Paskali Mayala, mbona huleti "analysis" ni nini zitakuwa athari kisiasa za uamuzi wowote kesi ya Mbowe?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Kwa kweli kaka yangu ninakuaminia sana kwa kufanya uchambuzi. Hata hivyo ukimya wako kuhusu kufanya uchambuzi na utabiri wa nini itakuwa athari kisiasa kuhusu uamuzi wowote utakaohusisha kesi ya Mbowe.

Kwa mfano kwa sasa tunasubiri iwapo Mahakama itaamua Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu na ikafikia hadi hatua ya utetezi athari zake zitakuwa ni zipi?

Baadaye wanajitetea na mwishowe utetezi wao unakuwa hauna mashiko then wanafungwa, hapo athari za kisiasa katika nchi hii na Mbowe mwenyewe zinakuwaje kwa uamzui huo?

Au inatokea wanajitetea na Mahakama inaona hawana hatia hapo pia kisiasa Mbowe na siasa za nchi kwa ujumla inakuwaje?

Au inawezekana pia DPP akaingia "nolle" ya ghafla ghafla ghafla tu hapo athari kisiasa kwa Mbowe na nchi kwa ujumla inakuwaje?

Kwangu mimi hakuna ubishi kabisa kuwa kesi hii ni ya kisiasa! Kila MTanzania anayefuatilia siasa zetu kwa umakini analijua hilo - na utabiri wangu iwapo Mbowe na wenzake watafungwa basi ninaamini siasa za nchi hii zitakuwa zimenoga zaidi kwani kwa muda wote Mbowe atakaokuwa gerezani watu wanakuwa wakiongelea yeye tu.

Watazidi kuchambua uamuzi uliomfunga na proceedings hizi zinazoendelea na pia watazidi kuilaumu Serikali inayoongoza kwa unyanyasaji, uonevu na mtazamo hasi kwa upinzani. Serikali haitakuwa na Amani na watoa maamuzi hayo pia hawatakuwa na Amani maisha yao yote.

Watu wataondoa hofu watajihisi kuwa Mtawala akiamua kukufunga hata kama huna makosa anakufunga tu! Akifungwa Mbowe itakuwa ni chachu ya kuimarisha zaidi upinzani wa nchi hii.

Iktokea Mbowe kaachiwa katika hatua ya "nolle" kabla ya kufikia hatua ya wao kuwa na kesi ya kujibu basi Jamhuri itakuwa imepunguza aibu ambazo itaenda kupata kwani inaonesha hatua ya utetezi inaweza ikaibua mauzo mengi kwa upande wa washtaki katika kesi hii.

Kwangu mimi kwa Jamhuri ni bora wasivuke hatua ya kuwa hawa mabwana wana kesi ya kujibu kwani aibu haitakuwa kubwa sana na hata kisiasa awamu ya sita itaonekana kama yenyewe ndiyo imeamua kufikia muafaka na upinzani.

Hayo ni mawazo yangu - Je, ndugu yangu Paskali Mayala wewe unalichambuaje suala hili?
 
Tafuta pesa usaidie familia yako.

Ukiona matokeo yote unayohisi, wewe hujihusishi ujue hakuna kitakachoendelea. Hata kama Mbowe akifungwa, Maisha yataendelea kama kawaida.

Hakuna mbongo Yuko tayari kuumia kwasababu ya mtu. Wabongo Ni mabinhwa sana wa MIHEMKO na USHABIKI.

KILA mtu anataka akiamka, anaoga anavaa vizuri, ana pesa ya bando, baadaye anakaa kwenye viti virefu anashabikia tu huko Twitter.

" Duuh, aisee, makamanda ni noma Leo wamekinukisha balaaa.........😀

Au unakaa unawaza Mara Wazungu sijui watasaidia Nini, hakuna kitu.

Kwa lugha rahisi Ni kwamba watawala wanna uwezo wa kufanya chochote na wewe hakuna kitu utafanya zaidi ya kununua kibando kulalamika mitandaoni.
 
Kwani amekuomba hela ya kula au ya kulipia wanawe ada ya shule? Unaonyesha jinsi gani ulivyo mpumbavu usikute hapo unaishi kwa dada yako hata kupanga kachumba kamoja unashindwa. Kumbe ni kweli kuwa sifa kubwa ya kuwa CCM ni kujitoa ufahamu.
 
Du! Yaani umejiongelea ulivyo kabisa - Acha ubaki hivyo!

JamiiForums313878302.jpeg
 
Tafuta pesa usaidie familia yako.

Ukiona matokeo yote unayohisi, wewe hujihusishi ujue hakuna kitakachoendelea. Hata kama Mbowe akifungwa, Maisha yataendelea kama kawaida.

Hakuna mbongo Yuko tayari kuumia kwasababu ya mtu. Wabongo Ni mabinhwa sana wa MIHEMKO na USHABIKI.

KILA mtu anataka akiamka, anaoga anavaa vizuri, ana pesa ya bando, baadaye anakaa kwenye viti virefu anashabikia tu huko Twitter.

" Duuh, aisee, makamanda ni noma Leo wamekinukisha balaaa.........😀

Au unakaa unawaza Mara Wazungu sijui watasaidia Nini, hakuna kitu.

Kwa lugha rahisi Ni kwamba watawala wanna uwezo wa kufanya chochote na wewe hakuna kitu utafanya zaidi ya kununua kibando kulalamika mitandaoni.
Wewe mkaruka kwa mchango wako huu unatuthibitishia kuwa wewe unachowaza kwenye akili yako ni kupata mali (fedha) kwa gharama yoyote hata kama ni katika dimbwi la damu za watu, maangamizi na mparaganyiko wa taifa letu

"kwako wewe hela ni bora kuliko utu, haki, amani, na ustawi bora wa taifa letu".

Hata kama wewe ni mwana ccm, mchango wako huu hauwezi kukubalika kwa wenzako maana ni kuendeleza sura mbaya zaidi, haujali mshikamano, umoja na utaifa, inaonekana wewe Ndiyo wale vijana sampuli ya Sabaya, Musiba, Makonda nk..wanaotaka utajiri kwa kuharibu maslahi ya taifa.

Ikutoshe tu wewe kubadilika na kuwa na mtazamo Chanya wenye maslahi ya taifa kuliko kujivika ushetani huo kwa kisingizio cha kutetea chama.
 
Ukweli mchungu Ni kwamba hakuna wanasiasa au tajiri anapambania haki zako, sijui damu.

Wanasiasa wanaongoza kumwaga damu za watu ili kulinda nafasi zao.

Tena hili halina chama.

Wanasiasa wote WANAFANANA.

Hakuna MALAIKA.
 
Jamii inazidi kuelimika ukumbuke
 
Bahati mbaya hata hizo hela hana
 
Ukweli mchungu Ni kwamba hakuna wanasiasa au tajiri anapambania haki zako, sijui damu.

Wanasiasa wanaongoza kumwaga damu za watu ili kulinda nafasi zao.

Tena hili halina chama.

Wanasiasa wote WANAFANANA.

Hakuna MALAIKA.
When you concede to argue with a fool he will bring you down and beat you due to his experience!
 
Back
Top Bottom