OK labda nikuulize kulikuwa na umuhimu wowote wa yeye kusema HATOWAPIGIA MAGOTI WAZUNGU KUWAOMBA MSAADA.
kwani kuna mashindano kati yetu na wazungu?
Nani anayeteseka kati yetu na wao?
TUONGEE NAO, TUSIWAPIGIE MAGOTI.
Ukweli ni kwamba tunategemeana.
Nchi za Magaharibi zinaziihitaji Nchi za Afrika kwa mali asili (natural resources), masoko, na malengo mengine ya kimkakati (mf. usalama n.k) kama Nchi za Afrika zinavyozihitaji Nchi za Magaharibi kwa teknolojia, mitaji n.k.
Hivyo basi, ni muhimu kuheshimiana wakati pande zote mbili zinapokutana mezani kujadili biashara au mambo mengine yenye maslahi ya pande mbili.
Huwezi kupindisha ukweli kwamba Nchi za Magaharibi (na zingine) zilitenda vitendo cha kikatili na kinyama (historical injustices) dhidi ya bara la Afrika. Waweza kutaja utumwa, ukoloni na wizi kama mifano tu. Afrika haijawahi kuzitendea hivyo Nchi za Magaharibi na wenzao. Hata leo Nchi za Magaharibi haziji Afrika kwa ajili ya uhisani. La hasha. Wanakuja kufanya biashara au shughuli zingine zenye maslahi kwao. Wakikukaribisha "lunch" usijidanganye kwa kudhani unapendwa, wala usijidanganye ukajifanya wewe ni "Blue-eyes" mweusi. Never ever. Lazima kuna kitu wanatafuta kwa maslahi yao. Kama Mheshimiwa Rais Magufuli anavyosema mara kwa mara: "There's no free lunch". Hivyo basi, ni sahihi kwa Nchi za Afrika kusisitiza "win-win situation" na kamwe haiwezi kuwa hivyo kwa kupiga magoti. Tusipokuwa macho wazungu na sasa hata Wachina "watatulalia" na kutumaliza.