Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 45,585
- 135,551
Huu uonevu haivumiliki. Biashara nyingi kwa sasa zimeyumba kutokana na huu mdororo wa uchumi unaondelea nchini! Wafanyabiashara wanahangaika kupambana na marejesho, hali ngumu ya biashara, nk. Unachelewa kulipa kodi kabla ya tarehe 30, eti unapigwa penati ya laki 2! Kama siyo upumbavu ni nini?Kwann mtu akichelewa kufile return siku moja tuu fine ina anza 200k
Majitu yanashinda ofisini, hayajui chochote kuhusu hali ya biashara mtaani, makadirio yao yenyewe ya kodi hayana uhalisia! Na bado yanaumiza wafanyabiashara kwa kuwalipisha faini za uonevu, na mwisho wa mwezi waje kujisifia wamevunja rekodi ya makusanyo ya kodi!! How come kodi inageuka kuwa kama marejesho ya Vikoba? Hivi hii faini nikigoma kulipa na kuamua kufunga biashara, watanifanya nini?
I wish ningekuwa Rais. Wafanyakazi wengi wa TRA mngekuwa mnashinda mtaani kwenye jua ili mjifunze nini maana hasa ya kufanya biashara kwa nchi isiyo na msaada wowote ule kwa wafanyabiashara kama Tanzania.