Taifa Stars ya sasa inanikumbusha kikosi cha "Kakakuona"

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,129
7,896
Mageuzi ya kweli kwenye jambo lolote huwa yanahitaji kufanya maamuzi magumu. Wakati mwingine maamuzi hayo yanaweza kushtua watu, yanaweza kuogopesha wengine, yanaweza kukatisha tamaa kwa baadhi na utegemee lawama na shutuma nyingi.

Nimependa ushujaa wa Kocha wa Taifa Stars Amrouche ambaye amekuwa haogopi kubadili kikosi chake na kujaribu damu mpya kila mara. Wameachwa kina Mohamed Hussein Zimbwe, Shomari Kapombe ambao bado ni tegemeo pale Simba. Wakati timu ina uhaba wa washambuliaji ameachana na John Bocco ambaye pale Simba bado ana nafasi ya kucheza. Ni juzijuzi tu Mzamiru Yassin alikuwa tegemeo la kiungo pale Stars, ila hakumuita katika game hizi mbili za mwisho. Hakuna ambaye alitegemea katika game gumu kama la jana dhidi ya Morocco angewaweka benchi Msuva, Samatta, Feisal na Manula ila tuliona jinsi timu ilivyocheza kwa umoja na kujituma kipindi cha kwanza.

Niliwahi kuhadithiwa hadithi moja na wahenga. Miaka ya nyuma kuliwahi kuwa na mashindano fulani ya CECAFA ambapo Tanzania tulikuwa na timu mbili. Timu ya kwanza ilikuwa ndiyo ya wachezaji wenye majina makubwa makubwa tegemeo wa Simba na Yanga. Hiyo ndiyo ilikuwa Taifa Stars. Timu ya pili ilikuwa na madogo waliokuwa hawana majina makubwa ambao hakuna aliyetegemea kuwa wangeenda kufanya lolote. Hiyo timu B ilipachikwa jina la "Kakakuona". Wakati kikosi cha kwanza cha Taifa Stars kilitolewa hatua ya makundi, Kakakuona ilienda hadi fainali na kufungwa kwa taabu.

Hawa madogo wanaopewa nafasi sasa hivi wanaweza wasiwe na uzoefu mkubwa katika mashindano ya kimataifa ila wana vitu muhimu sana, vingine wazoefu wetu wanavikosa na tukistick nao naamini miaka 3 hadi 4 ijayo tutakuwa na kikosi kizuri sana. Kilichobaki tutafute wakali kama wanne kwa safu ya ushambuliaji na viungo washambuliaji ili tuongeze makali pale mbele na katikati.
 
Haikuwa Taifa Stars ila ni timu mbili za bara moja A na ya pili B. Ile ya kwanza Kilimanjaro Stara ilikuwa na nyota wakali na Kakakuona wakachukuliwa wale wa kawaida. Hiyo ilikuwa michuano ya Challenge wakati ikiwa ya moto.
 
All in all, Taifa stars itaendelea kubakia kuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka ile siku tutakapo amua rasmi kuwekeza kwenye mpira wa miguu kwa vitendo.
Pamoja na kwamba bado kuna mengi ya kufanya sidhani kama ni sahihi tena kuiita Kichwa Cha Mwendawazimu. Kumbuka wakati inaitwa hivyo hata vilabu vyetu navyo vilikuwa hohehahe ila wote tunakubali sasa kiasi navyo vimebadilika.

Morocco walituheshimu sana kwa kutuletea kosi lile.
 
Back
Top Bottom