Ku-Cheat": Biblia Inakuitaje Dhambi Hii?

Ku-Cheat": Biblia Inakuitaje Dhambi Hii?

Oscar Wissa

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
128
Reaction score
196
HAIITWI “KU-CHEAT”…

Biblia inaiita:

• KUZINI
“Usizini.” — Kutoka 20:14

• UASHERATI
“Uikimbieni zinaa…” — 1 Wakorintho 6:18

• HIYANA KWA MWENZI WA UJANA WAKO
“Bwana amekuwa shahidi kati yako na mke wa ujana wako, ambaye umemtendea kwa hiyana…” — Malaki 2:14

• KUVUNJA AGANO
“Kwa sababu Mungu anachukia talaka na mtu anayemtendea mwenzi wake kwa jeuri.” — Malaki 2:16

• UPUNGUFU WA AKILI
“Afanyaye uzinzi hana akili kabisa…” — Mithali 6:32

• KUHARIBU NAFSI YAKO MWENYEWE
“Afanyaye uzinzi… hujiangamiza nafsi yake.” — Mithali 6:32

• DHAMBI DHIDI YA MWILI WAKO
“Kila atendaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” — 1 Wakorintho 6:18

• KUUZA HESHIMA YA NDOA KWA TAMAA YA MUDA
“Ndoa na iheshimiwe na watu wote…” — Waebrania 13:4

• KUMDANGANYA MUNGU NA MWENZI WAKO
“Mungu atawahukumia waasherati na wazinzi.” — Waebrania 13:4

Siku hizi dunia imepunguza uzito wa dhambi kwa kubadilisha majina yake.

Wanasema:
“Ni mistake tu…”
“Ni ku-cheat tu…”
“Ni distraction…”
“Ni fun…”

Lakini mbele za Mungu:
Ni usaliti.
Ni hiyana.
Ni kuvunja agano.
Ni dhambi.
 
NAMNA YA KUSHINDA DHAMBI.

Ukweli ni kwamba tupo kwenye kizazi cha uzinzi na dhambi kama Yesu alivyothibitisha kwa ushahidi wa neno...

Marko 8
38 Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.

Kwa sababu hiyo kundi kubwa la watu hasa vijana kwenye kizazi hichi wamechukulia kuishi maisha ya dhambi ni suala la kawaida,

Na mtazamo umejengeka kuwa ni vigumu mno kwa mtu kuishi bila kutenda dhambi.

Kwa ushahidi wa neno la Mungu nitakuonyesha namna ya kufanya ili kushinda dhambi jumla...

1.KUWA NA HOFU YA MUNGU YA KWELI

Mwanzo 39
9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?

Yusuph alipata Fursa ya kutenda dhambi ila kwa sababu ya hofu ya Mungu hakufanya hivyo.

Vitu ambavyo hofu ya Mungu inaleta kwa mujibu wa andiko hili:-

i.inakupa kujua thamani yako hivyo starehe ya muda mfupi itapoteza uzito kwako.

II.itasababisha uheshimu na uzingatie miiko ya nafasi uliyopewa bila kufanya mambo yatakayoumiza watu wengine.

III.itakufanya kuepuka fursa ya kutenda dhambi bila kujali mazingira yanakuruhusu na hakuna anayekuona.

2.KUFUATILIA VITU VINVYOKUJENGA NA KUEPUKA VITU VISIVYOKUJENGA.

Lazima uwe makini unachoangalia na unachotazama kwenye mitandao ya kijamii na mazingira unayo kuwepo Kila siku.

Tumia fursa ya kuwepo mahali au mitandaoni kujijenga na sio kufuatilia mambo yatakayokuingiza katika ushawishi wa kutenda dhambi
Mfano.kuangalia picha za uchi,video za ngono,na kujihusisha na uchafu wowote.

1 Wakorintho 15
33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

3.KUEPUKA MARAFIKI WABAYA.

Kuna watu ukiambata nao wanageuka sumaku ya kukuvuta kwenye upande unaweza kupelekea uanze kuwa na tabia kama zakwao hata kama mwanzo haikuwa hivyo.

Mithali 13
20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

Mithali 1
10 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.

4.KUWA NA MAJUKUMU YA KUFANYA.

Jiweke busy na kazi ili usiwe na muda wa kupoteza kwenye mambo yasiyofaa
Wanaofanya dhambi wengi ni kwa sababu wapo huru muda mwingi hawana majukumu ya kufanya na muda huo unawapa nafasi ya kujiingiza kwenye matendo ya dhambi.

2 Samweli 11
1 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu.

2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.

3 Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?

4 Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.

Usipokuwa na kazi shetani atakupa kazi ya kufanya .

5.JIWEKE CHINI YA MALEZI YA KIROHO.

Lazima uwe na mahali ambapo unalelewa Kiroho na mtumishi wa Mungu mwamminifu na ukubali kuwajibishwa na kutoa ripoti ya maendeleo yako.

Huyu atakufuatilia na kukusaidia kuishi maisha ya kumpendeza Mungu mbali na dhambi.

2 Timotheo 2
22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

6.KUISHI MAISHA YANAYOONGOZWA NA MAONO.

Usiishi kiholela tu
Uwe na picha unyotaka iwe utambulisho wako katika Maisha
Uwe na picha ambayo Kila ukiiangalia inakukumbusha kuepuka dhambi kwa gharama yoyote

Ni ukweli usiopingika kwamba watu wasio na maono wanafanya dhambi za rejareja maana hawana Cha kuwazuia.

Mithali 29
18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

7.KUWA NA HURUMA NA KIZAZI KILICHOPO NA KINACHOFUATA BAADA YAKO.

Madhara ya dhambi hayaaishii kwa mtenda dhambi peke yake Bali yanavuka mpaka kwa jamii na Dunia kwa ujumla.

Madhara ya dhambi hayaishii kwako tu
Dhambi inakuathiri wewe na kizazi chako baada yako
Maana yake chochote unachofanya wakati huu kitaathiri na uzao wako baada yako
Usikubali kuharibu kizazi chako chote na kukiingiza kwenye matatizo ya kudumu.

Ezekieli 18
2 Je! Maana yake ni nini hata mkatumia mithali hii katika Israeli, mkisema, Baba wamekula zabibu mbichi, nao watoto wakatiwa ganzi la meno?

Kama umekwama dhambini kabisa na unahitaji msaada wa kiroho tuwasiliane 0755788312

Pastor Emanuel Clement Malogo
23.04.2026
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom