Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,718
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la Jumapili ya leo ambayo ni Sikukuu ya Pasaka.
Pasaka ni sikukuu ya ukombozi na ushindi dhidi ya dhambi zozote ikiwemo dhambi ya dhulma ya uchaguzi, Je tuitumie Pasaka hii kuombea uchaguzi wetu uwe uchaguzi huru kweli na wa haki kweli, au tuuache tuu uendelee vile vile kama kawa, kama vile alivyosemaga Nape?.
Kwa vile leo ni Jumapili ya Sikukuu ya Pasaka, nianze kwa kuwatakia heri za sikukuu ya Pasaka kwenu nyote na kwa wenye majina ya Paskali, Paschal, Pascal, Pasco, Pascalia, Pascalina, Pascoe, Pasqa, Ester, Estarina, ambao walipewa majina hayo kutokana na walizaliwa siku ya Pasaka, nawatakia heri ya kuzaliwa, nikiwemo mimi nilizaliwa siku ya Jumapili ya Pasaka, nikitanguliza miguu!.
Japo mimi ni Mkristu Mkatoliki, Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa Waraka wa Pasaka, lakini kwa mwaka huu, sijabahatika kuona na kuusoma, lakini kwa vile mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, salaam zangu za Pasaka zitajikita humo humo kwenye Uchaguzi.
Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya Kikristo inayoadhimisha ufufuko wa Yesu Kristo kutoka kwa wafu, tukio linaloaminika kutokea siku ya tatu baada ya kusulubiwa, kufa na kuzikwa kwake. Ni kilele cha siku tatu kuu za Pasaka na inachukuliwa kuwa tukio muhimu na la furaha zaidi katika kalenda ya Kikristo. Inasherehekewa siku ya Jumapili mwanzoni mwa majira ya kuchipua, ikiashiria maisha mapya, tumaini, na ushindi dhidi ya dhambi na mauti.
Historia ya Pasaka
Jina la "Pasaka" limetokana na sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi linaloitwa pasakh kwa lugha ya Kiebrania. Kinyume cha Kiingereza, ambacho kina maneno mawili, Passover na Easter, katika Kiswahili na lugha nyingine nyingi majina ya sherehe za Kikristo na Kiyahudi hazitofautiani.
Asili yake ni kwamba kusulibiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo kumetokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi mnamo Aprili ya mwaka 30 BK.
Wakristo wa kwanza, ambao wote walikuwa Wayahudi, walisheherekea sikukuu ya pasaka ya Kiyahudi pamoja na kumbukumbu ya ufufuko wa Yesu. Baadaye sherehe na pia tarehe zikawa tofauti.
Badiliko kubwa zaidi lilikuwa lile la Wakristo Wakatoliki kuamua kuadhimisha sikukuu ya Pasaka daima iwe ni siku ya Jumapili kwa kuwa ndiyo siku ya ufufuko, wakati Wayahudi waliendelea kuidhimisha Pasaka kwa kuangalia tarehe, bila kujali ni siku ipi ya juma na mwisho zikatokea pasaka mbili, pasaka ya Kiyahudi ambayo tarehe haibadiliki, na pasaka ya Kikiristu ambayo ili uiangukie siku ya Jumapili, tarehe zinakwenda zikibadilika.
Kwa vile, Pasaka ni siku ya ukombozi, Kristo ameyashinda mauti na kutukomboa, kwa mateso hadi kifo msalabani, ni kwa kupigwa kwake au kwa kuteswa kwake, sisi tumeponywa, tumekombolewa.
Kwa vile huu ni mwaka wa uchaguzi, uchaguzi wa mwaka huu pia tuufanye ni uchaguzi wa ukombozi, muangalia mgombea wako wa udiwani, umbunge na urais kwa jicho tunduizi, huku ukijiuliza, mtu huyu ataweza kutukomboa kata yetu, jimbo letu au nchi yetu, bila kujali anatoka chama gani, ukimuona anaweza, mchague, ili kukuletea ukombozi kwenye kata, jimbo na nchi.
Kama ni mgombea aliyekuwe kabla, na sasa anagombea tena, mpime kwa jicho tunduizi, kwenye hiyo miaka mitano mliomchagua, amewafanyia nini?, amewaletea maendeleo gani?, kama hakuna cha maana alichofanya, hata amwage mapesa kiasi gani ya rushwa ili achaguliwe tena, pesa zake kuleni, lakini kwenye kura, tupa kule, piga chini hata awe maarufu kiasi gani, ili muikomboe kata yenu, jimbo lenu nan chi yenu, mchagueni mtu atakayewaletea maendeleo, bila kujali anatoka chama gani.
Na wakitokea wagombea wawili au watatu wote wana sifa zinazokaribiana, kwanza angalie mgombea mwenye kitu cha kuonyesha aliwahi kukifanya, mtu akija na maneno matupu, nitafanya hiki , nitafanya kile, kama hakuna chochote cha kuonekana alichowahi kufanya, huyo ni mgombea maneno matupu, vitendo sifuri, tupa kule!, ukimchagua mtu ambaye hajawahi kufanya chochote cha kuonekanika, ujue hata fanya chochote!.
Mtu kuwa kiongozi mziri, sio lazima kwanza uwe kiongozi ndio uweze kufanya kitu, muangalie huyu mtu kuanzia kwenye familia yake, anaiendeshaje, kijijini kwake, nyumbani kwake kukoje?, kwenye jamii yake, anajitoa kiasi gani, ukijiridhisha ndio mpeni uongozi, akija mtu, hata akiwa na maneno matamu kama asali, lakini ameshindwa kuiongoza familia yake, hana chochote cha kuonekanika alichowahi kukifanya, mtu huyo kama kula tuu pesa yake kula pesa, tupa kule, hawezi kuwaletea maendeleo yoyote!.
Na mwisho uchaguzi wakati mwingine ni vita, ni mapambano ya ukombozi, hivyo kunaweza kutokea watu wazuri tuu wasio na hatia, wakasulubiwa kama Yesu, msiwe na wasiwasi, ni kwa kutesswa kwao nyinyi mtaponywa, kuna wakati Mungu huweza kulifanya lile jiwe lililokataliwa na waashi, likafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!.
Hivyo kama ilivyo kwa Wakristu, keshini mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa, Watanzania, tukeshe tukimuomba Mungu, atupatie viongozi bora na waadilifu kwenye uchaguzi huu, tuuombe uchaguzi wetu uwe huru na wa haki.
Mungu Ibariki Tanzania,
Nawatakieni Pasaka Njema.
Wasalaam.
Paskali

Umuhimu
Pasaka ndio sikukuu muhimu kabisa katika kwa madhehebu mengi ya Ukristo, kwa sababu ufufuko huo ndio msingi mkuu wa imani ya Kikristo ambapo fumbo la imani ya Kikristo ni Kristo Alikufa, Kristo Alifufuka, Kristo Atakuja tena, hivyo Wakristo wanaishi kwa matumaini ya kumsubiria mwokozi wetu Yesu Kristu arudi tena kuja kutuchukua, tena tunasisitizwa “kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa”.Kwa vile, Pasaka ni siku ya ukombozi, Kristo ameyashinda mauti na kutukomboa, kwa mateso hadi kifo msalabani, ni kwa kupigwa kwake au kwa kuteswa kwake, sisi tumeponywa, tumekombolewa.