Waziri wa Mambo ya nje ni mtu muhimu sana katika taifa. Ni mwanadiplomasia mkuu ukimuondoa Rais. Leo tnaye Palamagamba Kabudi, namba moja kuwaimbia Mabeberu Singeli.
Ni huyu Kabudi aliyekuja na sheria za hovyo zinazotufanya sasa hivi kuonekana vituko kimataifa. Ndiye Kabudi aliyesababisha wawekezaji wengi kuondoka Tanzania akiwa Waziri wa Sheria.
Huyu Kabudi anayeimba nyimbo za kuwakandia mabeberu ndiye aliyekuwa namba moja kuzunguka nchi za Ulaya kupiga magoti tusiwekewe vikwazo. Inakuwaje anawahadaa watanzania huku anaivuruga nchi?
Bila shaka, Kabudi ndio beberu namba Tanzania.
NI SHERIA ZIPI ZA HOVYO?
Unamaanisha zile sheria za Tanzania kumiliki uchumi wake na kusimama rasilimali za nchi dhidi ya uporaji?
Kiuhalisia na kwa mantiki yoyote iwayo, sheria hizi siyo za hovyo. Ni sheria muhimu sana kwa ustawi na heshima ya Nchi. Ni kupitia sheria hizi rasilimali za nchi zitalindwa na kutumika kwa maslahi ya Nchi, kwetu tukio hai sasa na kwa vizazi vojavyo.
Kwa wale walio na nia ovu ya kupora rasilimali za nchi hii, ni dhahiri wataziona sheria hizi hazifai maana zinawakwaza.