Mku
u Simba Songea, kwanza asante kuangalia kipindi changu cha Saba Saba na PPR.
Pia ni kweli nilitembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuzungumza na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Ramadhan Kailima, kisha nilizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva.
Hoja zangu kuu zilikuwa 3. 1. Wizi wa Kura, 2. Uchakachuaji wa Matokeo, 3. Kukubali matokeo au kuyapinga!.
1. Wizi wa Kura.
Nlionyesha masanduku ya kura kuwa yako transparent. Kama kura hazijaanza kupigwa, masanduku yanakaguliwa na mawakala wa vyama, na hayaondoki hapo hadi zoezi la kuhesabu kura likamilike, hivyo hakuna namna yoyote ya ku temper na sanduku la kura bila kuonekana!. Ila hapa nikazungumzia unless kama kuna masanduku mengine yaliyajazwa kura zilizokwisha pigwa, yakafichwa chumbani, baada ya zoezi la kupiga kura, masanduku hayo yakaletwa kwa mazingaombwe, hivyo kura bandia kugeuzwa ni kura halali.
2. Uchakachuaji wa Matokeo.
Kwenye kila kituo kina mawakala wa vyama, wakati Tume ikitangaza matokeo ya kila jimbo, ilionyesha nakala halisi za matokeo hayo zilizosainiwa na mawakala wa vyama na kila chama kupatiwa nakala halisi, sasa kama kuna tofauti kati ya matokeo halisi ya vituoni na matokeo ya NEC, then vyama lalamishi wangeionyesha nakala zao ili umma ushuhudia uchakachuaji huo wa NEC wenye matokeo tofauti na matokeo halisi.
3. Kukubali Matokeo/Kupinga.
Kwenye hili nilisema, asiyekubali kushindwa sii mshindani. Uchaguzi ni zoezi linaloendeshwa kwa mujibu wa katiba unaozingatia sheria, taratibu na kanuni za nini cha kufanya litokeapo jambo lolote. Hapa nilijikita zaidi kwenye matokeo ya Zanzibar, Jecha alifuta matokeo yale bila kufuata, sheria, taratibu na kanuni. Lakini pia kuna sheria, taratibu na kanuni za kufuatwa, pale ambapo sheria, taratibu na kanuni zinapokiukwa. Sheria, taratibu na kanuni hizo ni pamoja na kujaza fomu ya kupinga matokeo, na kwenda mahakamani. Hakuna lolote kati ya haya lililofanyika. Kupinga matokeo hakufanywi kwa kuitisha press conferences na kulalamika, kunafanyika kwa kujaza fomu na kwenda mahakamani.
Nilimalizia kwa kutoa wito kwa wana jf, kuwa wengi tulikuwa na wagombea wetu, kama wagombea wetu, wemeshindwa kihalali kwenye uchaguzi huru na wa haki, then tukubali matokeo, tukubali uchaguzi umekwisha, na kutoa ushirikiano kwa aliyeshinda kihalali!.
Tusiendelee kushadadia yaliyopita, bali tugange yaliyopo na yajayo ya uchaguzi wa 2020!.
Asante.
Paskali.