Marioo afunguliwa kesi ya Madai ya Tsh. Milioni 550 kwa kukiuka Mkataba wa Tamasha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1710146662739.png

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Omary Mwanga, maarufu Marioo, anayedaiwa zaidi ya Sh. milioni 500 kwa kuvunja mkataba, anatarajiwa kujitetea Mahakama Kuu Machi 18 na 19, mwaka huu.

Marioo na Meneja wake Sweetbert Mwinula wameshtakiwa katika Mahakama Kuu Masjala ya Wilaya ya Arusha mbele ya Jaji Joackim Tiganga, wakidaiwa jumla ya Sh. 550,000,000 kwa madai ya kuvunja mkataba wa kutumbuiza katika hafla ya Mr & Miss Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini.

Mdai katika shauri hilo ni Kampuni ya Kismaty inayojihusisha na kuandaa matukio ya burudani mbalimbali nchini.

Mdai anayewakilishwa na Wakili John Lairumbe, anadai kuwa Septemba 23, 2021, aliingia mkataba na wadaiwa kutumbuiza siku ya mashindano hayo kwa gharama ya Sh. milioni 15.

NIPASHE
 
Kapokea hela alafu katokea kwa tamasha amechelewa na kalewa. Kaanza kuimba eti toto bad in the building nakuwaambia watu eti ana demu mzuri. Watu wamefanya fujo mfululu mixer beto zilitembea sana. Imebidi toto bad akimbilie sentro pale chugani ambako amehifadhiwa mpaka mda huu Raia lombelombe wanataka kuruka naye kimasai. Wamesema mpaka atage yai hapo chugani.
 
Back
Top Bottom