Padre Amigu; Tafsiri potofu juu ya Talaka

Padre Amigu; Tafsiri potofu juu ya Talaka

Ukitaka kuelewa kusudio la jambo fulani kuwekwa na Mungu inabidi usome kwa mapana kile alichosema kwenye maandiko tofauti ili upate ukamilifu wa fundisho la Mungu. Mume na mke ni mwili mmoja na kama Mungu anasema ni mwili mmoja iweje tena aruhusu kuwe na sababu ya kufanya mwili huo kutengana? Mantiki tu ya mwili mmoja ni kifungo kuwa hakuna kutengana.

Pili hata Yesu wakati anawajibu waliomuuliza habari za talaka kuwekwa na Musa aliwaambia Musa aliweka sababu ya mioyo yenu migumu! Maana yake talaka si mpango wa Mungu na hapo ndipo Yesu akawa ametilimiza torati kama alivyotimiliza kwenye mengine.

Kwa ujumla hako ka mstari ndio kamekuwa kakileta ushetani wa talaka kwa baadhi ya makanisa hasa binafsi. Hakuna mstari mwingine unaounga mkono talaka na ndio maana tunapopata wanazuoni kama hawa akina Padre Amigu kufafanua tunaelewa kwanini ilikuwa ha make sense huo mstari kuwepo kama umesoma maandiko yote juu ya ndoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini huo mstari ndio kauli ya Yesu kuhusu ndoa na talaka. Na Bwana Yesu ni absolute ya mkristo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini huo mstari ndio kauli ya Yesu kuhusu ndoa na talaka. Na Bwana Yesu ni absolute ya mkristo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tatizo labda Yesu aliongea kwa Kiaramu alafu waandishi wakaandika kwa kigiriki au kiebrania alafu waswahili wakatafsiri huku wakidesea kwenye tafsiri ya kiingereza. Hapo lazima kuna uwezekano mkubwa baadhi ya mantiki kukosewa. Tena wakati tafsiri kwenda kiswahili inafanyika lugha yenyewe ilikuwa changa isiyojitosheleza kwa maneno yanayoleta mantiki ile tofauti.

Binafsi naona hata hizi applications za biblia za kwenye mitandao inabidi uwe makini sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kile kiapo cha ndoa kwenye madhabahu kuwa upo tayari kwenye shida na raha uliapa kwa Mungu huku wanadamu akiwemo mchungaji wanakuwa mashahidi tu. Kwani uliweka exemption kwenye kiapo kuwa akizini sitavumilia?

Ndio maana tunaaswa kuwa makini na kumshirikisha Mungu unapotafuta mwenza. Padre/mchungaji anapokuhoji kuwa maamuzi hayo unayotaka kufanya mbele za Mungu kama ni hiari yako mwenyewe bila influence yeyote na ukakiri umeamua mwenyewe ujue uzito wa kukiri kwako. Hakuna kurudi nyuma tena, Ndoa ni utume.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wenye mitazamo kama yako ndiyo wanaongoza kufa kwa magonjwa ya moyo na kiharusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hivyo mkuu ukamfuma wife anabanduliwa wewe utachukua uamuzi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna tofauti kati ya talaka na kutengana.
Kuna mambo yanayoweza kusababisha wanandoa kutengana lakini sii kutalakiana.
Hivyo basi hata kama mmetengana inakuwa bado mpo katika kifungo cha ndoa na ukioa au yule mke akiolewa wakati wote mliotengana mpo hai hata kama hiyo ndoa imefungwa na askofu mkuu au kadinali mbele za Mungu inabaki kuwa uzinzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naongezea kwa kushikamaniza na Cement;
Alichounganisha Mungu binaadam hawezi kukitenganisha.
Ndoa huunganishwa na Mungu kwa ridhaa ya wanandoa wawili. Hivyo basi kama ndoa imeunganishwa na Mungu halafu mtu akatoa au akadai talaka sababu mwenzi wake amechepuka maana yake hapa yule aliyechepuka na mmoja wa wanandoa hawa anapewa uwezo na utukufu wa ki-Mungu...wa kutenganisha kilichounganishwa na Mungu ambacho Mungu mwenyewe alimuondolea mwanadam uwezo huo.
angalia maandiko sio utashi na hisia tu
 
Kutokana na hasira na kutokusamehe kwako na Kanisa likajiridhisha kuwa kwa muda huo kuishi pamoja ni hatari kwenu mtatenganishwa hadi mtaposamehana. Mkitenganishwa wote mtaishi bila kumjua mume/mke.

Ila kutokusamehe nacho ni kifungo maana Mungu hapokei sadaka ukiwa na neno na ndugu yako na maana maandiko yanasema kabla ya kutoa sadaka jiulize kwanza hilo swali.

Sent using Jamii Forums mobile app
tunataka andiko linalotoa mwonozo huo au ni fikra za wachungaji tuu
 
Back
Top Bottom