Patana na mgomvi wako kabla safari CHADEMA wanafanya kosa la Lowassa wanaingia uchaguzi wakiwa na ugomvi na Serikali,vyombo vya dola,mahakama na Tume

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Kuna usemi mmoja kwenye Biblia unasema

Mathayo 5:23-24
“Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi utoe sadaka yako."

Lowasa aliendekeza ugomvi na Kikwete na kumhujumu na akagombana na CCM hakupatana nao lakini akaamua kwenda kichwa kichwa kwenye uchaguzi mkuu kugombea uraisi kilichomkuta haji kusahau

Chadema kosa hilo hilo la Lowasa wanalirudia .Wanaingia uchaguzi kichwa kichwa wakiwa na ugomvi na dharau kwa serikali,vyombo vya dola,mahakama na Tume ya uchaguzi

Nini kitawakuta tusubiri Uchaguzi mkuu.Walikuwa na kipindi kirefu tu cha kurekebisha mahusiano hawakujali .Sio kesi.Uchaguzi mkuu huu unakuja tayari.
 
Kura zinatoka kwa wananchi na siku hivyo vyombo. Ccm ndio inahitaji hisani ya hivyo vyombo ili ishurutishe kukaa madarakani.
 
Hakuna kitu cha kijinga kinachofanyika kama kufifisha demokrasia ya vyama vingi kwa kuwafanya watanzania waliofuata katiba na kujiunga na chama tofauti na chama tawala kuwa wakosaji, na kuwabagua kwa maneno na matendo. Demokrasia ya vyama vingi sio mtu bali ni dhana pana ambayo imewekwa katika jamii yetu na katiba. Wajinga hufikiria hata kuandika hivi ni ufuasi wa vyama tofauti na ccm. Nakubaliana na Askofu Bagonza kwamba pamoja na kuwa tuna utitiri wa vyuo vikuu Watanziania wamebaki wajinga kwa uwingi mkubwa. Naongezea kwamba Watanzania umaskini wao uko vichwani mwao ulikoingizwa na viongozi wa kisiasa wenye dhamana kubwa serikalini.
 
Takwimu zinasemaje?

Mwaka ambao chadema waliingia uchaguzi wakiwa na maelewano na tume, dola n.k matokeo yalikuaje?

Mwaka ambao Lowasa aligombana na tume, dola n.k matokeo yalikuaje?
 
Kisutu ana kesi kama tano na mahakama inamsubiri kwa hamu.
Speaking of kesi. Asilia kubwa ya kesi za serikal kachomoa. Sijui ni wanasheria wa serikal si competitive kweny field yao.. au kuna kitu hakiko sawa. Somehow anawazid.
Sipend alichokifanya but sitoshangaa akishinda tena
 
Wananchi ndio wenye maamuzi ya kutaka aina ya serikali waitakayo na sio hivo vyombo,hivo ni sawa na bua la mahindi Kama wananchi wakiamua.
 
Hivo vyombo vyote ni ccm na wanaonufaika ni wakuu wa hivo vyombo na sio watendaji wa chini Hawa ni wahanga wa udhalimu Kama wengine.
 
Kwani wafanyakazi serikalini,vyombo vya dola,mahakama na Tume ya uchaguzi sio wananchi? HAMTAKI KURA ZAO?

Hatutaki kura za dhuluma wala za mbeleko, bali za wananchi. Tofautisha wananchi na taasisi.
 
Speaking of kesi. Asilia kubwa ya kesi za serikal kachomoa. Sijui ni wanasheria wa serikal si competitive kweny field yao.. au kuna kitu hakiko sawa. Somehow anawazid.
Sipend alichokifanya but sitoshangaa akishinda tena
Kesi gani kachomoa maana ana kesi nyingi tu za uchochezi. Na nyingi bado hazijaisha.
Ipi ambayo ameshinda? Maana hata wadhamini wake baadhi walishajitoa.
 
Back
Top Bottom