Orodha ya madaktari na maeneo wanayosali/abudu

Orodha ya madaktari na maeneo wanayosali/abudu

Kutokana na mfumo wa nchi hii, wa kuwa ni nchi isiyo na dini lakini watu wake wanadini, na kwamba nikiamini kuwa madaktari karibu wote watakuwa waumini wa dini na madhehebu mbalimbali. Hii inanipa fursa ya kutaka kufahamu kama ni waumini wazuri katika dini zao, kwani hofu yangu ipo katika maeneo yafuatayo;
1.kama watakuwa ni waumini wazuri, kushiriki kuwatesa na kuwasababishia vifo watu wasio na hatia, huku wakifahamu wazi kwamba ni dhambi kutenda matendo kama hayo.
2.Kama kweli ni waumini na wanamwamini mwenyezi Mungu, wao huenda kutubia madhambi gani?
3.Kama wanaishi kwenye jamii ya watanzania na endapo patatokea kifo au msiba unaotokana na mgomo wao, je watashiriki mazishi?
4.Je madaktari hawa tunawahitaji katika dini zetu na madhehebu yatu? akiwa jirani yako ungependa ahame?
5. Je,Tatizo ni kwamba kipato wanachopata kwasasa kinaweza kuwasababishia kifo madaktari ndio maana wanajihami kabla hawajafa na kwamba hakuna njia nyingine wanayoweza kuitumia zaidi ya kuwatesa wananchi na kuwaua ili nawao waweze kuishi.
6.Inavyoonekana wadaktari hawa hawajasoma au kusomeshwa na kodi za wananchi wanaowatesa sasa na kuwauwa, hivyo wanataka kurejeshewa gharaza zao walizotumia wakati wanasoma vyuo.
7.Kwamba kutokana na mateso na vifo vitakavyo tokana na mgomo wao, manufaa na maisha bora yatapatikana na hivyo kuifunza serikali sikunyingine wasiwachezee tena kwani wananchi watakuwa wamekiona chamoto.
8.Kwamba wao hakuzaliwa katika hospitali za watanzania na hawakuhudumiwa na madaktari na wahudumu wengine wa afya, hivyo haiwahusu kuhusiana na maisha ya wananchi wengine.
9.Walimu na watumishi wengine si wamuhimu sana kwani wao wamejifundisha taaluma hizo kwa juhudi zao binafsi, hivyo hakuna haja ya kuangalia uwianao wa kimaslahi,na pia si msingi mkubwa wala sababu ya wao kutopata maisha mazuri.
10.Kuwafunza na kuwapa uzoefu wale wote wanaotaka kusoma basi wachague kuwa madaktari kwani wanaogopwa sana, na wakati unasoma unapewa fedha kama grant 100% na sio mkopo kama wanafunzi wengine

Kutokana na sababu nilizoainisha hapo juu,madaktari kufanya mgomo inapaswa waungwe mkono?njia wanayotumia ni sahii?
MUSSA -0763623082
Kwanini hiyo namba moja isiwahusu viongozi wa serikali wanaotibiwa India wakati wananchi wake wanakosa huduma bora za afya na kupoteza maisha yao kwa kukosekana kwa vitendea kazi na madawa hata ya bei rahisi? Hujawahi kuona vijiji vilivyopewa matoroli/guta ili waweze kuwasafirisha wagonjwa wao? Umeshazunguka huko vijijini ukaona hali ilivyo mbaya kwenye hospitali za serikali? kwanini unataka serikali iendelee kuwatesa madaktari kwa kuwaangalia kila siku wagonjwa wakifia mikononi mwao kwa kukosa tu dawa/vifaa hata vile vya bei nafuu? Gia yako ya kisensasensa inaonyesha wewe utakuwa ni mtu wa ubwabwa tu...
 
Kaka yangu Mussa,njia waliotumia madaktari ni sahihi na nawaunga mkono kwa sababu zifuatazo 1) Whether kuna mgomo au la,watu hufa mahospitalini
2)Umejikita katika maslahi hasa mishahara,nataka nikwambie habari za mishahara na posho ni sehemu tu
ndogo ya madai yao,kikubwa ni vifaa kwa ajiri ya huduma wanayotoa.Na hili si kwa faida yao ni kwa ajiri
yawananchi

3)Madaktari wana uchungu na wagonjwa kuliko serikali,hii inathibitishwa na ahadi za serikali kwa madaktari
zisizotekelezeka.Kama serikali ina uchungu na wananchi wake kwanini isitekeleze makubaliano?
4)Ni dhahili kabisa kwamba kwa kazi wanazofanya madaktari na mishahara yao haviendani,ukizingatia
wabunge wanasinzia tu bungeni na kuondoka na 10 m kwa mwezi.
Mwisho nirudie kuwapongeza madaktari kwa kugoma,lakini pia nitumie fursa hii kuelekeza lawama zangu kwa serikali kwa kutoonyesha nia ya kweli ya kuokoa maisha ya watanzania maskini.Kweli nimeamini aliyeshiba hamjui mwenye njaa,familia za viongozi zinatibiwa nje ya nchi na hivyo hawaoni umuhimu wa kuboresha hospitali zetu.
hakuna haja ya kumjibu mtu mpumbavu asiyejua anachokiandika
 
kama kila upumbavu utapishwa na mods na kujadiliwa humu sasa naanza kupata sababu za kuachana na jf tafadhali chujeni na makapi yasiingie humuuuuuuu alaa

umeona mkuu, sasa hivi kila ukifungua thread kilichoandikwa ni upambavu tu mpaka unabaki unajiuliza hivi huu upumbavu nafurahiwa na mods au ndo mods wamelala!
 
Hao madaktari waliofanya mgomo ilipaswa wananchi tuchukuwe sheria mkononi tukawape kichapo kama tunavyowapa vibaka. Tukiwatandika wawili watatu wengine watarudi kazini au wataacha kabisa udaktari.

Serikali hawa ndio wakuwashughulikia ipasavyo. Sasa fungeni madai yao yote, wakatafute pa kufanya kazi. Na wote wanaogoma wasiruhusiwe kufanya kazi za udaktari hata private hospitals.

kichapo akirudi kazini..mgonjwa..Doz 1X12, Upasuaji PUA badala ya kidole
 
Mgomo wa madaktari unapashwa utazamwe kwa mapana na marefu. Kwa maoni yangu, tatizo hapa siyo udogo wa mshahara au posho, ugomvi ni mgawanyo wa hako kasungura miongoni mwa wanajamii wa Tanzania; Kila mtu anaona kwamba linapokuja suala la mgawanyo wa pato la taifa, hao walioko jikoni wanajipendelea mno. kwa jinsi walivyojipangia mishahara na marupurupu wao wanaishi katika sayari ya kwao, tofauti na watanzania wengine. Hiyo ni dhuluma hisiyokubalika na hivyo nafarijika kuona kwamba kuna watanzania ambao wako tayari kuhatarisha ajira zao kwa kupiga vita dhuluma hiyo kwa vitendo. Najua fika kwamba hatua hiyo uenda ikahadhiri baadhi ya watu, hata hivyo, kwangu mimi naichukulia kuwa hiyo ni gharama ndogo ikilinganishwa na mamilioni ya watu wanaokufa kwa utapia mlo, na magonjwa yanayotibika, lakini ambayo kwao wanashindwa kuyashughulikia kutokana na umasikini wa kipato unao sababishwa na ulafi uliokithiri wa hao walioko jikoni. NATOA RAI KWA WATANZANIA WOTE, KWAMBA TUSIKUBALI KUDANGANYWA, KAMA KUNA YEYOTE ATAKUFA KUTOKANA NA MGOMO HUU WA MADAKTARI, WA KUSHIKIA BANGO NI WALE WALIOKO JIKONI AMBAO WAMEAMUA KUKOMBA CHAKULA CHOTE NA HIVYO KUTUFANYA WENGINE WOTE TUAMBULIE MAKOMBO
 
Mimi Reagan, sijawhi kuona wala kusikia yafuatayo toka nchi hii ipate uhuru
1) Rais au Makamu wa Rais akitokea kaskazini
2) Mkuu wa majeshi TPDF akitokea uchaggani
3) Waziri mkuu au waziri wa mambo ya nje akitokea kaskazini

Na UVCCM wakakoleza chumvi kwa tamko lao la Kibaha.H uyu chakula maalum cha wakuu wa serikali dhaifu atajibu nini tukisema hoja hizi ni za kupuuza na inabidi wahusika washtakiwe kwa uchochezi na baadhi yao uhaini?

Mchango wa kila mkoa kwa pato la Taifa hauna uwiano kiuongozi maana Pwani wasingakaa watoe hata RC. Lakini hatutaki kujenga hoja kidini, kikabila, kikanda au kijinsia. ccm wamethubutu ktk hayo, hata kwa nafasi muhimu kama spika waliiitumia. CCM need to be ousted soonest
 
Tangia nianze kuingia humu jamvini sijawahi kuona comrade zomba katoa point! Mchukulieni jinsi alivyo, ni mchemkaji!
 
Tuanze kukusanya facts kabla ya kutoa conclusions. Maswali haya yajibiwe na madaktari au anayejua kilichotoke.
1. Madaktari walipogoma awamu ya pili, viongozi wao walikutana na Rais na kujadiliana naye kwa muda ulioripotiwa kuwa zaidi ya masaa sita. Muda huu ni hakika yatakuwa yamezungumzwa mengi baina yao. Je, baada ya watendaji wa serikali kutokutimiza "ahadi za serikali" na kutokidhi matumaini ambayo Rais aliwapa madaktari, viongozi wa madaktari walirudi kwa Rais kuelezea kutoridhishwa kwao na utendaji huo?
2. Kama walirudi kwa Rais, je walijibiwa vipi?

Tukipata majibu ya maswali haya tunaweza kupata picha halisi kama hatua zinazufuatwa katika utatuaji wa mgogoro huu ni za kisomi au za kisiasa kutoka katika pande zote mbili yaani serikali na madaktari.
 
Mbona mnajaribu kukwepa ukweli haya yote ni kutokana na Serikali dhaifu na rais dhaifu hivi mmejaribu kuangalia katika hayo madai kwanza jambo la kwanza linahusu kuboresha mazingira ya kazi pamoja na vitendea kazi ambavyo vitasaidia kupunguza vifo ambavyo vingeweza kuzuhlika na utoaji wa huduma ukawa bora. sasa nadhani wote mmeona bajeti ya serikali inasema kwamba afya na elimu ya wananchi ingoje fedha kutoka kwa wahisani huku posho na allowance za vikao vya mabwana wakubwa na ma vx hizo ziko limited yaani ni kusaini tu na unapewa lakini hawa hamuoni kama wanauwa wananchi nyie mnakimbilia kwa madaktari jamani tuwe tuna reason kwanini tumefika hapa. sasa hivi wahisani waliokuwa wanafadhili miradi mingi ikiwemo ya Ukimwi wamejitoa na tulikuwa tunawategemea asilimia 100% na kulingana na bajeti hiyo tumeshajua watu wangapi watakufa kwa kukosa huduma bora sasa hili hamlioni?
Kutokana na mfumo wa nchi hii, wa kuwa ni nchi isiyo na dini lakini watu wake wanadini, na kwamba nikiamini kuwa madaktari karibu wote watakuwa waumini wa dini na madhehebu mbalimbali. Hii inanipa fursa ya kutaka kufahamu kama ni waumini wazuri katika dini zao, kwani hofu yangu ipo katika maeneo yafuatayo;
1.kama watakuwa ni waumini wazuri, kushiriki kuwatesa na kuwasababishia vifo watu wasio na hatia, huku wakifahamu wazi kwamba ni dhambi kutenda matendo kama hayo.
2.Kama kweli ni waumini na wanamwamini mwenyezi Mungu, wao huenda kutubia madhambi gani?
3.Kama wanaishi kwenye jamii ya watanzania na endapo patatokea kifo au msiba unaotokana na mgomo wao, je watashiriki mazishi?
4.Je madaktari hawa tunawahitaji katika dini zetu na madhehebu yatu? akiwa jirani yako ungependa ahame?
5. Je,Tatizo ni kwamba kipato wanachopata kwasasa kinaweza kuwasababishia kifo madaktari ndio maana wanajihami kabla hawajafa na kwamba hakuna njia nyingine wanayoweza kuitumia zaidi ya kuwatesa wananchi na kuwaua ili nawao waweze kuishi.
6.Inavyoonekana wadaktari hawa hawajasoma au kusomeshwa na kodi za wananchi wanaowatesa sasa na kuwauwa, hivyo wanataka kurejeshewa gharaza zao walizotumia wakati wanasoma vyuo.
7.Kwamba kutokana na mateso na vifo vitakavyo tokana na mgomo wao, manufaa na maisha bora yatapatikana na hivyo kuifunza serikali sikunyingine wasiwachezee tena kwani wananchi watakuwa wamekiona chamoto.
8.Kwamba wao hakuzaliwa katika hospitali za watanzania na hawakuhudumiwa na madaktari na wahudumu wengine wa afya, hivyo haiwahusu kuhusiana na maisha ya wananchi wengine.
9.Walimu na watumishi wengine si wamuhimu sana kwani wao wamejifundisha taaluma hizo kwa juhudi zao binafsi, hivyo hakuna haja ya kuangalia uwianao wa kimaslahi,na pia si msingi mkubwa wala sababu ya wao kutopata maisha mazuri.
10.Kuwafunza na kuwapa uzoefu wale wote wanaotaka kusoma basi wachague kuwa madaktari kwani wanaogopwa sana, na wakati unasoma unapewa fedha kama grant 100% na sio mkopo kama wanafunzi wengine

Kutokana na sababu nilizoainisha hapo juu,madaktari kufanya mgomo inapaswa waungwe mkono?njia wanayotumia ni sahii?
MUSSA -0763623082
 
kichapo akirudi kazini..mgonjwa..Doz 1X12, Upasuaji PUA badala ya kidole

Kichapo cha vibaka huwa anarudi kazini? baada ya kichapo huwa ni moja kwa moja mortuary.
 
Madakitari hawana wajibu na afya za watanzani,,serekali ndo inapaswa kutoa afya kwa wananchi wake,,,kama wabunge imewezekana kuwalipa mil1o kwa mwezi...450000/- kwa siiku kwa ajili ya watu wa tume ya kukusanya maoni,,kwa nn ishindikane kwa madakitar?

Mkuu Serikali DHAIFU na Bunge DHAIFU wanafanya maamuzi DHAIFU! Wananchi tunapaswa kuamka sasa na kudai mgawanyo halali wa mapato ya kodi zetu! Tunadanganywa eti Watanzania wote tuko sawa ila kiukweli kuna walio sawa kuliko wengine! (cfr. The Animal Farm - "All animals are equal but some animals are more equal than others"!!!
 
Tuanze kukusanya facts kabla ya kutoa conclusions. Maswali haya yajibiwe na madaktari au anayejua kilichotoke.
1. Madaktari walipogoma awamu ya pili, viongozi wao walikutana na Rais na kujadiliana naye kwa muda ulioripotiwa kuwa zaidi ya masaa sita. Muda huu ni hakika yatakuwa yamezungumzwa mengi baina yao. Je, baada ya watendaji wa serikali kutokutimiza "ahadi za serikali" na kutokidhi matumaini ambayo Rais aliwapa madaktari, viongozi wa madaktari walirudi kwa Rais kuelezea kutoridhishwa kwao na utendaji huo?
2. Kama walirudi kwa Rais, je walijibiwa vipi?

Tukipata majibu ya maswali haya tunaweza kupata picha halisi kama hatua zinazufuatwa katika utatuaji wa mgogoro huu ni za kisomi au za kisiasa kutoka katika pande zote mbili yaani serikali na madaktari.
inaonekana unajua yaliyojiri vizuri sana.hebu tueleze!
Unajua kuwa kuna kopi ya barua ya wawakilishi wa madaktari juu ya mwenendo wa mazungumzo kati ya pande hizi mbili iliyotumwa kwa jk?
Ni vizuri ukaiuliza serikali nini kilifanyika baada ya mazungumzo kuonyesha mwelekeo wa kukwama?jambo ninaloliona ni kuwa serikali inatumia muda na rasilimali nyingi kutafuta public sympathy badala ya kulenga kiini cha mgogoro huu.madai yalioko mezani sio ya juzi au jana,je unaweza kuonyesha jitahada za dhati za serikali
kushughulikia?
Miezi mitatu iliyopita tulishuhudia mgomo wa madaktari ambao haujawahi kutokea,je kwenye bajeti ya sasa kuna sehemu serikali imeonyesha kupata somo na hivyo kuweka mikakati itakayozuia mgomo wa namna hii kutokea?
Nikupe mfano mmoja tu...ambao utausikia bungeni siku chache zijazo,katika bajeti ya mwaka huu fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa imepungua kulinganisha na mwaka jana...ni kweli serikali iko serious na afya za wenyenchi?je srikali ilizingatia migomo iliyopita katika kupanga bajeti ya afya mwaka huu?
 
Masikini Musa Loth, watu kama wewe ndio mtaji wa mafisadi wa CCM!

tanzania_maternity_hosp.jpg

Tanzania_mothers_459847artw.jpg

IMG_8413.JPG

Masikini Musa Loth, picha hizi zinakupa ujumbe gani?
Katika mazingira haya, Daktari afanye nini?
Wakati huo huo;

asset.php

​
 
Samahani mleta mada naomba nikuulize swali dogo tu; ivi ulishawahi kumuuliza mama yako mzazi kwamba ulilia baada ya mda gani siku uliyozaliwa? Mi nina walakini na hili!!!!!
 
Nijiavyo mimi hawa watu waligoma siku nyingi labda sasa wanachofanya ni kumalizia tu? NA PILI hii ni mtaji kwa waganga wa kienyeji.

pili naomba kama kuna mtu anajua serikali inawalipa bei gani madaktari aiweke hapa watanzania wanataka kuona hali halisi
 
Kutibia wagonjwa bila mask jamani hata ili nalo......yani mask nayo hadi mtu agome????
Umeshawahi kupata TB wewe??? Na utasema pia hata gloves inawagomesha madaktari jaribu kupata hepatitis au HIV ndio labda utawaelewa au ikiwezekana njoo nikuwekee hao viruses na ufurahie sequele ya ugonjwa labda utawaelewa.
 
inaonekana unajua yaliyojiri vizuri sana.hebu tueleze!
Unajua kuwa kuna kopi ya barua ya wawakilishi wa madaktari juu ya mwenendo wa mazungumzo kati ya pande hizi mbili iliyotumwa kwa jk?
Ni vizuri ukaiuliza serikali nini kilifanyika baada ya mazungumzo kuonyesha mwelekeo wa kukwama?jambo ninaloliona ni kuwa serikali inatumia muda na rasilimali nyingi kutafuta public sympathy badala ya kulenga kiini cha mgogoro huu.madai yalioko mezani sio ya juzi au jana,je unaweza kuonyesha jitahada za dhati za serikali
kushughulikia?
Miezi mitatu iliyopita tulishuhudia mgomo wa madaktari ambao haujawahi kutokea,je kwenye bajeti ya sasa kuna sehemu serikali imeonyesha kupata somo na hivyo kuweka mikakati itakayozuia mgomo wa namna hii kutokea?
Nikupe mfano mmoja tu...ambao utausikia bungeni siku chache zijazo,katika bajeti ya mwaka huu fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa imepungua kulinganisha na mwaka jana...ni kweli serikali iko serious na afya za wenyenchi?je srikali ilizingatia migomo iliyopita katika kupanga bajeti ya afya mwaka huu?

Maelezo yako mazuri sana. Asante, sasa toa jibu la swali nililouliza. Madaktari wakurudi kwa Rais kuelezea kutokuridhika kwao? Je, Rais aliwajibu nini?
 
Back
Top Bottom