Mtatiro: NEC inakuwa tawi la CCM, hivi uchaguzi wa kata 43 hakuna dosari za kurekebisha kabla ya uchaguzi wa wabunge?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amenisikitisha sana. Nimesoma majibu yake juu ya mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya NCCR, CUF, NLD, CHAUMMA na CHADEMA kuhusu mwenendo wa uchaguzi na hali ya kisiasa nchini Tanzania.

Ndugu Kailima amesema kwamba vyama hivyo vina hiari ya kushiriki au kutoshiriki uchaguzi na kuwa vyama hivyo haviwezi kuipangia NEC namna ya kufanya shughuli zake na kuwa NEC itaendelea na mipango yake bila kujali chochote.

Well and Good!
______________________
Kailima hajajibu hoja hata moja ya vyama vyetu na amejawa na pupa ambazo haziisaidii NEC. Tume ya Uchaguzi ni mdau mkuu wa uchaguzi, na vyama ni washiriki. Vyama vitano vimeeleza USHENZI mkubwa uliofanywa kwenye uchaguzi wa marudio wa kata 43 uliombatana na matukio mabaya kabisa;

(1) Mawakala wa vyama vya upinzani kutolewa vituoni na ama kutoruhusiwa kuingia vituoni kwa wastani wa saa 4 hadi 7 (kwenye asilimia 80 ya vituo) na waliporuhusiwa kufika vituoni wakikuta maboksi yameshajaa kura.

Walioongoza mkakati huo ni Wasimamizi Wakuu wa Uchaguzi (DED's), Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata (WRO) ambao wako chini ya usimamizi wa NEC. Na RC's, RAS's, DC's, DAS's walioko chini ya usimamizi wa Serikali ya CCM.

NEC haijatoa majibu wala kufanya tathmini ya hali hiyo, badala yake imeitisha uchaguzi mwingine wa majimbo na kata.

(2) Wanachama, wafuasi, wapenzi, viongozi na wagombea wa vyama vya upinzani wamekatwa mapanga hovyo hovyo, wamepigwa na kuumizwa sana, wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubambikiziwa.

Yako maeneo - mameya, madiwani, wabunge na wagombea walivamiwa na polisi siku moja kabla ya uchaguzi na kukamatwa - wakiwa kwenye kambi za timu za kampeni na wengine hadi leo hawajapewa dhamana, huku mashtaka wanayopewa hayana kichwa wala miguu.

NEC haijafanya tathmini juu ya hali hiyo, imekimbilia kuitisha uchaguzi mpya.

(3) Kwenye kata takribani 15, wagombea wa UPINZANI walishinda uchaguzi (takwimu zipo) lakini muda wa kutangaza mshindi ulipofika Wasimamizi wa uchaguzi wakawatangaza wagombea wa CCM kama washindi kisha polisi wakatumia nguvu kuwatawanya wananchi na kumtaka asiyeridhika aende mahakamani.

Uhuni huu unafanywa NEC ikijua kuwa huko mahakamani kesi zitaendeshwa hadi mwaka 2020 na kwamba vyama vilivyokuwa vimeshinda vitakuwa havina uwezo wa kupata haki yake.

NEC badala ya kutoa kauli juu ya UHUNI huu inasisitiza kuwa uchaguzi mwingine lazima ufanyike.

(4) Sehemu kubwa ya wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya na majimbo (ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri), ni makada wa CCM kwa waziwazi.

Makada hao hivi karibuni walielekezwa na Rais kwamba iweje walipwe mshahara, wapewe gari, wapewe ulinzi na nyadhifa hizo halafu inatokea wanamtangaza mpinzani?

Ma-DED hao baadhi yao wameonekana wakiwa wamevaa sare za CCM kwenye mikutano mikuu ya UVCCM, Umoja wa Wanawake wa CCM na Umoja wa Wazee wa CCM (Wazazi).

NEC haitaki kabisa kuzungumzia suala hili, badala yake inasisitiza uchaguzi mwingine uendelee. Uchaguzi unafanyikaje wakati ma-DED ambao ni wasimamizi wa uchaguzi tayari wao ni wanachama wa chama kinachoshiriki uchaguzi huo huo?

(5) Kata zote zilizofanya uchaguzi ambapo wakuu wa wilaya, mikoa, Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama (taasisi za serikali) zilihusika moja kwa moja na waziwazi kuhujumu uchaguzi kwa lengo la kuisaidia CCM.

Badala ya NEC na Kailima kueleza wamechukua hatua gani, wanakimbilia kutangaza uchaguzi mwingine bila kutatua matatizo ya uchaguzi uliopita.

6. NEC na Kailima wanasema vyama vinavyolalamila vipeleke malalamiko hayo kwenye vyombo vya serikali vinavyohusika ili kulalamika.

Mathalani, NEC inataka watu waliokatwa mapanga, kupigwa na kuumizwa wakashtaki polisi. Fine, watu hao walisharipoti polisi na uchunguzi utachukua miaka - lakini vyama vyetu vinaona kuwa pamoja na masuala hayo kuripotiwa kwenye vyombo vya dola, NEC inapaswa kuwa mwarobaini kwa asilimia zaidi ya 70.

NEC inajua kuwa inalo jukumu la kumuonya mtu yeyote anayeingilia uchaguzi, huu ni muda wa kukaa na vyama na wadau kufanya kazi hiyo na kuhakikisha uhuni na upuuzi uliotokea haujirudii. Je, NEC haina ofisi na ukumbi kwa ajili ya kuita wadau wake na kutatua na matatizo yake?

Je, NEC inaamini kuwa hawa polisi waliokuwa wanatumwa kupiga wapinzani bila sababu, watashughulikia malalamiko ya wapinzani ya kupigwa na polisi hao hao ambao ndiyo wapokea kesi?

Je, NEC inadhani kuwa kutolewa na kutokuwepo kwa mawakala wa vyama mbadala kwenye vituo ni suala litakaloshughulikiwa na mahakama na polisi? Kailima ana kiburi cha nini? Kailima anaamini kuwa hivi ndivyo NEC inapaswa kuwa?
__________________________________

Wito wangu ni kuwa Tanzania isifundishwe ukatili, na watanzania wasifundishwe kuwa wanyama. Siyo kweli kwamba vyama vya upinzani havina uwezo wa kutumia mabavu, uhuni, ushenzi na mbinu za kimafia za kuumizana, kutiana vilema na kujeruhi watu kwenye chaguzi, vinaweza sana!

Vyama hivi havitumii mbinu hizo kwa sababu vinaheshimu utu wa watu wa taifa hili na vinataka NEC ichukue nafasi yake, iite vyama vyote mezani, iite vyombo vya serikali vilivyohusika kwenye chaguzi hizo na kwa pamoja mjadala mkubwa ufanyike na suluhisho la kila hujuma au tatizo litafutwe, kisha NEC itangaze uchaguzi kwenye maeneo mapya huku matatizo hayo yakitatuliwa.

Vyama vya CUF, NCCR, CHAUMMA, CHADEMA na NLD vimesema kuwa kama NEC haitatui matatizo hayo haviwezi kwenda kwenye uchaguzi wa Januari 13 katika mazingira hayohayo. Vyama hivi vina hoja nzito na siyo za kubeza, hakuna mtanzania anayependa kusikia kuwa makumi ya watu wameuana kwenye uchaguzi, hakuna mtanzania anayetaka kusikia Msimamizi wa Uchaguzi amepigwa au kudhuriwa, hakuna mtanzania anayetaka kusikia ati askari wetu walipigwa na wananchi pale walipokuwa wanalazimisha kumtangaza mwana CCM aliyeshindwa.

Wanachama, wafuasi, wapenzi, viongozi na wagombea wa upinzani wanaweza kujilinda, lakini kutakuwa na madhara, vurugu, machafuko na umwagaji damu. Hatutaki tufike huko, Tanzania haipaswi kumwaga damu yoyote kwa ajili ya uchaguzi. Ndiyo maana NEC inapaswa kufanya kazi yake walau kwa aibu ili isivizoeshe vyama vurugu, mapigano, ushenzi, uhuni na rafu.

Najua Ndugu Kailima ni wakala mzoefu wa "KITENGO" na aliwekwa NEC kimkakati. Watu wa KITENGO wanajua kuwa maslahi ya vyama dola hulindwa kwa akili ya hali ya juu, siyo kupitia vitendo hivi tulivyoona kwenye kata 43. Kailima atambue kuwa kuilinda CCM hakupaswi kufanyika wazi wazi na bila aibu, yani hadi makada wa CCM wanaoshinda na nguo za kijani kila siku wanaachiwa hadhi na kazi za kuwa wasimamizi wa uchaguzi. Tusifikr huko. Kailima na wenzako amkeni na chukueni hatua. Amani ya Taifa hili italindwa tukitenda haki, haki ndiyo msingi wa amani ya taifa lolote.

Usiku mwema.

Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
The Civic United Front (CUF),
12 Disemba 2017,
DAR.
 
Wel said!!
Hata kukemea tu NEC imeshindwa.
Hata kulezea wasiwasi kuhusu Ma DED kuwa returning officer wameshindwa!!
Upinzani msiumize wananchi,waachieni angalau chaguzi hizi marudio wafanye vile wapendavyo!!
 
Mtatiro anapata wapi moral authority ya kunyooshea kidole Nec,wakati yeye aliongoza kikao cha kumtoa lipumba kwenye kupiga kura alinyoosha mikono miwili?
 
Mtatiro et al.
When are you guys going to start being pragmatic in your approach?

Nendeni mahakamani huo ndio utaratibu, hivi mnategemea kweli NEC wataacha kufanya shughuli zao kwa sababu ya matamko ya UKAWA which is not even a registered political party?

Mbona hivi juzi mahakama imetoa haki kwa wabunge 8 wa CUF waliofukuzwa...

Acheni kupoteza mda.
 
Mtatiro Siku hizi anapauka Kichwani!

Kama mmeona kuna dosari kwny Uchaguzi wa kata 43 Katiba imewaelekeza kwenda Mahakamani sio kulia lia kwenye Tweeter na Instagram na Facebook

Mnasema Sheria haziruhusu kupinga Ushindi wa Urais Mahakamani jee Sheria imewakataza kupinga Ushindi wa Madiwani Mahakamani?
 
Mtatiro et al.
When are you guys going to start being pragmatic in your approach?

Nendeni mahakamani huo ndio utaratibu, hivi mnategemea kweli NEC wataacha kufanya shughuli zao kwa sababu ya matamko ya UKAWA which is not even a registered political party?

Mbona hivi juzi mahakama imetoa haki kwa wabunge 8 wa CUF waliofukuzwa...

Acheni kupoteza mda.
Angalia dhamira ya matendo yaliyotokea,angalia hatua zilizochukuliwa kwa mapungufu yaliyotokea.Connect dots na uone je ilikuwa ni bahati mbaya au a well coordinated plan?
Katika mazingira kama hayo wakati mwingine it is better to look for another avenue (boycott and let them be players,referrees and linesmen).
Ni dharau kwa Taifa kutokukemea yaliyotokea!!!
 
Umesema vema, kuna watu wana ongea neno uzalendo na umoja wa kitaifa,kwa mazingira haya ya kihuni?! Dhuluma?!Tuseme hapana Tanzania ni yetu sote,wanatuharibia nchi!
 
Kwa hali ilivyo TUME YA UCHAGUZI tuliyo nayo viongozi wake ni makada Wa CCM tusitegemee uchaguzi ulio huru.
 
Ndio maana nikaweka neno mora authority,katafute tafsiri yake
I don't give a shit, unajaribu kutetea NEC kwa makosa ya Mtatiro, ni udhaifu mkubwa!!!
Kwanza zijibiwe hoja za wapinzani zilizotolewa kwa NEC,
Matatizo ya Mtatiro na Lipumba ni mada nyingine unayoweza kuianzishia uzi wake na sio kuchanganya mambo hapa.
Matatizo au makosa ya Mtatiro kwa Lipumba hayahalalishi 'madudu' ya NEC!!
 
Angalia dhamira ya matendo yaliyotokea,angalia hatua zilizochukuliwa kwa mapungufu yaliyotokea.Connect dots na uone je ilikuwa ni bahati mbaya au a well coordinated plan?
Katika mazingira kama hayo wakati mwingine it is better to look for another avenue (boycott and let them be players,referrees and linesmen).
Ni dharau kwa Taifa kutokukemea yaliyotokea!!!
Hii ndio tume iliyosifiwa na mtatiro kwamba imeweka mazingira mazuri uchaguzi uliopita mpaka CUF wakapata majimbo mengi. Hapo alikuwa anamjibu lipumbwa kuwa hana umuhimu CUF baaba ya lipumba kuwakimbia CUF kabla ya uchaguzi MKUU uliopita. Leo anasema tume haitendi haki. Awamu hii kila ngoma itachezwa.
 
I don't give a shit, unajaribu kutetea NEC kwa makosa ya Mtatiro, ni udhaifu mkubwa!!!
Kwanza zijibiwe hoja za wapinzani zilizotolewa kwa NEC,
Matatizo ya Mtatiro na Lipumba ni mada nyingine unayoweza kuianzishia uzi wake na sio kuchanganya mambo hapa.
Matatizo au makosa ya Mtatiro kwa Lipumba hayahalalishi 'madudu' ya NEC!!
Mkuu punguza basi povu.mambo haya hayataki kujibiwa kibavicha
Hoja za wapinzani zinajibiwa mahakamani,wana siku 30 za kukata rufaa kwa nini wasikimbilie mahakamani,badala yake wanakujua kukuzuzueni bure tu
Kesi za uchochezi mnawekeana mawakili 50,lakini kesi za kikatiba kama hizi,mnaleta usanii,kulia lia hakutawasaidia,uchaguzi upo pale pale
 
UKAWA mgetusaidia, mnatumia vifungu vipi vya sheria kuwataka NEC kuahirisha uchaguzi maana mna wasomi wengi tena wanasheria, NEC washasema wanatakiwa si chini ya siku 20 na zaidi ya siku 50 wawe wamefanya uteuzi wa Wagombea kuziba nafasi wazi za Ubunge na nyie toeni vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka ya kuishurutisha NEC kusimamisha uchaguzi uliokwisha Tangazwa kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom