Pascal Mayalla atoa dongo kwa UKAWA

simba songea

JF-Expert Member
Feb 8, 2016
1,498
1,214
YULE mtangazaji mwenye makeke mengi kinapofika msimu wa sabasba Pascal Mayala ambaye pia ni mwenyekiti wa PPR(Press and Public Relations). pia ni mtangazaji wa kipindi cha PPR na sabasaba kinachorushwa TV mbalimbali ikiwemo TBC1.

Tarehe 9 july aliingia banda la tume ya uchaguzi Tanzania(NEC) na kufanya mahojiano na mkurugenzi wa uchaguzi (jina nimelishau) alipoona haitoshi akaenda kuwahoji viongozi wa vyama vingine vya siasa waliotembelea banda la tume hilo. nao waliiunga mkono NEC kwa kazi nzuri na uchaguzi ulikuwa huru na haki.

Kazi ilikuja namna Pascal mayalla alipokuwa akiongea baada ya kuhoji wadau, alisema wale wajumbe wa jamii forum waache kumpigia debe kiongozi wao aonekane ameshinda kumbe hajashinda. Wakubali matokeo yaliyotangazwa sio kila siku tunazungumzia uchaguzi.

Pia aliongezea kwa kusema, uchaguzi unafom ya kujaza kama hujaridhika na matokeo hasa kama hujajza hiyo fom ya madai inaonesha uchaguzi ulikuwa huru na haki....
 
Bora waambiwe, wanaboa sana badala ya kushusha mambo muhimu tutingishe vichwa tusio wana siasa wanaleta ya ajabu. Wakiendelea hivi, kura za kushinda za 2020 wasahau kabisa tena % itashuka kupita 2015.
Mkuu ni aibu kila siku kushadidia ya jana. Lazima ifike wakati masuala ya nani alikosa na nani alishinda tuachane nayo, after all katika kutafuta ushindi kuna mbinu nyingi ukishindwa hizo mbinu kubali umeshindwa. Je, Wamarekani wakati ule si walilalamika lakini wakaendelea na ujenzi wa nchi yao? Hivi mikutano ya hadhara ikiendelea tutapata wapi nafasi ya kufanya kazi? Aliyekosa 2015 asubiri 2020 ila asimbane aliyeshinda ili ikifika 2020 aonekane hajafanya lolote. Nchi gani iliongozwa kwa maandamano jamani, kama ni vikao vya ndani nani kazuia mbona CUF wanafanya, Chadema walichagua Katibu Mkuu n.k. Tumechoka sasa
 
Unaongelea uchaguzi wa Ubunge na Udiwani au?

Matokeo ya u-Rais hayapingwi popote tume ikishiyatangaza.

Kwa kifupi: hairuhusiwi kuhoji matokeo ya u-Rais mahakamani.

Uwe umeridhika au hujaridhika itakuwa kama tume ya Uchaguzi watakavyo.
 
Mmmmmmm

Sasa unaandika mengine hata sijaongelea na ninaongelea sasa na baadae muweje ubishi mwingi na mie kama mwananchi nasema mnaniboa na hamnivutiiiii...hadi nimeshindwa kusoma yote uliyoandika...hadi kama nitapata muda sijui lini.
 
Mkuu wa Uchakachuaji na kamati za Ufundi January ndiyo aliyegeuza matokeo na kuwa yalivyo sasa , kinyume na Hapo Leo hii ccm ingekuwa chama cha upinzani Kama KANU ya Kenya .
mm namkubali mh wasira alipeleka kesi mahakamani kupinga ushindi wa bulaya akaambiwa ameshindwa akakubali. kimbembe kipo kwa wapinzani hawakubali mpk waandaman e, leo hii kafulila kila siku anashinda mahakamani aiseeee pesa za ubunge tamu
 
Bora waambiwe, wanaboa sana badala ya kushusha mambo muhimu tutingishe vichwa tusio wana siasa wanaleta ya ajabu. Wakiendelea hivi, kura za kushinda za 2020 wasahau kabisa tena % itashuka kupita 2015.
tunataka maendeleo sio maandamano, mnyika miaka 5 anaandamana kila mara badala ya kuleta maendeleo kutahamaki uchaguzi huu na jimboni hakuna alichofanya akaamua kuhama jimbo
 
Unaongelea uchaguzi wa Ubunge na Udiwani au?

Matokeo ya u-Rais hayapingwi popote tume ikishiyatangaza.

Kwa kifupi: hairuhusiwi kuhoji matokeo ya u-Rais mahakamani.

Uwe umeridhika au hujaridhika itakuwa kama tume ya Uchaguzi watakavyo.
Kama unalijua hilo kwa nini uendelee kubwabwaja?

Mara ooh mwaka huu hatutaibiwa!!

Mara ooh yule mtaalamu wa kuiba kura kahamia ukawa.

Mara ooh pigeni kura tu swala la ulinzi niachieni..!!

Halafu baadae unaibuka na story ya kuibiwa kura.
 
Aaaagh umenichekesha sana kwa kuandika hivyo...yaani kabisa umeandika nini hypo.... Duh!!!!
Ndio unaniambia hivyo mimi mwananchi nisie na chama, kweli maajabu ya upinzani hayaishi.
Usijali, chama unacho. Kwenye masuala haya si lazima uwe na kadi hai. Hata mimi hiyo kadi sina. Na kwa maoni yako uliyotoa, you belong where I have 'placed' you, at chechemeee!
 
Back
Top Bottom