Palamagamba Kabudi, Unaivuruga Nchi....!

Palamagamba Kabudi, Unaivuruga Nchi....!

Mapato ya tanzania kwa kukadiria kiwango cha juu kabisa ni 1.4 trillin per month mara 12 ni 16.8 trillion budget ya serikali ni trillion 32! Go figure hizo 15.2 trillion za ziada zinatoka wapi?
Kwa hesabu hii, kuanzia huyo namb 1 wao hadi mwenyekit wa kijiji nimewaona misukule tu
 
Waziri wa Mambo ya nje ni mtu muhimu sana katika taifa. Ni mwanadiplomasia mkuu ukimuondoa Rais. Leo tnaye Palamagamba Kabudi, namba moja kuwaimbia Mabeberu Singeli.

Ni huyu Kabudi aliyekuja na sheria za hovyo zinazotufanya sasa hivi kuonekana vituko kimataifa. Ndiye Kabudi aliyesababisha wawekezaji wengi kuondoka Tanzania akiwa Waziri wa Sheria.

Huyu Kabudi anayeimba nyimbo za kuwakandia mabeberu ndiye aliyekuwa namba moja kuzunguka nchi za Ulaya kupiga magoti tusiwekewe vikwazo. Inakuwaje anawahadaa watanzania huku anaivuruga nchi?

Bila shaka, Kabudi ndio beberu namba Tanzania.
Huyu mtu toka nilipomshuhudia kwenye ule msiba wa Mengi akiiga sauti za ma MC wa kwenye masherehe katika kumuwakilisha rais nilimtilia mashaka na kumshusha hadhi.
 
Grace maana yake ni kazi mpokeaji asiyowajibikia. Kama ni hivyo basi huu ni msaada.
Sasa unamkataa je mtoa grace(msaada) kwako?
 
Ujuha na ongo mtupu,hakuna wakati wowote Tanzania imewahi kurudisha msaada.
Kukataa msaada nako mnaita ni maamuzi magumu!
Ni masharti gani yasio na maslahi kwetu ambayo tumepewa mpaka sasa?Hakuna.
Iwe kurudisha watoto waliopata mimba shuleni,kuheshimu haki za wakosoaji, uchaguzi huru,nk
Wewe unaona uongo na ujuha wenzio Bungeni Kabudi amewasomesha wameelewa
 
Huyu Anafaa aitwe Kalamaganda Kibudu,
Ila nisaidieni maana ya maneno yafuatayo
1.Beberu
2.Bwanyenye
3.Wakoloni
4.Walowezi
 
Tatizo mambo mengi,wanajifanyia wenyew kina kabudi.mpk Leo mkataba wa bagamoyo project hajauelezea kisheria,maan ni yeye anehusik kweny kuutema.sasa,tuwekewe wazi
 
Waziri wa Mambo ya nje ni mtu muhimu sana katika taifa. Ni mwanadiplomasia mkuu ukimuondoa Rais. Leo tnaye Palamagamba Kabudi, namba moja kuwaimbia Mabeberu Singeli.

Ni huyu Kabudi aliyekuja na sheria za hovyo zinazotufanya sasa hivi kuonekana vituko kimataifa. Ndiye Kabudi aliyesababisha wawekezaji wengi kuondoka Tanzania akiwa Waziri wa Sheria.

Huyu Kabudi anayeimba nyimbo za kuwakandia mabeberu ndiye aliyekuwa namba moja kuzunguka nchi za Ulaya kupiga magoti tusiwekewe vikwazo. Inakuwaje anawahadaa watanzania huku anaivuruga nchi?

Bila shaka, Kabudi ndio beberu namba Tanzania.
Utakuwepo kumpokea lisu
 
Ebu twambie ni muwekezaji yupi aliyekimbia kuwekeza, fwatilia kwa makini mapato tunayopata kwa sasa baada ya sheria mpya za madini, kwanini Watanzania tu nawapenda watu wanatuibia? Nadhani tumtende haki Kabudi kwenye eneo hili la sheria za madini kasimamia vizuri Sana.
Unasubiri 'mwekezaji aliyekimbia', humfikirii mwekezaji aliyesita kuja kuwekeza?
 
Naona unasahau matatizo yote tunayokumbana nayo yanasababishwa na utendaji mbovu wa serikali yetu. Nikakaa chini na kutafakari huwa nashindwa kupata majibu juu ya hili ambalo serikali yetu inatufanya sisi mavuvuzela na kuendeleza ujinga kwa watanzania.
Wapi katika uso wa dunia hii ama nchi yoyote duniani ambayo wananchi wake washaondokana na shida ambazo unaona kwetu zipo??? NItajie tafadhari
 
Mfano wa HOVYO kabisa. Kuna haja gani msomi wetu KUANZIA MABEBERU kila wakati. Ni lugha ya kuudhi sana hiyo. Haifai. Tujirekebishe tu twende MBELE. Binafsi nakereka sana kuitana Beberu!!
Hatuna waziri anaitwa Kalamagamba kosa la kwanza

Hoja yako haina mashiko na umeandika hayo kwasababu Avatar yako inathibitisha ulichokiandika na maneno ya Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi!!!

Acha umagharibi katika kufikiri !!

Nikuambie tu machache kuhusu Unakokupenda huko ...nchi ya Kongo DRC inaweza ku supply HEP Barani Africa kwa 22 asilimia ,,ina vyama vya siasa vinakaribia 200 na ushehe na ndio miongoni mwa nchi ktk Afrika zinazojiita Democratic lakn kiuhalisia hakuna demokrasia ....huu n wimbo ambao wazungu wameuleta tunauimba hadi leo mbaya zaidi hata watoto wadogo wameanza kuuimba yani uhuru uhuru uhru uhuru uhuru na kusahau mambo ya msingi,,,, si kwenye kutenda ,kufikiri kuabudu na hata kwenye utamaduni ndio maana leo kote uendako tunaangalia movie za kigeni na wewe kuutukuza umagharibi kwa kuona kujiita hvyo ni kuwa civilized !! Afrika hakuna cha kujivunia sasa bali ni kupigana majungu tu na kubezana sisi kwa sisi kwa kutumia sindano za hawa jamaa ....pata muda ujifunze ya Libya na maisha yao hivi leo.....Hakuna kitu kibaya iwe katika haki za binadamu ama kidemokrasia kwa Afrika kulaumiwa!!! Yote haya walitengeneza wao kwetu na sasa sisi tulioathiriwa sasa tumesaahau kw kisa tu wamekuja kivingine !!

Amka!
 
Mfano wa HOVYO kabisa. Kuna haja gani msomi wetu KUANZIA MABEBERU kila wakati. Ni lugha ya kuudhi sana hiyo. Haifai. Tujirekebishe tu twende MBELE. Binafsi nakereka sana kuitana Beberu!!

"MABEBERU" NI "IMPERIALISTS"

Ni lugha tu. Kwa Kiingereza "Mabeberu" huitwa "mperialists" ambao ni mabepari waliokubuhu.

Madhara ya ubeberu kwa bara la Afrika ni dhahiri.

Unataka wale wanaotumia mfumo wa Ubeberu kuendeleza na kuendekeza unyonyaji wa nchi zingine waitweje kama siyo "Mabeberu"? Ni jina gani zuri unalolijua?
 
Back
Top Bottom