figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,591
- 55,213
(1) Manji aliwahi kuwalipia Viingilio Mashabiki wa Yanga Mechi ya Yanga na TP MAZEMBE, Mashabiki na Wanachama Wakaingia Bure.
(2) Manji Aliwalipia Viingilio Wanachama Wa Yanga kwa Ajili ya kwenda Kuangalia Mechi ya Brazil na Taifa Stars, Brazil ya Akina Kaka.
(3) Manji alianzisha Week ya Wananchi na Kila Jumamosi kwa Miezi Miwili, Mashabiki na Wanachama wa Yanga Walikuwa Wakikutana Viwanja vya Mnazi Mmoja Wakila na kunywa gharama zote Zikibebwa na Yusufu Manji.
(4) Manji alishawahi kukodi Ma-Bus na kusafirisha Wanachama wa Yanga kutoka Dar Kwenda Morogoro kuishangilia Yanga.
(5) Manji alishawahi kuwalipia Ada ya Uanachama Wanachama Wote wa Yanga kwa Muda wa Miaka Mitatu
(6) Kipindi Hiko Jengo la Yanga likiwa Limechakaa zaidi, Manji aliweza kulifanyia Ukarabati na kulirudishia Muonekano Wa kupendeza
(7) Manji Aliwapa Yanga sehemu ya Ardhi ambayo Alikuwa anaimiliki Kigamboni ili Waweze Kujenga Uwanja Wao.
(8) Manji alikuwa na Vision kubwa sana na Yanga lakini Pia Yanga ilikuwa Moyoni mwa Manji
(9) Manji ndiye Tajiri wa kwanza kupandisha Thamani ya Usajili na Mishahara kwa Wachezaji Nchini Tanzania
Manji alisimama kama Kigezo na Kipimo Cha Mwekezaji yeyote Ndani ya Yanga na Simba
Kuna heshima ya kipekee Yusufu Manji anastahili kwenye Soka letu
Mungu Ampe Pumziko Jema Yusufu Manji
=====
Pia soma: Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani