzania.

Katika hili suala la kashfa ya Richmond tumeona wazi kwamba hawa jamaa wa PCCB waliifagilia na kuipigia deki ripoti ya Richmond lakini ukweli wenyewe umekuja kujulikana na tume ya Mwakyembe.

Wakati na muda umefika kwa watanzania kuvunja vyombo hivyo ama kubadilisha kabisa muundo na utendaji wa vyombo hivyo. Kwa kipindi hiki kuna umuhimu wa wazi kabisa wa kuwachukulia hatua wale wote waliopewa jukumu la Richmond na wakalipitisha bila kuona wizi na madudu machafu yaliyofanywa na mafisadi.
 
Ninapata mashaka yale yale ya siku zote! Kwamba huwa hatusomi vizuri btn the lines...

Chombo kilichoshindwa kuchunguza ile rushwa ya Richmond kilikuwa ni PCB au TAKURU...

Naomba mukumbuke kwamba PCB/TAKURU inanzishwa na sheria dhaifu sana... hiyo sheria haikuweza kupambana na rushwa hata kidogo...

Ndio maana sheria ikapelekwa kubadilisha hiki chombo... sasa PCCB/TAKUKURU...

Nina pata mashaka kwamba Tume ya Mwakyembe iliihukumu PCB/TAKURU kwa sheria ya PCCB/TAKUKURU.

Bila kumtetea Hosea... lakini najua hajiuzulu kwa sababu hii tu na si nyingine...

PCB/TAKURU ilikuwa ina zungumzia bribing tu! ambayo sio Tume ya Mwakyembe wala PCB/TAKURU walioweza ku-establish kwamba rushwa (bribing and not corruption) ilikuwepo....

Ni kwa sababu hii bado Hosea ana confidence maana ripoti yake imefanya kazi kwa kufuata sheria ile ya 1971 ya Rushwa
 
Jamani kuna taarifa zilizoenea kwamba eti ripoti aliyoisoma Bw. Hosea kwenye vyombo vya Habari wakati PCCB walipofanya uchunguzi wa Richmond sio ambayo iliwasilishwa mezani kwake na wafanyakazi wake....! taarifa zinasema aliifanyia marekebisho na kutoa ripoti mpya aliyioiandika yeye binafsi.

Hivi bado yuko ofisini? Anasubiri nini huyu mtu, au kashaomba kuachia ngazi...? mi nashauri kikwete amfanyie kama Balali, asipokee kujiuzulu kwake, amfukuze...!

Kuna tuhuma za kwamba alimpikia majungu mwandishi wa habari wa Gazeti la THE FAMILY MIRROR akahakikisha kijana amekwenda jela, eti kwa sababu alimuandika vibaya kwenye gazeti hilo la FAMILY MIRROR...! Mwandishi huyo yuko jela mpaka hivi sasa nnapoandika hii email, hii ni habari ya ukweli kabisaaaa...!

Hosea anaujua sana Umafia na usabato wake wa kijinga .Anayajua waliyo yafanya wakati wa uchaguzi mwaka 2005 na sasa ana madaraka so anaweza kufanya lolote .Lakini leo anachekelea madaraka na kesho nguvu ya Mungu na uwezo wake ukiamua kulipa haki Hosea ataadhirika sana .Siku zake naamini zimeanza kuhesabika .
 
Ninapata mashaka yale yale ya siku zote! Kwamba huwa hatusomi vizuri btn the lines...

Chombo kilichoshindwa kuchunguza ile rushwa ya Richmond kilikuwa ni PCB au TAKURU...

Naomba mukumbuke kwamba PCB/TAKURU inanzishwa na sheria dhaifu sana... hiyo sheria haikuweza kupambana na rushwa hata kidogo...

Ndio maana sheria ikapelekwa kubadilisha hiki chombo... sasa PCCB/TAKUKURU...

Nina pata mashaka kwamba Tume ya Mwakyembe iliihukumu PCB/TAKURU kwa sheria ya PCCB/TAKUKURU.

Bila kumtetea Hosea... lakini najua hajiuzulu kwa sababu hii tu na si nyingine...

PCB/TAKURU ilikuwa ina zungumzia bribing tu! ambayo sio Tume ya Mwakyembe wala PCB/TAKURU walioweza ku-establish kwamba rushwa (bribing and not corruption) ilikuwepo....

Ni kwa sababu hii bado Hosea ana confidence maana ripoti yake imefanya kazi kwa kufuata sheria ile ya 1971 ya Rushwa

Mkuu Kasheshe,

wewe ndo unashindwa kusoma between the lines. Dr Hosea anajua chanzo cha kiburi chake ni nini. Tunajua, na hata tume ya Dr Mwakyembe imesema, kwamba taarifa ya TAKURU, au PCB ya wakati huo, ilishindwa kubaini uozo huo.

But the bottom line ni kwamba, hata baada ya sheria kubadilishwa, na kuwa bora zaidi, kwani PCCB hawawezi kuchunguza tena Richmond? Wewe unadhani hawawezi kwenda kuichunguza scandal waliyoshindwa kwa udhaifu wa sheria ya zamani?

Makosa ya Prof Mahalu, ni PCB au PCCB ndo inashughulikia? PCCB came into being just last year, na mikataba mibovu itatuua pole pole for decades to come kama kansa. Tufanyeje basi ili PCCB watukomboe na hali hii? Mbona hakutueleza, na wala hakuieleza tume ya DR Mwakyembe kuwa sheria ya PCB haikuwapa nguvu ya kutosha kupambana na Richmond? Au hakuona umuhimu wa kujitetea yeye na taasisi yake?
 
Mkuu Mbalamwezi, ndio hapo bado haujaelewa sheria ya PCB ilikuwa inaongelea hongo... period... wewe, mimi, Hosea, Mwakyembe wote tunajua kwamba hakuna sehemu yeyete aliyesema kulikuwa na Hongo.

But the bottom line ni kwamba, hata baada ya sheria kubadilishwa, na kuwa bora zaidi, kwani PCCB hawawezi kuchunguza tena Richmond? Wewe unadhani hawawezi kwenda kuichunguza scandal waliyoshindwa kwa udhaifu wa sheria ya zamani?
Kwa hiyo tungejadili hili na wala sio tofauti na hili!

Makosa ya Prof Mahalu, ni PCB au PCCB ndo inashughulikia? PCCB came into being just last year, na mikataba mibovu itatuua pole pole for decades to come kama kansa. Tufanyeje basi ili PCCB watukomboe na hali hii? Mbona hakutueleza, na wala hakuieleza tume ya DR Mwakyembe kuwa sheria ya PCB haikuwapa nguvu ya kutosha kupambana na Richmond? Au hakuona umuhimu wa kujitetea yeye na taasisi yake?

Kesi ya mahalu ni ya uhujumu uchumi,,, nakushauri uwe unasoma mambo vizuri zaidi, PCCB waliingia kwa ajili ya ile issue ya kwamba kama kuna ulimbikizaji wa mali... lakini sio Rushwa...
 
JK alishasema juzi kuwa......anasubiri majumuisho ya Bunge kuhus ripoti ya Tume teule ili ayafanyie kazi mapendekezo yaliyoidhinishwa na Bunge...........i can't see neither Hosea nor Mwanyika surviving........only if Mr President is BOLD from what he said
 
Kesi ya mahalu ni ya uhujumu uchumi,,, nakushauri uwe unasoma mambo vizuri zaidi, PCCB waliingia kwa ajili ya ile issue ya kwamba kama kuna ulimbikizaji wa mali... lakini sio Rushwa...

Nimekusoma, Mkuu Kasheshe.

Sasa, are you still of the opinion kuwa kama chombo kilichoundwa kusimamia maslahi ya nchi, PCCB, baada ya kuchungulia uvundo mle, it had nothing to in the Rich scandal? Hata kushauri tu? Let us be honest.
 
Mbalamwezi Mzee kuuliza kwamba PCCB ivunjwe au la ni sawa na kuuliza kama wewe kweli unaitwa Mabalamwezi. Jibu litakuwa ni resounding YES! Mimi binafsi nafikiri tatizo kubwa sana la kwanza hapa ni huyo Dr. Hosea mwenyewe ambaye huhitaji digrii kujua kwamba si muadilifu hata kidogo. Kwa hiyo hata tungechukua sheria za Marekani tukazileta hapa, kama kiongozi wa taasisi ni huyu Dr. Hosea, hakuna cha maana. Yeye amegeuka kuwa Arron Ringera kule Kenya ambaye licha ya kupewa Kshs. 2.5 million kwa mwezi, amekuwa ndiye mtu wa mbele ku-insulate wala rushwa walimweka madarakani.

Huyu bwana ni tajiri wa kutupwa na yet ofisi yake ya kisheria hata kesi ya kulipwa fees shs. 5 million hajawahi kupata. Akijua kwamba kuna possible conflict of interest, mkubwa huyu ananedesha ofii ya uwakili na kuchukua kesi kwenda mahakamani ambako huwatisha mahakimu kwamba kama hatashinda kesi basi hakimu huyo atamnasisha na rushwa akamatwe na kushtakiwa. Hii imetokea wazi nami nafahamu hilo kwa kesi moja pale kisutu. Yeye anaitumia ofisi hii kupokea rushwa na kuwa-refer wale ambao wanataka kumpa rushwa waende pale ionekane ni wateja tu wa kawaida. In 1997 yeye akiwa Mkurugenzi wa operations aliwahi kumelekeza mu-Eritrea mmoja aliyemtungia kesi aende pale akatoe Tzs. 5 million ili amalize kesi yake hiyo ya kutunga.

Huyu bwana hafai, aondolewe na chombo kivunjwe na kuundwa upya kikiwa na Mzalendo ambaye atachapa kazi kwa uadilifu. Mimi naamini wapo watu wenye sifa. Kwani kina Mwakyembe, Ludovick Utouh na wengine si ni watanzania kama sisi?
 
Wana JF, PCCB imetuangusha WaTz katika mapambano ya rushwa. Ili tuwe na silaha kali, je tuivunjilie mbali tuunde chombo kipya kitakachokuwa, pengine chini ya wabunge? Au tubadili uongozi wa sasa?

Ivunjwe na kindwe chombo kingine kiwajibike moja kwa moja kwa Bunge
 
Nimekusoma, Mkuu Kasheshe.

Sasa, are you still of the opinion kuwa kama chombo kilichoundwa kusimamia maslahi ya nchi, PCCB, baada ya kuchungulia uvundo mle, it had nothing to in the Rich scandal? Hata kushauri tu? Let us be honest.

Ukweli ni Kwamba Dr. Hosea alikuwa asiwe na hatia, kama walichunguza wakati wa PCB, tatizo ni Kimbele mbele kwenye ile barua/tangazo lao maana sidhani kama ina-qualify kuitwa ripoti, ya kusema nchi haukupata hasara yoyote... hapa ndio kwa kufuata PCCB ya sasa tunasema PCCB huenda imepewa mlungula hata kama hatuwezi kudhibitisha... na sheria ya sasa sio kila kitu lazima udhibitishe without doubt.
 
Yote ni sawa na kila moja ina hoja za kuelezeka lakini kwa upande wangu naona, "Tusiruke mko.., Tukakanyaga ma..", hilo ndio la kuchunga zaidi.
 
Naandika hivi nikiwa na JAZBA sana kwani ndani ya Idara za Serikali inaonekana HAKUNA kitu kinaitwa CODE OF CONDUCT.

Nasema hivi kwani nchi hii pamoja na UMASKINI wake pia tunautajiri wetu.

Tatizo kubwa ambalo sasa ni chanzo cha huo UMASKINI ni UBADHIRIFU wa viongozi wetu tuliowaamini na kuwaweka madarakani. Tatizo ninaloliona katika kipindi hiki ni "MAVUNO" makubwa wanayofanya viongozi wetu, kila mmoja katika nafasi yake. Katika hatua ambayo Serikali imekuwa ikijaribu kujinasua katika kukabiliana na SHUTUMA dhidi ya mtindo huu wa Viongozi kuvuna WASICHOPANDA, imekuwa ikiunda vijitaasisi ili jamii iwe na imani na serikali.

Taasisi mojawapo ambayo kwangu mimi naiona kama ni changa la macho katika KUKABILIANA na RUSHWA nchini ni hii TAKUKURU. Hadi sasa sijaona kama ipo kwa maslahi ya taifa. Imeundwa kwa ajili ya kukimbizana na vijirushwa vya mahakamani, vituo vya polisi, mahospitalini, mashuleni na sehemu nyingine ndogo ndogo. Kwa hakika rushwa halisi zipo kwa viongozi waandamizi wa serikali, mfano halisi ni katika hali ilivyo hivi sasa kwani kila kukicha magazeti hayaishi kuandika habari za rushwa za hao viongozi wetu.

Jambo la kushangaza ni kwamba TAKUKURU imekuwa ndiyo shield ngao ya kuwalinda viongozi wanaotuhumiwa. Watanzania hatuna imani na taasisi hii, hadi inafikia tumekuwa na tafsiri mbadala ya neno TAKUKURU kwamba siyo tena TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA. Infact Rushwa haipo kabisa kama wahusika hawapo. Kupambana na rushwa badala ya wala rushwa ni sawa na neno "kesho haiwezi kuwa leo kwani kesho ni kesho milele"

Tunaitaka taasisi hii ipambane na wala rushwa ili rushwa hiyo isiwepo. Hata hivyo kutokana na kutofanya kazi yake ipasavyo kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia mfano wa kuboronga ni katika repoti yake kuhusu ufisadi BoT ambapo taasisi hii ilitoka na taarifa kwamba hakuna matatizo ndani ya BoT ikapelekea Serikali kutangaza tenda ya kufanya uchunguzi wa kiina ndani ya benki hiyo, ndipo Ernst & Young ikashinda na kutoka na ripoti kinyume na ripoti ya TAKUKURU.

Kutokana na hali hii ilikuwa ni nafasi pekee kwa Mkurugenzi wake Dr E Hosea akaonyesha uungwana akajiuzulu wadhifa wake kwa kutoa ripoti ambayo mimi nadhani aliitunga kwa maslahi yake na ya hao ambao hadi leo inaonekana wana manufaa naye. Taasisi hii haina kigeni ni afadhali wafanyakazi wake waingizwe katika taasisi ya Usalama wa Taifa, waendelee na kazi zingine ikiwemo ya kupambana na wala rushwa. Hatuwezi kupambana na dhambi tukaacha kupambana na mtenda dhambi mwenyewe.

Sasa kama kazi ya Taasisi hii itakuwa haina jipya kama ilivyokuwa katika ripoti ya BoT, basi sasa mtakuwa mamilionea kwani huyu Chenge anazo ni wakati wenu KUVUNA. Tunashukuru na tunakuwa na imani kwamba huenda haki itatendeka kuhusu tuhuma hizi dhidi ya Andrew Chenge kwani TAKUKURU haiko peke yake katika kumchunguza kuna taasisi toka Uingereza SFO ambayo tunadhani Watanzania tutatendewa haki.

Kuna wakati mimi huwa naona kwamba ni afadhali tungeendelea kutawaliwa tukajua moja kwamba tunatawaliwa na mkoloni, kuliko kutawaliwa na mzalendo mweusi mwenzetu kwa nje lakini fisadi mbaya. Yaani serikali mnatutesa wananchi. "Mtenda dhambi unatenda dhambi hadi shetani anachukia?" Tumevuka kiwango cha kuvunja maadili ya uongozi.

Mimi na wengine ambao ni wazalendo na wanaipenda nchi yao tunadhani tafsiri halisi ya neno TAKUKURU siyo TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA bali ni TAASISI YA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA. hii ni kutokana na kuonekana kwamba inawatetea wala rushwa na ndiyo maana rushwa ipo.

Pambaneni na WALA RUSHWA na si RUSHWA. kama Mwizi hatakuwepo Waizi nao hautakuwepo. Ukipambana na wizi utauona wapi wakati hujamuona mwizi.

Badilikeni la sivyo mtaiwa TAASISI YA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA.
 
Back
Top Bottom