Pangua ya Baraza la Mawaziri yanukia

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Uteuzi wa Dk Stergomena Tax kuwa mbunge, unaibua hisia kama ni mwanzo wa Rais Samia Suluhu Hassan kupangua Baraza la Mawaziri.

Dk Stergomena, mwanamke mwenye heshima kubwa kwenye uga wa kidiplomasia, anaingia bungeni kipindi ambacho Taifa halina Waziri wa Ulinzi kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi na Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa alifariki dunia Agosti 2, mwaka huu.

Kwa nafasi hiyo kuwa wazi na kwa uteuzi wake, tafsiri ya moja kwa moja inayojengeka kwa baadhi ya wachambuzi wa mambo ni kuwa Dk Stergomena yupo njiani kwenda kuteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 55, ibara ndogo ya (4), imeweka sharti la kuwa ili mtu awe na sifa ya kuwa waziri au naibu waziri, anapaswa kwanza kuwa mbunge katika Bunge la Tanzania.

Tayari Dk Stergomena ameapishwa bungeni juzi na Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye hakusita kuonyesha furaha yake wakati akimkaribisha mwanadiplomasia huyo.

“Nakupongeza kwa kuteuliwa na Rais katika nafasi zake zile; nichukue fursa hii kukukaribisha na kukupongeza kwa kazi kubwa uliyomaliza kuifanya ya kuwa Katibu Mkuu wa Sadc na tunasikia fahari kubwa, kwani umetujengea heshima na tunasikia fahari kwamba, wewe sasa ni miongoni mwetu. Karibu sana nyumbani,” alisema Spika Ndugai baada ya kumaliza kumwapisha.

Dk Stergomena anakuwa mbunge wa tisa kuteuliwa na rais na hivyo nafasi za uteuzi alizopewa kikatiba kubaki moja.

Dhana nyingine kuwa uteuzi wa Dk Stergomena kuwa mbunge ni mwanzo wa safari ya uwaziri, inajengwa na ukweli kwamba tangu kifo cha Kwandikwa, imechukua muda mrefu kwa Rais Samia kujaza nafasi yake.
 
Uteuzi wa Dk Stergomena Tax kuwa mbunge, unaibua hisia kama ni mwanzo wa Rais Samia Suluhu Hassan kupangua Baraza la Mawaziri.

Dk Stergomena, mwanamke mwenye heshima kubwa kwenye uga wa kidiplomasia, anaingia bungeni kipindi ambacho Taifa halina Waziri wa Ulinzi kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi na Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa alifariki dunia Agosti 2, mwaka huu...
JE MWENYEKITI WA UVCCM?
 
Kwa mara ya pili Tanzania Waziri Mkuu anaenda kusitishwa uongozi katikati tukumbuke Warioba na Sokoine waliwai kusitisha uwaziri mkuu kwa sababu mbali mbali

Sokoine ilikuwa kwa ajili ya Masomo Lakin Warioba ilikuwa kushindwa kutoa ushauri murua .

Wengine wanaoaga ni Nchemba anapelekwa Kilimo!

Tax anakuwa wa Fedha !
Jaffo out !!!

JMsoga
 
Nawafurahia sana watanzania, yaani si mambumbumbu ila wanakumbuka sana mambo kinafki😁!.

👉🏾 Kwenye masuala ya uongozi hasa linapokuja suala la kiongozi mpya watanzania kupitia keyboard wana matarajio makubwa sana kutoka kwa kiongozi mtarajiwa, ukiweka elimu ya huyo mtarajiwa ndipo hasa unapata picha halisi.

Wengi wanasahau mfumo wetu wa uongozi unapwaya sana kutokana na siasa za nchi yetu, mteuliwa hata awe mzuri kiasi gani siasa ya nchi inampeleka njia tofauti, sababu anakuta muongozo mezani.
 
Kwa mara ya pili Tanzania Waziri Mkuu anaenda kusitishwa uongozi katikati tukumbuke Warioba na Sokoine waliwai kusitisha uwaziri mkuu kwa sababu mbali mbali...
Haya maumbeya mnayatumia kulinda watu wenu

eti spin

spin my foot
 
Back
Top Bottom