Pasco na waandishi wenzako...

myhem, Pasco wa jf ni Pasco wa Jf, na Pascal Mayalla ni Pascal Mayalla, wote ni waandishi mmoja Pasco ni mwandishi wa jf na Pascal Mayalla ni mwandishi wa kiukweli.

Hapa jf tunazosheria zetu tulizojiwekea, hairuhusiwi kumfananisha membe yoyote humu na mtu mwingine hata kama unamfahamua kuwa ndiye yeye, hili ni kosa liitwalo 'Name Calling' na adhabu yake ni ban!.

Hiyo ban kampige mkweo! mi sioni kosa langu hapo.
 
Mkuu Pasco mzee wa majungu bado uko msibani huko Arumeru njoo utupe maelezo ya mapenzi yako na bahasha unazo gawa tafadhali .
Mkuu Lunyungu, kweli wewe ni wa kuniita mimi mzee wa majungu!, of all the people hata wewe?!. Anyway baada ya thread hii kuchafuka kwa kumchanganya member mwingine isiyehusika, nimepandisha thread maalum ya waandishi na bahasha na wewe ukiwa ndio mchokoza mada!.
 
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako .Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku .Ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi .

Heshima yako mkuu hebu saidia.

Mkuu Lunyungu,

Shalom.

Sikubahatika kabisa kukuona hapa, kwa vile haya yamewatokea waandishi huko Arusha, na Matinyi ni rafiki yangu, nasikitika sana kwa hayo, tembelea hapa ili tuumalize huu mjadala. https://www.jamiiforums.com/habari-...a-sio-kila-bahasha-ni-rushwa-pasco-wa-jf.html

leo nitamalizia.

Pasco.
 
Mkuu....
pasco ni mwanadamu....ana familia inamtegemea....
pasco na wenzake maslahi yao ni duni......huu ni wakati wa pasco na wenzake kuutumia.....
nategemea wakina pasco nao waendeshe mikoko ya bei juu...watoke kwenye nyumba za kupangisha mabondeni...wahamia kwenye nyumba zao sala sala.....
Kazi ya uandishi wa habari ni kazi ya wito, kama ualimu, commitment yetu ni kuihabarisha jamii na sio kazi ya maslahi, waandishi wa ukweli usafiri wetu ni daladala, hakuna mwandishi wa ukweli mwenye tamaa ya mkoko achilia huo wa bei juu, na nyumba za kupanga ndio nyumba zetu!
 
Nimefuatilia hii topic kwa umakini mkubwa na bado sijaelewa, kwamba tuhuma hizi ni za Pasco kama Pasco ama Pasco ametumiwa tu kufikisha ujumbe. Ni kweli kwamba tuna waandishi ambao wanafahamika kuwa ni "waandishi wa bahasha" na wapo waandishi makini wanaofanya kazi zao kwa kuzingatia maadili.

Hivyo si sahihi kuwachanganya wote kapu moja. Tuangalie pia sekta nyingine, wapo polisi ambao hawawezi kukufungulia RB au kwenda kumkamata mtuhumiwa bila kuwapa chochote, lakini kuwapo kwa polisi wa aina hii hakumaanishi kuwa hakuna polisi wanaofanya kazi zao kwa kuzingatia mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.

Ni vyema wakati tukijadili tutumie maneno ya "baadhi" au "wengi wao". Na suala la specialization si suluhisho la mtu kupokea hongo. Walioingia mikataba mibovu kwa kupewa 10% ni wasomi waliobobea tena wengine wana mpaka PhD. Kwa hiyo suala la ukiukwaji wa maadili ni la mtu na si taasisi au kundi zima.
 
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako .Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku .Ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi .

Heshima yako mkuu hebu saidia.
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Mkuu Pasco shalom
Najua nikisema nawe hapa utawaambia na wenzako .Hivi hii tabia ya kupewa bahasha ndiyo habari ziandikwe kwenye magazeti na TV zenu ina manufaa gani kwa Taifa ? Nasema haya nikiwa n ushahidi nitarudi baadaye kuona ushauri wako ili niendelee kumwaga mtama kwenye kuku .Ila tuna kwazika na hizi rushwa za bahasha kisa habari ziende kwa jamii utadhani hamlipwi .

Heshima yako mkuu hebu saidia.
Nawatakia waandishi wenzangu wote wa habari, maandimisho mema ya siku hii ya kimataifa ya uhuru wa habari.
P.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom