KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,179
..Unazungumzia AFDB yenye makao makuu Abidjan, Ivory Coast?
..kuna mabeberu wana hisa ktk benki hiyo.
..pia mahitaji yetu ya mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni makubwa na hayawezi kutoshelezwa na AFDB peke yao.
..muelekeo tuliochukua utatuletea ugumu ktk kupata misaada na mikopo ya masharti nafuu.
..Tukichukua mikopo mingi ya masharti magumu tunaweza kufika mahali ncho ikaelemewa na mzigo wa madeni. Nadhani unakumbuka matatizo ya ulipaji madeni tuliyokuwa nayo wakati wa utawala wa Mzee Mkapa.
..marafiki zetu and our development partners, wanatushauri, hawatulazimishi, tulinde haki za binadamu, tudumishe utawala wa sheria na katiba, tujenge demokrasia ya kweli, tukomeshe vitendo vya kikatili, etc etc.
..mengi wanayotushauri ni mambo ambayo tunaweza kuyatekeleza. Hakuna haja ya kuliumiza taifa[ walio wengi] kwa kiburi cha watu wachache.
..Ushauri wangu ni Raisi Magufuli afanyie kazi dondoo ambazo haziwaridhishi marafiki zetu na wadau wetu wa maendeleo. Akifanya hivyo ataiweka nchi ktk nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi ya kimaendeleo.
Ushauri mzuri, lakini wao wanachotafuta ni sifa.
Wakisikika na hao wanaowavimbisha vichwa kwa vigelelegele maneno kama anayoyasema Kabuti "hatutapiga magoti" kwao inakuwa faraja kubwa.
Inashangaza kidogo, kwa sababu mwanzo nilidhani ni utani tu, walipoanza kelele za "Mabeberu, Wasaliti," n.k., kwa sababu maana ya maneno kama haya enzi hizi kwa kweli yamepitwa na wakati sana.
Enzi za Mwalimu Nyerere maneno kama 'unyonyaji', mabeberu yalikuwa na maana, na tulijifunza maana hizo tukazielewa.
Sasa kuendelea na mbinu zile zile za kuita watu majina wakati huu kwa kweli hakufai.
Hii haina maana kwamba hakuna wapigaji/wanyonyaji. Lakini kama unajiandaa mwenyewe ili unyonywe pamoja na kujua kuwa kunyonywa kupo, halafu ukizinduka uanze kupiga kelele zile zile za zamani za kuita watu kijumlajumla majina- 'mabeberu' kana kwamba umegundua mvinyo mpya haipendezi.. Kwa hiyo sisi tunalianzisha upya, la Magharibi na Mashariki; vita baridi mpya inaanzia Tanzania?
Vita ya mabwenyenye na watwana ilishapiganwa miaka mingi. Leo hii ukitaka tena kujiweka kwenye utwana hiyo ni hiari yako hakuna anayekukataza. Lakini unapojifanya umezinduka na kuanza kupiga kelele zilizopigwa zamani, watu watakuona kama mwenda wazimu fulani.
Kama umegundua mahali umegongwa, shughulika na hao hao wanaokugonga. Usianze kujifanya unapambana na mfumo na kuhusisha kila mtu. Wazungu wote kwa sababu ya uzungu wao hawawezi kuwa 'mabeberu'.
Kwa ujinga mwingi sasa nchi nzima inaimba 'Mabeberu'. Huu sio ukichaa? Nilidhani ni utani; kumbe hali hiyo ndiyo inayowaletea sifa na wanafurahi wanapoona wajinga wakishangilia upuuzi huo.
Profesa mzima anakwenda kuongea Bungeni "kuwapigia magoti" watu, na wakati huo huo analilia wawekezaji waje kwa wingi kuwekeza nchini. Anawekea mkazo "hatutawapigia magoti", ili wajinga waone kuwa nchi inamsimamo - lakini wajinga wasichojua viongozi hawa ndio wapiga magoti wakubwa; ombaomba wa kutupwa kwa njia mbalimbali wasizotaka wajinga wao wasizitambue kama ndio 'kupiga magoti' kwenyewe huko.