GodfreyTajiri
JF-Expert Member
- Sep 26, 2010
- 1,006
- 712
Wana JF
Nimeona kama bandiko langu wachache wananshindwa kunielewa na kuanza kuuliza maswali ya kijinga .Mimi wakati naandika hili sikujua na sikutegemea kama Pasco anakula mlungula ila kwa sababu rafikia yangu alitaka habari yake iende kwenye jamii kuhusiana na matatizo ya majanja yta moto Tanzania , basi akaambiwa anaweza pia kuwaita waandishi au aende habari na maelezo akaseme aliyo nayo .Alienda akaambiwa saa moja ni shiling 60,000 na pia lazima ajiandae kwa bahasha kama anataka habari yake itoke kwenye chombo cha habari maana bila hivyo hawataandika watamsikiliza na kukaa kimya .Ndiyo nikaja kuleta hoja hapa na kuomba Pasco asaidie maana ni mwandishi wa habari .
Sasa naomba tujikite kwenye hoja na tuache uvivu wa kusoma na kuanza kuhoji kijinga kijinga .Wachache wanafanya kila kitu siasa no hii ni serious .Kwa ninij bahasha kwanza ndipo habari iende hewani ?
Pasco tafadhali saidia maana ulisha sema unagawa bahasaha na wazipenda .
hii shida ipo kweli. hebu andaa warsha au kongomano (haijalishi ya kitaifa au kimataifa)
waandishi watakuja na bila soni watakuambia ukitaka itoke kwenye vyombo vyahabari
inabidi utoe "nauli".