WAGOSI WA KAYA - "Vinatia Uchungu"
--------------------------------------
(verse 1)
Msije mkaona watu wanapewa ridandasi,Eti mkafikiri walikuwa wazembe wa kazi. Hiyo ndiyo hali halisi hapa kwetu Tanzania. Kila mmoja kazini kwa nguvu zake amepania, kumtimua mwenzake abakie peke yake.
Mmesha mtimua mpeni madai yake, mnamzungusha hamjui mnampotezea muda wake, nyie mnadhani profesa Ludigo anatokea hapa town? Basi kwa taarifa yenu mwenzenu anatokea Lushotooo..
Mnamdanganya na Kiingereza chenu cha ugoko,Eti you know sijui, sometimes photocopy together, pailot standard sijui ma’ crossing check. Please Ludigo hebu come tomorrow, hiyo timiro timoro kuna siku n’tamminya mtu nimtoe uharo, hatielewani kiofisi mpaka tileteane kokolo.
Chonde chonde ndugu zangu mlio chuo kikuu, mkipata kazi msilete zarau na makuu, mtakuta vikongwe kazini tena wana wajukuu, wanaelimu ndogo bwana wanatembea kwa miguu.
Ole wako ufanye kazi pale miezi sita tu, halafu wakuone huyooo unaingizana na mark II, hawakawii kukwambia umeshaibia shirika, Bongo ukiwa na mark II watu wanaona umetajirika,utajiri gani huo fanyeni kazi acheni upumbavu.
Tinaomba Tanzania amani ijae makazini, pasipo na amani hapo ni uchawi na kutupiana majini, siikiza ndugu yangu nikuhadithie huu mkosi, Mama Josephine alituhadithia huu mkosi.
Bosi alimzimia halafu akamtongoza, yeye akakataa ndugu yangu akafukuzwa, hakuchukua raundi ridandasi lilimpata, sasa yuko Sahale huko na mwanae Josephine, wana kigenge chao wanauza bamia, nd’o hivyo tena Mungu anawasaidiaaa.
KIITIKIO
Wapo walofukuzwa kazi, wapo walo shushwa ngazi ah! vinatia uchungu ridandasi, hizi za majungu
x 3
(verse 2)
Khoo! I am very sorry, mimi nikiwa mzima maneno hayatoki mdomoni, lakini sasa nimekunywa naweka mambo hadharani, anayeniona mlevi anichukulie mlevi, anayenisikiliza hilo jambo liko wazi.
Hii inaonekana sana sehemu za kazi, This is too much utanipotezeaje kazi, kama ni kusoma mimi nimefika Makerere, tena kule kule alikosoma Nyerere.
Mimi sikuajiriwa kwa kufoji vyeti, wanaofanya hivyo ndiyo hao hao wanafiki, wanasababisha makazini hakukaliki, chai ya messenger vile vile hainyweki, waweza kunywa kumbe wamekuwekea kitu, unajua nini roho zao za kutu.
Wakiona unajenga wanasema eti mwizi, wanasababisha mpaka unafukuzwa kazi, hivi ni kwa nini mnakuwa wambea wambea?, au kwa sababu mnakosa hela ya bia.
Mimi nakunywa kutokana na biashara zangu, swezi kukaa kutegemea mshahara wangu, nashangaa kazini mnaniwekea majungu na vikwazo, nd’o maana nakunywa ili nipoze mawazo.
Khoo! sitapiki, naeleza ukweli na siyo unafiki, hata mkisema John Hoka analopoka poa tu, ujumbe wangu umefika.
KIITIKIO
(verse 3)
Ole wako wende kazini hufuati mambo yako, kila ukikaa ni unafiki kwa wenzako, ipo siku ukaambiwa lete cheti chako, utaanza hoo! bosi unajua, mimi nimesoma na degree za kuhonga honga mjini, lete cheti baba maneno mengi ya nini, kelele mtindo mmoja ka’soko la Ngamiani, sasa nd’o hapoo utapo tahayari.
Watu wenye tabia hii naomba mjihadhari, uongo mwingi, fix nyingi, kumbe vyeti hamna ,mna roho mbaya,nd’o mana kumbe maendeleo hamna, miji ofisi kibao imejaa ukabila, watu wajigawa mafungu sababu ya ukabila, Mtumeee! Allah akbar.
Kaombe kazi uone walivyo na dharau, kwanza watakuuliza je?, wajua Kingereza, kama so broken hapo utawaweza, ukiwajibu watakupeleka kwenye ukabila, huko ndugu yangu najua tu utateleza.
Zipo ridandasi za mashirika kuuzwa, lakini majungu nayo si ya kuyapuuza, fanyeni kazi jamani acheni majungu.
KIITIKIO...
NIMEWAMISI SANA HAWA WATU.
MASHAIRI YAO HADI KESHO YANASIKILIZIKA LOOOH JAAAMAAAANI.