Pamoja na Simba kupeleka kikosi cha kwanza Zanzibar katika mashindano yasiyopewa uzito bado imeshindwaa kutwaa ubingwa

MwananchiOG

JF-Expert Member
Apr 4, 2023
645
1,301
Pamoja na kupania na kukamia mno katika michuano ambayo timu zingine makini iliyachukulia kama sehemu ya kupima baadhi ya sajili zake huku zikipeleka vikosi B na kujàribu baadhi ya wachezaji wa u20 kwa ajili ya kutunza nguvu ya vikosi vya kwanza kwa mashindano makubwa na kuepuka majeraha kwa wachezaji tegemeo kwa ajili ya mashindano makubwa

Hali ambayo imeķuwa tofauti kwa Simba sc ambayo yenyewe ikapeleka kikosi cha kwanza ambacho kilishuhudiwa kucheza katika mashindano ya CAF dhidi ya Wydad, Asec na Jwaneng n.k

hii inaonyesha kwamba timu hii yenye makazi yake msimbazi pamoja na kupeleka kikosi cha kwanza bado haina uwezo wa kutunishiana misuli hata na vilabu vidogo kama mlandege ambao wamewaadabisha vikali mithili ya mbuzi aliyemwagiwa maji ya moto katika michuano hiyo.Je, kama kikosi cha kwanza hali ni hii, Je ingepeleka kikosi B pamoja vijana wa u20 hali ingekuwaje, Je, isingekuwa mwanzo wa 5G zingine?

Inasikitisha sana.

20240113_224306.jpg
 
Simba Ina zaidi ya wachezaji sita kwenye mashindano ya Afrika Ila mmekaa kulishana matango pori kuwa Simba ilipeleka kikosi Cha kwanza, kipigo cha APR bado kinawasumbua.
 
Simba Ina zaidi ya wachezaji sita kwenye mashindano ya Afrika Ila mmekaa kulishana matango pori kuwa Simba ilipeleka kikosi Cha kwanza, kipigo cha APR bado kinawasumbua.
20240114_183945.jpg

20240114_183733.jpg

Haya nimekuwekea na ushahidi hapa, ukimtoa Inonga, 90% ya wachezaji waliocheza mapinduzi ni wachezaji wa kikosi cha kwanza.
 
View attachment 2871798
View attachment 2871799
Haya nimekuwekea na ushahidi hapa, ukimtoa Inonga, 90% ya wachezaji waliocheza mapinduzi ni wachezaji wa kikosi cha kwanza.
Sasa mbona umejijibu vizuri
Kikosi Cha Wydad kilichoanza ambao hawakucheza Zanzibar yupo Shabalala, Inonga, Mzamiru, Kibu Dennis na Chama wachezaji watano hawapo huoni unampa credit aliyesema huko kwenu wenye akili ni wawili.
 
Ifikie mahali mjione huko Yanga hamna content yani bila Simba hamna cha kufanya...
Akili zenu chache mlizobaki nazo ni za kuizungumzia Simba...
Poleni sana
Humu jukwaani Vyura wanaongoza kwa kuandika thread zinazohusu Simba...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom