Pascal Mayalla atoa dongo kwa UKAWA

Pascal Mayalla atoa dongo kwa UKAWA

Bora waambiwe, wanaboa sana badala ya kushusha mambo muhimu tutingishe vichwa tusio wana siasa wanaleta ya ajabu. Wakiendelea hivi, kura za kushinda za 2020 wasahau kabisa tena % itashuka kupita 2015.
Naona umechelewa sana, hiyo cd yako ni zilipendwa sana ya miaka 20 nyuma
 
Aaaagh umenichekesha sana kwa kuandika hivyo...yaani kabisa umeandika nini hypo.... Duh!!!!
Ndio unaniambia hivyo mimi mwananchi nisie na chama, kweli maajabu ya upinzani hayaishi.
Hata usipo kuwa mwananchi uwe mwananchi hutusaidii kitu chochote
 
Mmmmmmm

Sasa unaandika mengine hata sijaongelea na ninaongelea sasa na baadae muweje ubishi mwingi na mie kama mwananchi nasema mnaniboa na hamnivutiiiii...hadi nimeshindwa kusoma yote uliyoandika...hadi kama nitapata muda sijui lini.
Wewe ombea kona bar iendelee kufanya kazi ili upate mkate wako wa kila siku,mambo ya siasa yaache kwa wananchi na wenye uchungu na nchi yao
 
Pascal huna uwezo wa kuwambia wajumbe ulitegemea huyo Mwenyekiti angekwambia nini?waandishi wa watanzania shida sana jk alisema changanya Na akili zako kwani suala la tume linahitaji uwe Na PhD kulifahamu!
 
He he heeeeeeee! Sijacheka kitambo, anyway sukari imeanza kupatikana acha nicheke tena.

Nijuavyo mimi, SABA SABA ni INTERNATIONAL TRADE FAIR...haya NEC nao wana biashara ipi?

Mwaka huu hadi makaburi yatapigiwa promo. Ndio maana Mzee alikabidhi 12bn faida ya mwaka wa fedha uliopita.
 
Yan najua kabsa kwamba nilishinda alafu nikadhurumiwa, alafu leo unakuja na hoja nyeps kama za #Pascal Mayala# Watanzania tumefikia sehemu mbaya ya kugeuza ukweli na kuwa uwongo, alafu anausimamia huo uwongo kwa hoja za kijingaaa!! Nape alisha sema tutashnda hata kwa bao la mkono, na kweli ndiyo yaliyotekea!
 
Kwa taaluma ya Malaya, oops! I mean Mayalla, huwezi kutoka bila kuwa mnafiki na kujipendekeza. Anaishi kwa matangazo ya taasisi za serikali, hawezi kuwa na jipya, zaidi ya jipu.
 
Kwani Lowasa anajua kila kitu duniani. Losawa is a man and therefore susceptible to errors! You need to have your own vision of the issues, your own analysis of the issue guided by reason! Huwezi kushika dola kama watu hawakujui, na njia ya kukujua ni kuwaendea wananchi na kuwahubiria. Ndio maana dini huwa zinahubiriwa particularly hizi zinazomea kama uyoga ili zipate wafuasi. Likewise katika siasa lazima uhubiri sera zako watu wakujue na watofautishe na wengine. You need to identify yourself particularly when you are in an oppressive environment like ours. Losawa is overlooking this important point! The political environment in Tanzania is hostile to the opposition! You need to be more tactical!
Nakuhurumia nadhani unajifunza siasa. Hii yako ni mihemuko tu
 
YULE mtangazaji mwenye makeke mengi kinapofika msimu wa sabasba Pascal Mayala ambaye pia ni mwenyekiti wa PPR(Press and Public Relations). pia ni mtangazaji wa kipindi cha PPR na sabasaba kinachorushwa TV mbalimbali ikiwemo TBC1.

Tarehe 9 july aliingia banda la tume ya uchaguzi Tanzania(NEC) na kufanya mahojiano na mkurugenzi wa uchaguzi (jina nimelishau) alipoona haitoshi akaenda kuwahoji viongozi wa vyama vingine vya siasa waliotembelea banda la tume hilo. nao waliiunga mkono NEC kwa kazi nzuri na uchaguzi ulikuwa huru na haki.

Kazi ilikuja namna Pascal mayalla alipokuwa akiongea baada ya kuhoji wadau, alisema wale wajumbe wa jamii forum waache kumpigia debe kiongozi wao aonekane ameshinda kumbe hajashinda. Wakubali matokeo yaliyotangazwa sio kila siku tunazungumzia uchaguzi.

Pia aliongezea kwa kusema, uchaguzi unafom ya kujaza kama hujaridhika na matokeo hasa kama hujajza hiyo fom ya madai inaonesha uchaguzi ulikuwa huru na haki....
Huyo pascal mayala ni nani katika nchi hii,zaidi ya mganga njaa tu.
 
Mtu poa lakini naona he's still stuck in the 90s. Tazama anavyoendeshwa mbio na Max.

Swali langu kwa nini mpaka leo hajatuambia kwa nini Magu was the chosen one na factors zipi CCM na wenye nchi walitumia kwenye thread yake ya utabiri?
 
Mie nataka nitoke kabisa humu lakini nilishauliza jinsi ya kujitoa sikupata jibu, nishaomba madmin wanitoe mpaka leo nikiingia nakuta nipo,.nielekezeni nijitoe kabisa humu jamii unafanyaje bila kupigwa ban,.manake ban inakuwa kama ni adhabu
pole mkuu,wasiliana na mods waambie wakuremove,...tatzo hawa jamaa washanunuliwa na wakiambiwa ukweli wanafura sasa nashukuru hata vyombo vya habar vishaujua uchafu wao,hii ni aibu kwa jf
 
YULE mtangazaji mwenye makeke mengi kinapofika msimu wa sabasba Pascal Mayala ambaye pia ni mwenyekiti wa PPR(Press and Public Relations). pia ni mtangazaji wa kipindi cha PPR na sabasaba kinachorushwa TV mbalimbali ikiwemo TBC1.

Tarehe 9 july aliingia banda la tume ya uchaguzi Tanzania(NEC) na kufanya mahojiano na mkurugenzi wa uchaguzi (jina nimelishau) alipoona haitoshi akaenda kuwahoji viongozi wa vyama vingine vya siasa waliotembelea banda la tume hilo. nao waliiunga mkono NEC kwa kazi nzuri na uchaguzi ulikuwa huru na haki.

Kazi ilikuja namna Pascal mayalla alipokuwa akiongea baada ya kuhoji wadau, alisema wale wajumbe wa jamii forum waache kumpigia debe kiongozi wao aonekane ameshinda kumbe hajashinda. Wakubali matokeo yaliyotangazwa sio kila siku tunazungumzia uchaguzi.

Pia aliongezea kwa kusema, uchaguzi unafom ya kujaza kama hujaridhika na matokeo hasa kama hujajza hiyo fom ya madai inaonesha uchaguzi ulikuwa huru na haki....
Mkuu Simba Songea, kwanza asante kuangalia kipindi changu cha Saba Saba na PPR.
Pia ni kweli nilitembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuzungumza na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Ramadhan Kailima, kisha nilizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva.

Hoja zangu kuu zilikuwa 3. 1. Wizi wa Kura, 2. Uchakachuaji wa Matokeo, 3. Kukubali matokeo au kuyapinga!.

1. Wizi wa Kura.
Nlionyesha masanduku ya kura kuwa yako transparent. Kama kura hazijaanza kupigwa, masanduku yanakaguliwa na mawakala wa vyama, na hayaondoki hapo hadi zoezi la kuhesabu kura likamilike, hivyo hakuna namna yoyote ya ku temper na sanduku la kura bila kuonekana!. Ila hapa nikazungumzia unless kama kuna masanduku mengine yaliyajazwa kura zilizokwisha pigwa, yakafichwa chumbani, baada ya zoezi la kupiga kura, masanduku hayo yakaletwa kwa mazingaombwe, hivyo kura bandia kugeuzwa ni kura halali.

2. Uchakachuaji wa Matokeo.
Kwenye kila kituo kina mawakala wa vyama, wakati Tume ikitangaza matokeo ya kila jimbo, ilionyesha nakala halisi za matokeo hayo zilizosainiwa na mawakala wa vyama na kila chama kupatiwa nakala halisi, sasa kama kuna tofauti kati ya matokeo halisi ya vituoni na matokeo ya NEC, then vyama lalamishi wangeionyesha nakala zao ili umma ushuhudia uchakachuaji huo wa NEC wenye matokeo tofauti na matokeo halisi.

3. Kukubali Matokeo/Kupinga.
Kwenye hili nilisema, asiyekubali kushindwa sii mshindani. Uchaguzi ni zoezi linaloendeshwa kwa mujibu wa katiba unaozingatia sheria, taratibu na kanuni za nini cha kufanya litokeapo jambo lolote. Hapa nilijikita zaidi kwenye matokeo ya Zanzibar, Jecha alifuta matokeo yale bila kufuata, sheria, taratibu na kanuni. Lakini pia kuna sheria, taratibu na kanuni za kufuatwa, pale ambapo sheria, taratibu na kanuni zinapokiukwa. Sheria, taratibu na kanuni hizo ni pamoja na kujaza fomu ya kupinga matokeo, na kwenda mahakamani. Hakuna lolote kati ya haya lililofanyika. Kupinga matokeo hakufanywi kwa kuitisha press conferences na kulalamika, kunafanyika kwa kujaza fomu na kwenda mahakamani.

Nilimalizia kwa kutoa wito kwa wana jf, kuwa wengi tulikuwa na wagombea wetu, kama wagombea wetu, wemeshindwa kihalali kwenye uchaguzi huru na wa haki, then tukubali matokeo, tukubali uchaguzi umekwisha, na kutoa ushirikiano kwa aliyeshinda kihalali!.

Tusiendelee kushadadia yaliyopita, bali tugange yaliyopo na yajayo ya uchaguzi wa 2020!.

Asante.

Paskali.
 
Back
Top Bottom