Pay stubs za mshahara wa Rais

Pay stubs za mshahara wa Rais

yote kwa yote ahadi ni deni jamani...mbona mnamtetea sana kulioni?....aliahidi mweneywe wala hakushurutishwa hizo slips ziwekwe tu.
 
Kijana nakushauri tu ufanye kazi kwa bidii ili ujinasue na umaskini uliokuzunguka na jamii yako, vinginevyo utakuja kulia siku za uzee wako. Ni ushauri tu.
 
Tuliyempigia kura hatuna haja ya kuiona hiyo "salary slip" kwani sisi ndiyo waajiri wake! Ni jambo la ajabu sana kama mwajiri anaomba apewe "salary slip" kutoka kwa mwajiriwa wakati ndiye anayemlipa mshahara!
 
Mwanamme kushikilia kuona pay slip ya mwanamme mwenzio ni majanga!

Hujiamini?

Unataka kusema kila mwanaume kuona payslip ya Makamu wa Rais ni halali kwa sababu yeye ni mwanamke? FaizaFox, kuna wakati, japo mara chache sana, huwa unatoa michango mizuri, muda mwingine sijui huwa unaingiwa na nini, michango yako inakuwa ya vijineno vya mitaani hasa. Umekulia mitaa gani? Unaweza kuwa wa thamani zaidi kwa kutoa michango ya kujenga kuliko vijembe.
 
Tuliyempigia kura hatuna haja ya kuiona hiyo "salary slip" kwani sisi ndiyo waajiri wake! Ni jambo la ajabu sana kama mwajiri anaomba apewe "salary slip" kutoka kwa mwajiriwa wakati ndiye anayemlipa mshahara!
unajua chanzo cha hii ishu?
 
Badala ya kujadili mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu tunapoteza muda kujadili mshahara wa rais, kwan akiamua kujichotea kuna atakae mzuia mi ata ajilipe 100 million cha msing atomize aliyoyahidi kwa kwa Watanzania that's all matter pay slip itupotezee muda hapana kwa kweli tubadilike ndugu zangu
 
Jana katika hotuba yake ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi nilidhani labda rais Magufuli atautaja rasmi mshahara wake na ule wa viongozi wengine waandamizi wa umma.

Kuna wakati katika hotuba hiyo alisema hata yeye anapenda mshahara au sijui anapenda mshahara mzuri (nukuu siikumbuki vizuri).

Niliposikia anazungumzia mishahara hamu ya kusikiliza anachokiongea ikazidi kukolea. Mwishowe nikaishia kuambulia patupu.

Sasa leo ni tarehe 2 mwezi Mei. Kama sijakosea, ni mwezi sasa umepita tokea iliporipotiwa kuwa rais alitoa ahadi ya kutoa pay stubs zake akisharudi Dar kutoka mapumzikoni huko Chato.

Mpaka hivi sasa sioni hata mwelekeo wa hicho kitu kufanyika. Je, ina maana tulidanganywa? Kama tulidanganywa, tulidanganywa na nani sasa? Hao waliosema kuwa rais kaahidi hivyo ilhali labda hata hakuongea nao au tulidanganywa na rais mwenyewe?

Mimi hili suala la mishahara ya viongozi wa umma nilianza kulivalia njuga takribani miaka 9 iliyopita na nitalivalia njuga mpaka siku yangu ya mwisho au mpaka hapo kitakapoeleweka.

Ni haki yangu ya msingi kabisa kujua hao viongozi ninawalipa kiasi gani na kwa ujumla wake ni haki yangu ya msingi kujua pesa zangu za kodi zinatumikaje.
 
Sijasahau na sitokuja kusahau kamwe hadi hapo kitapoeleweka kwa sababu kama mlipa nina haki zote za kujua kodi ninayolipa inatumiwaje.

Sasa hapa vipi...Anko Magu alitudanganya au habari kuwa atazitoa hizo pay stubs ilikuwa ya uongo?

Vyovyote vile, bado ni jambo muhimu na la lazima kwa sisi walipa kodi kujua hela zetu zinatumiwaje.

Hiyo ni kwa sababu hela ni zetu na si zao. Magufuli tunakulipa mshahara shilingi ngapi? Na marupurupu yako mengine nayo ni shilingi ngapi?

Halafu nitoe wito kwenu nyie wabunge...piganieni kuunda sheria ya uwazi katika matumizi ya kodi za wananchi ikiwemo kuweka wazi malipo yote ya viongozi wa umma.
 
Vipi....tulidanganywa?

Au ndo lishapita kama upepo......
 
Nyani ngabu kumbuka hilo tukio lilitokea pale clouds tv ktk kipindi cha 360 siku ya tar.01/04/2016. Ukikumbuka siku hiyo tar.01April huwa na matukio gani hupati shida...!!
Aliongea hayo wakati wa pasaka akiwa kule kwao Mwanza. Haikuwa tarehe 01.04.2016.
 
Back
Top Bottom