Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,231
113,594
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
 
Passport kitu gani bhana watu wanapoteza hela ndio maana kuna Balozi kwenye hizo Nchi cha kwanza ukifika ni kutoa taarifa ili ukipata matatizo yeyote inakua rahisi wao sehemu ya kuanzia kwa wasafiri kupoteza passport ishu ya kawaida tuu unaongea kama vile upo kwa Mpalange wakati unajinasibu upo Nje...au kwa kuwa hiyo passport kapoteza mwanasiasa?
 
Passport kitu bhana watu wanapoteza hela ndio maana kuna balozi kwenye hizo Nchi cha kwanza ukifika ni kutoa taarifa ili ukipata matatizo yeyote inakua rahisi wao sehemu ya kuanzia kwa wasafiri kupoteza passport ishu ya kawaida tuu unaongea kama vile upo kwa Mpalange wakati unajinasibu upo Nje...
Duh!

Sijakuelewa aisee.
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote?

Suala la nani aliiba passport anajua aliyeiba. Inawezekana ni wale ambao hawataki arudi Tanzania.

Kuhusu kumwambia Rais, ukiacha kuwa Rais ni taasisi, anayeshika nafasi ni mtu. Kila mtu huomba msaada kwa mtu mwenye connection na kitu fulani. Kama wewe una jamaa uhamiaji kwani ni shida kuomba msaada? Sasa yeye kakutana na mtu mwenye nafasi ya juu, na inawezekana alikuwa anakataliwa kupewa passport nyingine. Kaomba msaada kwa mtu mwenye connection naye.
 
Passport kitu bhana watu wanapoteza hela ndio maana kuna balozi kwenye hizo Nchi cha kwanza ukifika ni kutoa taarifa ili ukipata matatizo yeyote inakua rahisi wao sehemu ya kuanzia kwa wasafiri kupoteza passport ishu ya kawaida tuu unaongea kama vile upo kwa Mpalange wakati unajinasibu upo Nje...
Sasa raiis anatoa passport? Kwani utaratibu hsufahamiki? Namwona samia akicheza na nyani.
 
Kwamba huelewi anaposema ameibiwa passport? Kama aliibiwa mkoba wenye passport, leseni, pesa, nguo za ndani, kitabu cha katiba ya chama chake na vitu vingine, je alipaswa avitaje vyote...
Taratibu za kupata passport mpya kama uliyokuwa nayo imepotea, zipo wazi.

Kwanini uombe msaada wa Rais?

Kama alikuwa anakataliwa, alikuwa anakataliwa kwa misingi gani?

Bado sielewi aisee!
 
Tundu Anthipas Lissu ni mwanasheria na msomi. Sina wasiwasi kuwa alishafuatilia taratibu zote, lakini mamlaka zinazohusika haziwezi kufanyia kazi maombi yake kwa hofu iliyojengwa na watawala hasa utawala uliopita wa ile awamu ya giza.

Waliomwibia Lissu passport yawezekana walitumwa kumdhuru na/au kumwibia nyaraka mbalimbali anazofanyia kazi. Nina imani kuwa hizo nyaraka na passport zipo Tanzania zimekaa tu mezani kwa mtu.

Kwa mazingira hayo, ilifaa Lissu apeleke ombi lake kwa Rais ambaye anaweza kutoa tamko tu na wahusika wakaondoa hayo mambo machafu yanayoendelea kuiweka Tanzania katika zama za ujinga na giza.
 
Jamaa amepagawa, mwanzo alisema anarudi TZ mwezi wa 3 sijui wa 5, leo anaomba Rais amhakikishie usalama wake ili arudi. Badala ya kuzungumza na Rais mambo ya msingi kama anavyoropoka akiwa huko kwa space amefyata anaomba vitu vya kitoto mno.
Tuache siasa, hujui hata alisema atarudi lini. Waacheni wapinzani wahoji serikali, ambako kuhoji kwake waita kuropoka, uliyepo madaraka uwe waleta majibu sahihi.
 
Kuna logic! Labda siku moja atakuja kusimulia. Taratibu ni nyepesi sana, ila yamkini kwake kulikuwa na shida.
Hiyo shida ni nani sasa aliyekuwa anaileta? Na alikuwa anaileta kwa maagizo kutoka wapi? Juu? Katikati? Chini?
 
Tundu Anthipas Lissu ni mwanasheria na msomi. Sina wasiwasi kuwa alishafuatilia taratibu zote, lakini mamlaka zinazohusika haziwezi kufanyia kazi maombi yake kwa hofu iliyojengwa na watawala hasa utawala uliopita wa ile awamu ya giza...
Duh!
 
Back
Top Bottom