Kwa maoni yangu tayari serikali ya Marekani ishadondosha mpira kwenye hili kwa sababu sasa hata wakitoa bado watu watahoji authenticity ya hiyo au hizo picha. Kwenye mambo ya PR kama hili hutakiwi ku dillydally.
Pia sasa eti inasemekana Osama hakuwa na silaha yoyote ile na wala hakutoa resistance yoyote ile. Sasa kwa nini wasingemkamata wakamweka kwenye hifadhi yao kama walivyofanya kwa Saddam. Kwa Saddam tuliona hadi video footage akifanyiwa physical huku nywele zake zikiwa timtim.
Hii ya Osama inaibua maswali mengi mno. Kila kitu kimefanywa haraka haraka utadhani alikuwa mtakatifu. Pia tunaambiwa eti kazikwa (mimi nadhani kadondoswa tu baharini na hiyo ni kama kweli wamemuua kama wanavyodai)kwa kufuata taratibu za dini yake. Eti kabla ya "kuzikwa" aliombewa. Hiki nacho ni kichekesho. Huyo aliyemwombea ni nani? Ndugu au Imam wa Kimarekani?
Things just don't add up for me.