SaharaVoice,
Kwanza kabisa ndugu yangu ngoja nikuukize swali hili "Je utamwamini yule aliyepewa nyeti azitunze asimpe mtu halafu akakumegea na kukwambia kuwe iwe siri kwa vile aliyempa hizo siri alimwambi ni siri na hatakiwi mtu mwigine ajue; ila kwa vile wewe ni mshikaji nakumegea ila iwe siri!" . Haya nimbie mwenzangu kuna siri hapo? Wewe siyo custodian wa siri za SIRIKALI na bado watamani kuzipata ili iwe nini? Siri za serikali ni za serikali sio za kila mtu!
MENOSUGU
Menosuga,
Siri za serikali ni zile siri zenye manufaa kwa taifa, manufaa kwa wananchi walio wengi. Siri zenye faida kwa wachache, mafisadi na rafiki zao, hata siku moja haziwezi kuwa siri za taifa.
Civil servants hata kwenye nchi zilizoendelea huwa wanaleakisha siri za namna hiyo, matokeo yake viongozi wao wanawajibika zaidi, hawajiingizi kwenye vitendo vya ovyo kwa kutegemea civil servants watawatunzia siri.
Kwa faida ya nchi yetu, siri za hawa wezi zimwagwe tu. Kwa faida ya wanetu huko mbele, lazima hizio siri zianikwe nje ili wasikose pa kujificha.
Kwa kusoma ujumbe wako naona uko tayari kulinda hata uovu kwa kisingizio cha siri ya serikali, kwa kufanya hivyo na wewe utakuwa fisadi. Tukikujua tutakuumbua tu bila kuogopa.
Kama anavyosema Mwafrika wa Kike, inabidi tufike mahali tuchukie
ili hawa jamaa wasituone wajinga. Wakati ndugu zetu wanakufa huko wilayani, wengine wanapasuliwa vichwa badala ya miguu, sisi tunasema siri za serikali, ni serikali gani hii isiyowajibika kwa watu wake?
Tuleteeni hizo siri wengine tuzimwage hapa. Kama nilivyoandika mwanzoni, sijali mleta siri ana motives zipi, ninachojali ni ukweli wa hizo siri. Kitu ambacho sitaki ni kuwachafua kwa makusaudi watu ambao wanachapa kazi, kama walivyomfanya yule jamaa wa wizara ya elimu.