Pay stubs za mshahara wa Rais

Pay stubs za mshahara wa Rais

Rais Magufuli, wakati akiwa mapumzikoni huko Chato, iliripotiwa akinukuliwa kuwa akirudi Dar atatoa pay stubs za mshahara wake ili Watanzania anaowatumikia waujue.

Mpaka kufikia sasa, licha ya yeye kurudi Dar kwa zaidi ya wiki mbili sasa (niko tayari kusahihishwa maana siikumbuki vizuri tarehe aliyorudi), sijasikia wala kuona popote pale ambapo hivyo vitu alivyoahidi kuvitoa, kuwa kavitoa.

Naona hata watu walio wengi washasahau tena maana suala lenyewe hata halijadiliwi tena. Ni kama vile lishasahaulika....limekuwa upepo uliokwishapita.

Mimi hili suala siwezi kulisahau na msimamo wangu bado uko palepale. Watanzania walipa kodi wana haki ya msingi kabisa ya kujua pesa zao zinatumikaje.

Kwenye matumizi ya pesa za walipa kodi uwazi ni jambo la lazima.

Nasubiri kuziona hizo pay stubs za mshahara wa rais na asiishie hapo tu. Atuambie malipo yake yote yanayogharamiwa na walipa kodi.

Naamini yeye akifanya hivyo basi hata viongozi wengine wa umma nao wataufuata mfano wake.

Tuilaumu media pia kwa kutomkumbusha Rais au wabunge ili waweze kuhoji, kama yeye amesahau basi ilitakiwa akumbushwe alafu tuone kama hatotoa
 
Ni kweli.

Watu wenyewe hata hawajali.

Ukiuliza kuhusu malipo ya rais wenzio wanakuuliza 'wewe mshahara wake unakuhusu nini'.
 
Hilo ni tatizo, hatuna development ya habari, matukio mengi yanafunikwa tena ya msingi sana kwa sababu tumekuwa kama homa za vipindi, likiibuka hili watu wanasahau yote

Lakini tungekuwa ni watu makini naamini tungekuwa tunamaliza matatizo mengi sana hata kama matukio yapo mengi kiasi gani
 
tatizo kubwa watanzania wengi na viongozi wa serikali wanaishi na kuongoza nchi kwa hisia..kwaivo jambo likitokea linafunika mambo muhim ya nyuma.
na hii ni hatari sana coz nchi itaongozwa kwa hisia na sio mipango madhubuti
 
Hilo ni tatizo, hatuna development ya habari, matukio mengi yanafunikwa tena ya msingi sana kwa sababu tumekuwa kama homa za vipindi, likiibuka hili watu wanasahau yote

Lakini tungekuwa ni watu makini naamini tungekuwa tunamaliza matatizo mengi sana hata kama matukio yapo mengi kiasi gani

..tatizo lingine ni kuwa wa-Tz hatujui haki zetu.

..wananchi wangekuwa wanafahamu haki zao basi wasingeivumilia ccm miaka yote hii.
 
Rais Magufuli, wakati akiwa mapumzikoni huko Chato, iliripotiwa akinukuliwa kuwa akirudi Dar atatoa pay stubs za mshahara wake ili Watanzania anaowatumikia waujue.

Mpaka kufikia sasa, licha ya yeye kurudi Dar kwa zaidi ya wiki mbili sasa (niko tayari kusahihishwa maana siikumbuki vizuri tarehe aliyorudi), sijasikia wala kuona popote pale ambapo hivyo vitu alivyoahidi kuvitoa, kuwa kavitoa.

Naona hata watu walio wengi washasahau tena maana suala lenyewe hata halijadiliwi tena. Ni kama vile lishasahaulika....limekuwa upepo uliokwishapita.

Mimi hili suala siwezi kulisahau na msimamo wangu bado uko palepale. Watanzania walipa kodi wana haki ya msingi kabisa ya kujua pesa zao zinatumikaje.

Kwenye matumizi ya pesa za walipa kodi uwazi ni jambo la lazima.

Nasubiri kuziona hizo pay stubs za mshahara wa rais na asiishie hapo tu. Atuambie malipo yake yote yanayogharamiwa na walipa kodi.

Naamini yeye akifanya hivyo basi hata viongozi wengine wa umma nao wataufuata mfano wake.

MMatumbi hapa katika ubora wako, eti msimamo wako uko pale pale mshahara wa mtu ni siri ya mtu unang'ang'ania kujua mshahara wa mwanaume mwenzio unataka kumpa nini? Mshahara ni siri yake akipenda kukupa atakuonyesha ila sio lazima na ongea nae vizuri atakwambia tu malipo yake yote kwani nini?
 
Hapana.

Si mishahara yote ni siri.
 
Huwezi kuona tija yake kwa sababu ya kikomo cha upeo wako.

Unajua wewe ni Platnum member humu sasa mshahara wa JPM hauna tija yoyote Zaidi ya tabia zetu za kung'ang'ania watu badala ya kushika policy na hoja. Some times mods walitakiwa wawe wanashusha watu madaraja kutokana na vile wanavyochangia.

Unaelekezwa yapo mambo ya muhimu Zaidi kuliko pay stubs lazima itakuwa kati ya 7-8 digits lakini wacheza soka wanapiga 9 digits kwa wiki in Tzs. Jaribu kufikiri sahihi
 
Dah!

Unasikitisha sana kwa kweli.
 
Vipi na kwenye mshahara [ambao hatuujui] nako atakatwa kodi?
 
Hii ndo imeshatoka tena!

Tulidanganywa na hakuna anayejali zaidi yangu.

Maskini Watanzania. Tunatia huruma.
 
Sasa mtu tu hata katiba aliyo apa kuilinda anaivunja waziwazi
sembuse hili la mshahara?
 
Back
Top Bottom