Selous
JF-Expert Member
- Jan 13, 2008
- 1,325
- 145
Shadrack Sagati
Daily News; Saturday,May 31, 2008 @00:05
Kundi la vichekesho la Ze Comedy limetangaza kuhamishia maonyesho yake katika runinga ya Taifa ya TBC1 kuanzia Julai. Wachekeshaji hao waliokuwa wakifanya shughuli zao East Africa
Television Channel 5 pia wamemtangaza Mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia ni mfadhili wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji kuwa mlezi wao ambaye atakuwa na jukumu la kuwagharimia katika safari mbalimbali watakazozifanya kwa ajili ya maonyesho.
Mkurugenzi Msaidizi wa kundi hilo, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kundi hilo limeingia mkataba wa mwaka mmoja na kituo hicho.
Tunatangaza rasmi kuwa tayari tumesaini mkataba mnono na TBC1 kwa kweli ni mkataba wa heshima na unajitosheleza ndio maana tumeamua kufanya kazi na kituo hicho, alisema Masanja jana.
Kitendo cha wachekeshaji hao kumtangaza Manji kama mlezi wao kinaweza kuzusha hisia mbalimbali miongoni mwa wapenzi wao hasa kutokana na uhasama wa kibiashara uliopo kati ya Manji na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi.
Hata hivyo wasanii hao wameweka bayana kuwa wao ndio waliomwomba Manji awe mlezi wao na suala hilo halihusiani na chuki za kibiashara zilipo kati ya mlezi huyo na Mengi ambaye ndiye mmiliki wa Channel 5 kupitia Kampuni ya IPP.
Masanja alisema wamemteua Manji kuwa mlezi wa kundi lao kutokana na kuamini kuwa busara na umri wake atawalea vyema kama ambavyo amekuwa anafanya kwa klabu ya Yanga ambayo tangu atangaze kuifadhili imekuwa yenye mafanikio.
Tumeona mafanikio yake akiwa na Yanga kwa hiyo tunaamini kuwa sisi kundi la watu saba hatashindwa kutulea, alisema Masanja na kuongeza kwa kuanzia wiki ijayo wataenda Afrika Kusini kwa ajili ya mafunzo zaidi ya sanaa za uchekeshaji na safari hiyo itagharimiwa na mlezi huyo.
Naye muongozaji wa kundi hilo, Sekion David, Seki akizungumzia mkataba wake na TBC1 alisema kuna mambo mengi ambayo yameongezeka katika mkataba wao na kituo hicho. Mojawapo ni kuwekewa bima ya kutibiwa wao na familia zao wakati wote watakuwa ndani ya mkataba huo.
Unajua Ukimpiga teke Chura umemwongezea safari, alisema Seki ambaye kwa maelezo yake alisisitiza kuwa kulikuwa na uhuru mkubwa katika kuandaa mkataba huo Tulikuwa huru na mambo tuliyokubaliana ni ya msingi.
The Comedy ilisitisha kuonyesha vichekesho vyake katika Channel 5 baada ya mkataba wao kumalizika. Kundi hilo limesema tangu wasitishe maonyesho wamekuwa wakipigiwa simu nyingi na kutumiwa barua pepe zinazowataka warejee kwenye uwanja wa sanaa.