Padre Amigu; Tafsiri potofu juu ya Talaka

Padre Amigu; Tafsiri potofu juu ya Talaka

“PORNEA” SABABU YA KUMWACHIA MKE
Tunaendelea. Acha tung’oe nanga tena. Vijana, kati ya maswali yenu mliyoniomba niwafafanulie ni sababu ya kumwacha mke iliyotajwa katika Mt 19:9.

Mliniandikia na kuniuliza ifuatavyo: “Baba twaomba tuulize, mbona kwenye Injili Yesu anaruhusu talaka kama kuna uasherati umetokea kwenye ndoa wakati mafundisho ya Kanisa Katoliki hayaruhusu hivyo?”
Hivi ndivyo mlivyoniwekea.

Kwa kweli, mimi sijui msingi wa swali lenu kama ni hamu ya kutalikiana au kutaka kujua tu. Lakini kwa vyovyote sina sababu ya kuchimba mahali pakavu kama hapo. Mimi naenda kwenye swali lenu tu.

Muktadha wa Swali la Mafarisayo
Awali ya yote, acheni niwapeni muktadha wa swali aliloulizwa Yesu. Ni hivi katika Kum 24:1-4 imeandikwa hivi: “Ikiwa mwanaume ameoa mke na baadaye akawa hapendezwi naye KWA SABABU AMEONA KWAKE KITU KISICHOFAA, basi huyo mwanaume akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza nyumbani mwake, kisha huyo mwanamke akaondoka, akaolewa na mwanaume mwingine, kama huyo mume wa pili akimchukua, akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza nyumbani mwake, au kama huyo mumewe akifa, basi, yule mume wa kwanza haruhusiwi tena kumchukua huyo mwanamke kuwa mke wake kwa sababu alikwisha kutiwa najisi. Kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu Mwenyezi.”
Marabbi Wawili

Nukuu hii ndiyo iliyo nyuma ya swali la Mafarisayo waliokuja kumtega Yesu kwa swali juu ya talaka. Kifungu hiki kilishakuwa “habari ya mjini” kati duru za kisomi za Wayahudi na matokeo yake marabbi (walimu) wawili maarufu walijikuta wakipingana katika maelezo ya hicho “KITU KISICHOFAA” (kwa Kiebrania “ERWAT DAVAR”) ambacho mwanaume akikiona kwa mkewe kinaweza kuwa sababu ya kumwandikia na kumpa talaka. Marabbi hao walikuwa Hillel na Shammai. Sasa yasikilize mafundisho yao.
Haki ya kuacha ilikuwa ya mwanaume siyo mwanamke. Mume ndiye aliyeacha, mke ndiye aliyeachwa. Rabbi Hillel, babu yake Gamalieli aliyekuwa mwalimu wa Mtume Paulo, alisema “KITU KISICHOFAA” (“ERWAT DAVAR”) ni kitu chochote kile kingalichoondokea kutompendeza mume, mathalani, mke kuwa mchafu, kuacha kumwamkia, kuvaa vibaya na kadhalika na hata kama mwanaume angemwona mwanamke mwingine mwenye sura nzuri aliyetaka amwoe badala ya huyo aliyemwoa na kumwona ana sura mbaya.

Lakini kinyume cha Rabbi Hillel alisimama Rabbi Shammai ambaye alisema “KITU KISICHOFAA” (“ERWAT DAVAR”) kinachoweza kutumika kama sababu ya mume kumwacha mkewe sharti kiwe kitu chenye uzito wa kutosha, kwa mfano, ugoni, kutembea uchi mbele ya watu au kitu kingine cha aina hiyo kingalichofanya uchi wa mwanamke uonekane.

Pande hizi mbili zilikinzana sana na, kwa bahati njema au mbaya, kila upande ulikuwa na wafuasi wengi. Ndiyo katika muktadha wa mjadala mkali juu ya “KITU KISICHOFAA” (“ERWAT DAVAR”) wanapokuja Mafarisayo kumjaribu Yesu kama anajua kitu ama yeye naye ni maamuma tu. Basi, ndipo walimuuliza kama ni halali kumwacha mke kwa sababu yoyote, yaani kama alivyokuwa akifundisha Rabbi Hillel au la.

Kumbe, Yesu alitumia fursa ya swali lao, kuwasahihisha akina Hillel na Shammai japo pasipo kuwataja kwa majina. Kwa jibu lake aliwaponda marabbi wote wawili kwa kufundisha kitu kisicho matashi ya Mungu. Badala ya misimamo yao ya kuruhusu talaka akawafundisha wanadamu wote kwamba talaka ni kitu haramu kwa maana hutenganisha alichounganisha Mungu tangu mwanzo.

Yesu Alitaja “Pornea”
Hata hivyo, katika maelezo yake Yesu alisema kinachoweza kuwatenganisha watu ni ‘PORNEA’. Lakini kwa kutaja sababu hiyo swali likatuzukia wanadamu wa leo kuulizana hiyo “PORNEA” ni nini. Kumbe, hapa ndipo watafsiri wetu wanapopwelea kwa kushindwa kutafsiri kisahihi neno hilo. Ndipo katika Kiswahili walipotafsiri kwa mkato “uasherati” au “uzinzi.”

Huu ni mkasa wa kitaaluma. Najua watafsiri wengine walichungulia tafsiri za Kiingereza “fornication” au “adultery” ndipo wakatutafsiria “PORNEA” kwa maneno ya “uasherati” au “uzinzi” na hivi nao wao kulistawisha tatizo lile lile la tafsiri. Je, mnanielewa hadi hapa? Kama ndivyo, tusonge mbele pamoja. Ikiwa sijaeleweka hapo, rudia walau mara moja kusudi jibu langu lisikubabaishe huko mbele ya safari.
Vijana, kumbe hapo ndipo tulipofikia, yaani kwenye tatizo la kutafsiri kwa usahihi neno “PORNEA” katika Mt 19:9. Mahali pengi husomwa tafsiri ifuatayo: “Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakayemwacha mkewe isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini, naye amwoaye yule aliyeachwa azini.” Lakini kuna tafsiri nyingine inayosomeka neno “uzinzi” mahali pa neno “uasherati”.
Kwa vyovyote, tofauti hii si kitu cha msingi, mamoja iwe “uasherati” au “uzinzi”, maneno yote mawili ni tafsiri nyepesi mno ya neno lenye maana nzito zaidi - “PORNEA”. Maneno yote hayo mawili yanapwaya kabisa, wala hayakidhi haja ya tafsiri makini. Alichosema Yesu ni kizito zaidi. Hivi hapo “uasherati” au “uzinzi” isieleweke kama uasherati wa kawaida au uzinzi wa kawaida isipokuwa uhusiano wa kindoa kati ya watu waliokaribiana kidamu. Yaani uhusiano wa mahirimu au maharimu.

Uhusiano wa aina hii ndiyo sababu ya kuwatawanyisha watu waliothubutu kuoana. Ndiyo kisa Kanisa Katoliki hukataa kuwafungisha ndoa watu waliokaribiana kidamu. Watu waliokaribiana kidamu hadi digrii ya nne marufuku kuoanishwa katika Kanisa Katoliki. Nia ya kufunga ndoa inapotangazwa mara tatu ni pamoja na kutoa fursa kwa watu wanaowajua wanandoa watarajiwa kama wamekaribiana kidamu watoe taarifa mahali panapohusika.

Kukataa kuwafungisha ndoa mahirimu au maharimu siyo tu kutii kauli ya Yesu Kristo bali pia ni kujiepusha na madhara ya kukaribiana kidamu wazazi. Yaani kama mifugo ya sungura, nguruwe na bata inavyodhurika kwa damu zilizokaribiana za wazazi wao vivyo wanadamu. Watoto wa wazazi waliokaribiana damu si mara haba kuzaliwa na vilema vya kurithi kwa vinasaba pamoja na mikasa ya kuzaliwa na vilema vya upofu, uziwi na ububu. Waulize madaktari wakupe vinaganaga vya kwa nini hutokea hivyo na kisha uende Israeli wanakong’ang’ania kuoana wao kwa wao ushuhudie kwa macho vilema vya sampuli hii vilivyotamalaki. Basi, mkasa huu ukusaidie kuelewa kwa nini Yesu alipokuja duniani katika umbo la mwanadamu aliwashuhudia jamaa zake Waisraeli wakirabiwa na vilema lukuki (Lk 4:18, 7:22).

“Pornea” na “Moicheia”
Namalizia kwa kusema “PORNEA” si “MOICHEIA”. “MOCHEAIA” ndiyo uasherati au uzinzi tunaoufahamu (rej. Yn 8:3-4). Jambo hili tumeliangalia vizuri na kutafsiri vyema katika Biblia ya Kiafrika. Narudia kusudi kushadidia jibu langu. Neno la Kigiriki lililotumika ni “PORNEA” wala si “MOICHEIA”. Sheria ya Kanisa namba 1151- 1152 zina kitu cha kutuambia Wakatoliki. Zitafute uzisome.

Uasherati na Uzinzi Kusameheana kwa Kanuni ya Dhahabu
Katika Kanisa Katoliki, uasherati kama uasherati au uzinzi kama uzinzi si sababu ya kumwachia mke isipokuwa kutenganishwa kwa muda wa walau miezi sita tu. Baada ya kupoa hasira na kusameheana ndani ya miezi sita, wanandoa hualikwa kurejeana kusudi waendelee kuishi kama mume na mke. Kushikana ugoni huwa ni kuvunjika kwa koleo tu yaani kusikokuwa mwisho wa uhunzi. Ngumu lakini ndivyo inavyopasa kufanyika.

Dawa ya mgogoro wa uasherati na uzinzi ni msamaha kwa kanuni ya dhahabu. Kanuni ya dhahabu (Mt 7:12) inasema, Mtendee mwenzako unavyopenda utendewe mwenyewe, na katika maisha ya ndoa hakuna anayependa aachwe kwa sababu amekosa uaminifu. Hivyo, isiwe kwa kuwa umekosewa wewe mwenzio afunge virago aende zake wakati ukikosa mwenyewe eti mwenzio akusamehe! Basi, kusudi msamaha usiwe wa upande mmoja haki yake ni WOTE KUSAMEHEANA. Kwa herini tena!

Mzee wenu Pd. Titus Amigu

My take;

Baada ya kusoma hii kwa makini nimefikiria kupunguza ubishi wangu kwa Kagame juu ya Wachungaji lazima wawe na degree za Theology.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuanze kwa kujua ndoa ni nn
Vitu gani vinafanya ndoa iwe halali since day one,
Ndipo tutajua ni kweli kila kinachofungwa huwa ni ndoa halali na unganisho la Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kila inayoitwa ndoa ama kufungwa kanisani/msikitini inakuwa ni unganisho la Mungu?
vp kwa mwanandoa anaefunga sababu tu ya harusi,sifa,malengo Fulani na siyo nia ya kuishi milele na mwenza?

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kila ndoa ichukuliwe kuwa ni unganiko lililounganishwa na Mungu. Kinachoifanya ndoa iwe unganiko lilio fanywa na Mungu ni kitendo cha watu wawili timamu kuamua kwa hiyari yao kwenda madhabahuni na kula kiapo cha uaminifu, utii na uvumilivu katika hali zote.
Cc Malcom Lumumba Mzigua90 Evelyn Salt Mshana Jr
 
Ni kweli kila inayoitwa ndoa ama kufungwa kanisani/msikitini inakuwa ni unganisho la Mungu?
vp kwa mwanandoa anaefunga sababu tu ya harusi,sifa,malengo Fulani na siyo nia ya kuishi milele na mwenza?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee tambua Mungu ametupa nafsi huru na amejiwekea principle za ku interact na sisi. Kama ni mtu mzima na ukaamua mwenyewe hata kama ni kwa ujinga wako tayari ndio maamuzi yako na umeapa mwenyewe.

Imagine kila mtu arudi kanisani aseme mimi nilitaka harusi tu lakini si kuishi kama mume na mke hivyo ndoa si halali ivunjwe? Unafikiri unacheza na Padre/Mchungaji hapo?

Yapo mazingira ambayo ndoa hata iliyofungwa kanisani inaweza kuwa haikuwa ndoa tangu awali na inavunjwa (hapo ndio utaona talaka sasa). Mfano mtu anajifahamu ni tasa alafu anamdanganya mwenzake hadi wanafunga ndoa, ikigundulika huo utasa ulikuwa unafahamika kabla ya ndoa maana yake hapo ndoa haikuwa halali tangu mwanzo na inavunjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu uzi huu umeibariki jumapili yangu. Nimeuelewa sana, kiukweli biblia inahitaji vichwa sana kuitolea ufafanuzi maandiko yake. Sasa eti leo Masanja mkandamizaji anaenda kuwa mchungaji... Mweeeeeh tunaangamia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu achepuke alete magonjwa ndani,aharibu furaha ya familia and still ni m keep.
Hapana mm sitaangamia kwa kukosa maarifa.uzinzi nitampa mke talaka ila makosa mengine yote tutarekebishana

Sent using Jamii Forums mobile app
Na umpe hiyo talaka kwa kuwa wewe huchepuki... Ni utashi wako hakuna wa kuingilia maamuzi yako. Ila leo ndio nimeelewa vizuri tafsiri ile iliyopotoshwa ya talaka sababu ya uzinzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Father Titus Amigu afungue account humu ndani. Kuna Swali nataka Nimuulize la Kindoa.
 
Ni uhuni tu wakucheza na Lugha. Pornea ndiyo neno limezaa porno. Linamaanisha uasherati na si ngono kati ya ndugu. Ni uhuni wa kujaribu kujustfy mafundisho ya kanisa.
 
Si kila ndoa ichukuliwe kuwa ni unganiko lililounganishwa na Mungu. Kinachoifanya ndoa iwe unganiko lilio fanywa na Mungu ni kitendo cha watu wawili timamu kuamua kwa hiyari yao kwenda madhabahuni na kula kiapo cha uaminifu, utii na uvumilivu katika hali zote.
Cc Malcom Lumumba Mzigua90 Evelyn Salt Mshana Jr
Vipi km mwanandoa mmoja hakuwa na uhiari wa kuunganika milele ktk shida na raha,na alienda madhabahuni kwa malengo fulani tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 wakorintho 7:2 inasema. ili kuepuka uasherati basi kila mtu awe na mke wqke na mke awe na mume wake. Hapo neno lililotafsiriwa uasherati ni hilohilo Pornea lililoandikwa wakati Yesu anasema kuhusu talaka.

ikiwa Pornea inamaanisha Ngono kati ya watu wa damu inayokaribiana hili andiko lingetafsirika kiajabu sana. lingekuwa hivi.

"ili kuepuka ngono kati ya watu wanaokaribiana damu kila mwanamume awe na mke wake na kila mwanamke awe na mume wake.
 
Mzee tambua Mungu ametupa nafsi huru na amejiwekea principle za ku interact na sisi. Kama ni mtu mzima na ukaamua mwenyewe hata kama ni kwa ujinga wako tayari ndio maamuzi yako na umeapa mwenyewe.

Imagine kila mtu arudi kanisani aseme mimi nilitaka harusi tu lakini si kuishi kama mume na mke hivyo ndoa si halali ivunjwe? Unafikiri unacheza na Padre/Mchungaji hapo?

Yapo mazingira ambayo ndoa hata iliyofungwa kanisani inaweza kuwa haikuwa ndoa tangu awali na inavunjwa (hapo ndio utaona talaka sasa). Mfano mtu anajifahamu ni tasa alafu anamdanganya mwenzake hadi wanafunga ndoa, ikigundulika huo utasa ulikuwa unafahamika kabla ya ndoa maana yake hapo ndoa haikuwa halali tangu mwanzo na inavunjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeeleza vyema sana lkn nadhani haujalielewa swali langu ama unasima la maswali kwa jicho la ukorofi na majibizano,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi km mwanandoa mmoja hakuwa na uhiari wa kuunganika milele ktk shida na raha,na alienda madhabahuni kwa malengo fulani tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuana uhiari moyoni, lakini hakulazimishwa kwenda madhabahuni, wala hakulazimishwa kula kiapo, wala hakulazimishwa kuweka saini makubaliano ya ndoa.
Nia yoyote aliyokua nayo Moyoni hiyo na shauri yake, sisi hatuwezi kuitafuta hiyo bali tutaitafsiri kwa matendo yake. Kwa hivyo basi, kama ili malengo yake yatimie yanahitaji afunge ndoa basi anapaswa kuyafahamu mahitaji ya ndoa hiyo na sheria zake. Akishayaelewa na kuamua kuingia basi aelewe once in no way out.
Naipenda sana sheria ya ndoa ya Kanisa Katoliki.

Cc MTAZAMO
 
Nimemuelewa sana Padre Amigu..
Kuna mchanganyiko mwingi sana katika suala la kutoa talaka kwa mwenzi wako...hasa mume kumpa mke.....
Mambo ya mila na desturi na asili inaingilia sana pia..na ndo maana mke kuchepuka inaonekana ni kosa kubwa sana kuliko mume kuchepuka...nafikiri hii inatokana na asili ya mfumo dume ambao sio kosa la sisi binadamu lakini ni sababu ya asili...
Mfano mdogo katika historia za zamani na hata katika baadhi ya dini....mwanaume anaruhusiwa kuoa mwanamke zaidi ya mmoja na si kinyume chake..yaani mwanamke hawezi olewa na mtu zaidi ya mmoja..hiyo HAIPO...Kwenye biblia Wakina Daudi, Sulemani,Abrahamu..wote hawa walikua na wake wengi na bado Mungu aliwabariki..
Mababu zetu walikua wanaoa wanawake wengi....na ilikubalika sana tu....
Argument yangu inajaribu kuonesha uzito wa kwa nini ni rasihi zaidi kumpa talaka mwanamke aliesaliti ndoa kuliko mwanaume akiesaliti ndoa......ingawa kwa ujumla hakuna anaepaswa kusaliti..lkn incase ikitokea..uzito wake unakua tofauti...
Mfano mwingine...kipindi tunakua...UKISIKIA KAKA YAKO amelala nje...au katoka na msichana kimapenzi..halikua tatizo kivile au issue kubwa...LAKN SASA Dada ikijulikana katoka na mtu au kachepuka..ni vita vikuu
Kwa maoni yangu kinachofanya ndoa zivunjike baada ya kukamatana usaliti wengi wetu hatuangalii the Morality point of view lkn tunaangalia upande wa Magonjwa....
Najaribu kuwaza hali ingekuaje kama haya magonjwa kama UKIMWI yasingekuwepo nafikiri ukali wa kuachana sababu ya uzinzi, uasherati ingepungua....watu wangekua wanatenganishwa..then hasira zikipungua wanaendelea na maisha....kwa miaka ni ngumu hata kama ukimdamehe..magonjwa ni mengi sana hivyo itakua hatar sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amigu mara nyng anajibu maswali kwa historia badala ya maandiko
 
Hakuana uhiari moyoni, lakini hakulazimishwa kwenda madhabahuni, wala hakulazimishwa kula kiapo, wala hakulazimishwa kuweka saini makubaliano ya ndoa.
Nia yoyote aliyokua nayo Moyoni hiyo na shauri yake, sisi hatuwezi kuitafuta hiyo bali tutaitafsiri kwa matendo yake. Kwa hivyo basi, kama ili malengo yake yatimie yanahitaji afunge ndoa basi anapaswa kuyafahamu mahitaji ya ndoa hiyo na sheria zake. Akishayaelewa na kuamua kuingia basi aelewe once in no way out.
Naipenda sana sheria ya ndoa ya Kanisa Katoliki.

Cc MTAZAMO
Kwa hyo tapeli akifunga ndoa na mtu asiye tapeli wa ndoa na baada ya kutimiza malengo yake akasepa na kumuacha mwenye dhati pekee nayo itaitwa ndoa halali na imeunganishwa na Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kile kiapo cha ndoa kwenye madhabahu kuwa upo tayari kwenye shida na raha uliapa kwa Mungu huku wanadamu akiwemo mchungaji wanakuwa mashahidi tu. Kwani uliweka exemption kwenye kiapo kuwa akizini sitavumilia?

Ndio maana tunaaswa kuwa makini na kumshirikisha Mungu unapotafuta mwenza. Padre/mchungaji anapokuhoji kuwa maamuzi hayo unayotaka kufanya mbele za Mungu kama ni hiari yako mwenyewe bila influence yeyote na ukakiri umeamua mwenyewe ujue uzito wa kukiri kwako. Hakuna kurudi nyuma tena, Ndoa ni utume.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwani exemption tunaruhusiwa kuweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hyo tapeli akifunga ndoa na mtu asiye tapeli wa ndoa na baada ya kutimiza malengo yake akasepa na kumuacha mwenye dhati pekee nayo itaitwa ndoa halali na imeunganishwa na Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Najua unapotaka kwenda, ila maana ya ndoa haitabadirika hadi hapo itakapobainika kulikua na nia tofauti. Sababu tu ya binaadam kutokuwa na uwezo wa kuyaona yaliyo jificha moyoni hiyo haindoi maana ya ndoa kuwa imeunganishwa na Mungu. Atakayefanya atapeli na na heri iwe juu yake.
Hata katika maisha ya kawaida tunayaona kwamba sababu tu aliyeshinda mwingine akatangazwa mwingine, hiyo haiondoi aliyetangazwa kuendelea kutambulika na kuapishwa
 
Back
Top Bottom