Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Sept 9, 2020, ataenda Mahakamani kwenye kesi zake Kampeni zikiisha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Leo, Septemba 9, 2020 - mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Ndg. Tundu A. Lissu anaongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari.

Haya ni baadhi ya aliyoyasema:

======

Waandishi mmekuwa mnogopa kuni-cover, nikizungumza mna switch off. Hofu!

> Nazungumza na Vyombo vya Habari vya nje ya nchi kila baada ya siku tatu, lakini sio vya ndani. Sio kwamba kwa sababu hamtaki kuniskia ila kwa sababu mnaogopa consequences za kuni-cover.

> Niko sawa sawa kiafya isipokuwa mguu mmoja haukunjiki. Lakini hii hainizuii kufanya shughuli zangu.

> Uchaguzi Mkuu huu ni muhimu kuliko uchaguzi meingine wowote kuwahi kutokea nchini. Tangu mwaka 1958 tumekuwa tukiongozwa na chama kile kile chenye misingi ile ile.

> Vyovyote itakavyokuwa baada ya tarehe 28 mfumo wa uongozi hautakuwa sawa na miaka iliyopita, kwani Magufuli na chama chake wamesema wataondoa vizingiti ‘time limit’ vya uongozi kwa miaka 10 hivyo ratiba zitabadilika hivyo utawala mpya wa Magufuli utakuwa na dramatic consequences.

> Kuna viashiria vingi vya kuturudisha kiuchumi (uchumi dola) miaka 35 baada ya kuondokana nao, kwani hata ujenzi wa sehemu nyingi unajengwa na Suma JKT

> Tunarudi kwenye mfumo wa mwaka 1962 ambapo Rais ndio Alpha na Omega akisema Jambo basi linafanywa kama alivosema mfano jana amesema “Varabara ianze kujengwa” na ikaanza mara moja

> Kampeni zimenza na awamu ya kwanza tumeshamaliza ambapo tumefanya uzinduzi wa kampeni kwa siku 10 na tumemalizia Zanzibar Awamu ya pili tutaianza kesho

> Mikutano yetu haijaalikwa kwa kutumia magazeti kwa sababu magazeti yanatuogopa, sio kwa kutumia radio kwa sababu zinatuogopa na wala si kwa TV kwa sababu zinatuogopa tumealikana kwa kutumia WhatsApp.

> Tulichojifunza kwa siku hizi kumi tumejifunza kuwa kuna kiu kubwa sana ya mabadiliko. Japo media zilikuwa hazifanyi coverage hivyo tulikuwa tunaalikana wenyewe kupitia makundi ya WhatsApp

> Mikutano yetu imekuwa ya watu wanaokuja kusikiliza hoja za mikutano yetu na sio kuletwa kuja kuongeza idadi ya vichwa. Namnukuu Nama Maria Nyerere alivyosema “Nimeletwa tu kama wengine kuja kuongeza idadi ya vichwa”

> Hivyo watu wetu walikuja kwa hiari na hawakuletwa wala hatukutuma roli au trekta kuja kuwaleta bali walikuja wenyewe

> Pamoja ya kuenguliwa ki historia kwa wagombea wetu iwe madiwani au wabunge, lakini wagombea waliobaki wana nafasi ya kushinda.

> Baada ya miaka mitano ya kuzuiliwa kufanya siasa, kuteswa na kuburuzwa mahamani walijua CHADEMA itakufa lakini bado ina nguvu

> Pamoja na kila aina ya ugumu ambao tumewekewa, matatizo ya kifedha na engua engua, tuna uhakika wa kuiondoa CCM madarakani

> Hatujidanganyi hakuna anaejidanganya kwa kazi iliyo mbele yetu ni kubwa kwelikweli. Mimi binafsi nimeshiriki chaguzi za vyama vingi tangu1995 nilivyotoka tu chuo nafahamu jinsi ilivyo ngumu kushinda uchaguzi dhidi ya CCM katika nchi hii

> Na mwaka huu itakuwa ngumu zaidi kwa sababu mfumo wetu wa Tume hauko huru kwani Tume inakipendelea waziwazi chama kilichopo madarakani

> Tume ndo hiyo ya watendaji wote wa Rais ambao wanaweza kuondolewa muda wowote madarakani na Rais.

> Wakurugenzi wote na wote walio chini yao ni wateule wa Rais hivyo tuna mfumo ambao haujawahi kuwa huru

> Na Uchaguzi wa mwaka huu ndio haupo huru zaidi ya ule wa 2015 kutokana na pressure wanayoipata huko

> Maaskari na Usalama wa Taifa hawapo upande wetu na watumishi wote hawapo upande wetu na ndio maana tunasema kushinda Uchaguzi huu ni kazi ngumu. Lakini watanzania wapo tayari kwa mabadiliko na hata huko kwenye mikutano wanasema wako tayari kwa mabadiliko

> Hatutakubali tukishinda tusitangazwe. Hatutakubali kuibiwa kura! Hatutakubali twende kwenye uchaguzi tukiwa hatuna wakala wakati tumejiandaa.

> Kama mgombea wetu amechaguliwa tuna uhakika wa fomu kutoka kwenye vituo halafu hajatangazwa, tutaingia barabarani kupigania haki zetu.

> Tutakuwa na utaratibu ambapo mawakala wetu watakuwa na kituo cha kukusanyia matokeo kutoka vyanzo vyetu. Na tutajua tumeshinda au tumeshindwa and we will act accordingly.

> Sheria inasema kila chama kinachoshiriki uchaguzi kina haki ya kuwa na wakala lakini mmeshuhudia kwenye chaguzi za marudio mawakala wetu ilikuwa ngoma kuapishwa, ilikuwa ngoma mpaka Akwilina Akwilin akauawa na itakuwa ngoma mwaka huu pia.

> Sheria inasema mawakala watapewa nakala za matokeo lakini mwaka huu Tume imekuja na Kanuni kuwa mawakala watapewa nakala kama zipo. Huko ni kutafuta ugomvi na wataupata!

> Tunaitaka Tume ichapishe nakala za kutosha kwa idadi ya wagombea wa urais na ubunge kusiwe na sababu ya kusema nakala hazikutosha.

> Kama mgombea wetu amepita na tuna ushahidi wa nakala za kura, tutaingia barabarani na tutadai haki yetu. Tunataka tushindwe kihalali, tukishindwa kihalali tutakubali lakini endapo tutaibiwa na kunyang’anywa ushindi hatutakubali

> Kitu kinachohitajika hivi sasa kwa Tanzania ni kuvunja huu mfumo ambao umekuwepo toka ukoloni. Mfumo wetu wa utawala ukiungalia sawasawa unashabihiana na mfumo wa kikoloni kuliko ule wa Kenya na Uganda. Mfumo wetu ni wa kikoloni unahitaji kubadilishwa fundamentally kama usipobadilishwa hatutafanya kitu!

More:
> Tangu tumepata uhuru tumekua na ndimi mbili kuhusiana na lugha na ndimi mbili ni hatari

> Ulimi mmoja tumesema Kiswahili ni lugha ya Taifa na tumeiendeleza kwelikweli

> Ulimi wa pili tumesema Kiswahili si lugha ya kufundishia

> Sasa fikiria tu huo muda anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anaenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vile vile

> Kwa kifupi watu wetu hawajui kiingereza

> Mimi ni wakili, majaji wengi hawajui kiingereza, ukienda nchi za wenzetu huko mtanzania akiongea unatamani kuongia uvunguni mwa meza.

> Kiingereza chetu ni kibaya. Sio kwa sababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa sera ya lugha

> Ukiniuliza mimi, honest opinion nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya Lugha

> Tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani ‘language of instruction is everything’

MASWALI:

1) Umezungumza kuwa Serikali iliyopo madarakani inadhibiti usishinde katika uchaguzi wa mwaka huu, na miongoni mwa hoja zilizopo mtaani ni kuwa wanakudhibiti kwasababu unatumika na mabeberu. Je wewe unatumika na mabeberu? Na kama sivyo tutaamini vipi?

2) Umesema kuwa katika mikutano 10 mliyofanya inaonesha dalili ya ushindi kwa CHADEMA, lakini tumeona mitandaoni baadhi ya picha zilizotumika sio za kweli na zimesambazwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, zimetolewa katika mikutano ya mwaka 2015. Je, tunawezaje kuamini ushindi wenu wakati mnatumia propaganda kuonesha kukubalika?

MAJIBU:

> Kwanini tunaomba michango? Tunaomba michango kwasababu hatuna pesa, CCM wanajichotea pesa mnataka tuseme wanachotaje? Someni kitabu cha Mkapa. Sasa sisi CHDEMA hatuna hiyo privilege lazima tuchangishe!

> Mimi nimefukuzwa kazi na sijalipwa pensheni napata wapi pesa ya kuendeshea kampeni? Lazima wananchi wachangie chama chao.

> Sisi watanzania tunaona kama kuomba ni kujidhalilisha lakini ndio njia ya kuendesha hizi Siasa na Vyama vya Siasa kwa hiyo lazima tuombe na tunazihitaji hizo pesa kwelikweli
====

> Mabeberu: Jibu langu ni rahisi sana - Nani ni beberu? Mkinipa hilo jibu, we are good to go. Kama mabeberu ni Marekani, ndo wanaoifundisha Jeshi la Taifa. Madawa ya UKIMWI yote yanatoka kwao, hawa ndio wanatoa misaada nchini. Je, ni mimi ninatumika na mabeberu ama Serikali ndio inatumika na mabeberu?

> Magufuli ameharibu urafiki wetu na nchi nyingine, na sisi ndio tutarudisha uhusiano mzuri na kimataifa. Miaka mitano ya Magufuli nani anayemiliki migodi ya madini? Ni haohao mabeberu!

> Magufuli amewaita mabeberu lakini bado anaenda kuwaomba msaada sasa mimi kwenye serikali yangu nita repair huo urafiki uliopotea

> Serikali yenu inawaita mabeberu lakini bado mnatumia madawa yao, mnaomba mikopo pesa za kusomeshewa nje zinatoka wapi? Madini yetu yanamilikiwa na nani? Migodi yetu inamilikiwa na nani? Mgodi wa Geita ambao ndo mkubwa kuliko yote unamilikiwa na nani?

> Mimi nitarudusha diplomasia na mataifa ya nje

KUHUSU PICHA: Sifahamu hizo picha zilitokea wapi ila naweza kusema kuwa hatuhitaji hizo picha maana uwanja tunaweza kuujaza

> Serikali inapambana na ufisadi; wakamkamata Deo Mwanyika akawekwa huko gerezani. Leo hii Deo ni mgombea ubunge kupitia CCM halafu mnasema Serikali inapambana na ufisadi?

> Nasubiri Magufuli aende Njombe nione atamuinuaje mkono mhujunu uchumi yule(Deo Mwanyika)

> Kuna wakandarasi hawajalipwa fedha zao kwa miaka 5 sasa, wanalisha majeshi wanalisha Magereza wanawambia tunahakiki malipo


Swali:
Ndugu Lissu una kesi 6 mahakamani na mahakimu wa Kisutu wanakusubiri ufike mahakani kujibu kesi zako. Wadhamini wako wanajibu kuwa upo kwenye kampeni za urais. Je, wewe msimamo wako ni upi katika hili?

Lissu:
Mimi ni mgombea urais mahakama ya Kisutu haiwezi kunisubiri mimi nimalizane na hii biashara ya kampeni inayokoja mara moja baada ya mika mitano? Na ipo kikatiba

Kama mahakama imeweza kusubiri miaka 3 niliyokuwa nje, isubiri pia hii miezi miwili sasa hivi nafanya hili tendo la muhimu kikatiba

> Tutakutana mahakamani baada ya tarehe 28 Oktoba. Na mimi siziogopi hizo kesi na kudhihirisha hilo ndo maana nimerudi nchini.

> Kama nitashinda urais tutafuata taratibu kwani naapishwa kwa Katiba Npya? Katiba inasema Rais hatashtakiwa kwa kosa lolote akiwa madarakani lakini mimi kesi zangu zipo kabla sijawa Rais hivyo haziwezi kufutwa

> Hutajua jinsi nchi hii ilivyo sio ya haki mpaka ukikamatwa...

> Mimi nimelala Segerea mara nyingi na naweza kukwambia kuwa watu wengi waliopo gerezani ni kwasababu ya umaskini wao. Wameshindwa kuhonga mapolisi na mahakimu!
 
Kuna haja ya huyu rais mtarajiwa aongee ajenda za uchaguzi kwa undani, hata hapo alipoongea na wahariri awaeleze japo hawataandika, kutoa story kiundani ila ujumbe wawe nao.

Kikubwa wahariri wamwambie Lissu ukweli, sheria mpya iliyotungwa na ccm dhidi ya taasisi za habari imekuwa mwiba mkali kwa vyombo vya habari hata wafanyakazi wenyewe wa media hizo wanahofu na maisha yao, so wanashtuka!.
 
Campaign za mwaka zinaenda kidigitali maana magufuli anapigwa majukwaani alafu akianza kutoa povu anapigwa Kwa press conference.....

Huyu Mzee atachezea makofi ya uso kwelikweli na ameshaanza kucheza Ngoma ya lissu kuanzia yeye pamoja na akina bashiru na polepole
 
8b8772af65a848b2211cc750a1e7211b.jpg
 
Lissu anakiri uchaguzi utakuwa mgumu, sio kwasababu ya CCM kama chama cha siasa, ni kwasababu ya Tume iliyowaengua wagombea wa upinzani bila sababu za msingi, na wasimamizi wa uchaguzi wanaoonekana kuipendelea CCM, haya mambo yatasababisha hasira zaidi kwa wapinzani siku ya kutangaza washindi, CCM wasijaribu kuiba kura, hapo ndipo hasira za wengi zitakapolipuka.
 
Shida ya lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Mkuu, mbona kishaongea mara nyingi tu.

Bima ya afya kwa kila mtanzania, haki kwa wanfanyakazi na wafanyabiashara, kuimarisha kilimo na kuwapa uhuru wakulima kutafuta masoko yao wenyewe, kuimarisha miundombinu. sekta za Madini na gas kuimarishwa na kuwanemesha wakazi wa maeneo kwanza nk. n.k.

Tofauti ni kuwa JPM yeye anaongelea specifics ... nitajenga barabara ya Nyahungwe, daraja fulani n.k
 
Shida ya lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi

Lissu hawezi kuchambua au kueleza mambo pasina kulaumu au kumshambulia mtu,hivyo ndivyo alivyo na uzuri au ubaya kuna watu wanapenda hiyo hali ya kusikia malalamiko muda wote kuliko kusikia ni nini kifanyike.
 
Acha ujinga, kwa hiyo anayotaka kutuambia atafanya nini yameisha? Kwani akisema kila siku atatufanyia nini shida iko wapi?
Huyu anaanza kupotea, arudishwe kwa nguvu kwenye mstari
kama mpaka sasa hujawahi kusikia atafanya nini basi we haupo Tanzania au kichwani hamna ubongo kumejaa samadi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom