Paul Makonda kuiongoza Taifa Stars AFCON 2025 nchini Morocco

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ndiye ataongoza msafara wa Tanzania katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Morocco kuanzia Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani.

Hilo limethibitishwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi wakati alipotembelea kambi ya Taifa Stars nchini Misri.

“Tuna manaibu waziri wawili. Kuna mmoja ambaye mmeshamzoea, Mwinjuma (Hamisi) lakini pia sasa tuna Naibu Waziri wa pili, Paul Christian Makonda na katika mechi hizi za AFCON Morocco tutakuwa na Paul Christian Makonda,” amesema Kabudi.

Kabudi amesema kwamba Makonda ataungana na Taifa Stars kati ya Desemba 20 au 21 nchini Morocco.

Waziri Kabudi pia amewafikishia salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wachezaji, maofisa wa benchi la ufundi la Taifa Stars na viongozi wa soka walioambatana na timu hiyo Misri.
1766057301638.png
 
Hiyo timu siitaki ifungwe tu kwani mafanikio yake ni sifa kwa mtu asiyestahili ambaye anazitumia kisiasa kwa masilahi yake binafsi na hata huyo Bashite ni mtu Pariah.
 
Hakuna mechi watashinda nikupoteza muda tu.Hivi watu hawajawahi sanuka kuwa huyu kiongozi wa msafara huwa ana nuksi(Mwenyezi Mungu nisamehee).Ukiambatana na huyu mtu sahau kuhusu kuwa na mwisho mzuri

Tutafungwa na kutia aibu
 
Ila jamaa ana nyota Kali. Hizi comment za humu inaonesha jamaa hakubaliki ila yumo tu. Ila sometimes naona viongozi wanaamua kuwakera makusudi tu wananchi yan kuwaletea wasiempenda.
 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ndiye ataongoza msafara wa Tanzania katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Morocco kuanzia Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani.

Hilo limethibitishwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi wakati alipotembelea kambi ya Taifa Stars nchini Misri.

“Tuna manaibu waziri wawili. Kuna mmoja ambaye mmeshamzoea, Mwinjuma (Hamisi) lakini pia sasa tuna Naibu Waziri wa pili, Paul Christian Makonda na katika mechi hizi za AFCON Morocco tutakuwa na Paul Christian Makonda,” amesema Kabudi.

Kabudi amesema kwamba Makonda ataungana na Taifa Stars kati ya Desemba 20 au 21 nchini Morocco.

Waziri Kabudi pia amewafikishia salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wachezaji, maofisa wa benchi la ufundi la Taifa Stars na viongozi wa soka walioambatana na timu hiyo Misri.
View attachment 3517117
Huyu si ndo alitakiwa kuzungumza vya wasanii mbona yupo kimya?
 
Sisemi mengi ila matokeo yatajibu kuwa huyu kiongozi hakupaswa kwenda na Stars sababu ya....
 
Attachments

  • image_search_1766230350217.jpg
    image_search_1766230350217.jpg
    28.1 KB · Views: 9
Mungu sikia dua langu, wafungwe hawa kenge, waishie makundi
 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ndiye ataongoza msafara wa Tanzania katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Morocco kuanzia Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani.

Hilo limethibitishwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi wakati alipotembelea kambi ya Taifa Stars nchini Misri.

“Tuna manaibu waziri wawili. Kuna mmoja ambaye mmeshamzoea, Mwinjuma (Hamisi) lakini pia sasa tuna Naibu Waziri wa pili, Paul Christian Makonda na katika mechi hizi za AFCON Morocco tutakuwa na Paul Christian Makonda,” amesema Kabudi.

Kabudi amesema kwamba Makonda ataungana na Taifa Stars kati ya Desemba 20 au 21 nchini Morocco.

Waziri Kabudi pia amewafikishia salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wachezaji, maofisa wa benchi la ufundi la Taifa Stars na viongozi wa soka walioambatana na timu hiyo Misri.
View attachment 3517117
Ataondoka kwa aibu uko, maana kuna watu wanapiga mpira utafikiri wamelogwa.. 😂
 
Back
Top Bottom