Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 353
Sio mtaalamu wa mambo ya utabiri lakini kutokana na hii link ya Manji hapa, in the future- tegemea kuwaona Ze Comedy wakiburuzwa kortini kwa mashtaka ya kumchafulia Mengi jina.
Tusisahau kuwa tatizo la msingi ni kipato, iwapo wangekuwa wanapata malipo mazuri wasingekuwa na haja ya kutafuta kituo kingine cha TV na wala mlezi. SNL sio middle class americans.Ze Comedy ni maskini bado.
Ni muhimu kukumbuka uwa EATV pia wana media policy,hivyo basi uhuru kamili Ze Comedy wanaeweza kuwa nao iwapo tu watakuwa na TV yao.
Manji ajitosa Ze Comedy
Shadrack Sagati
Daily News; Saturday,May 31, 2008 @00:05
Kitendo cha wachekeshaji hao kumtangaza Manji kama mlezi wao kinaweza kuzusha hisia mbalimbali miongoni mwa wapenzi wao hasa kutokana na uhasama wa kibiashara uliopo kati ya Manji na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi.
...mimi namlaumu huyu mwandishi KWA HERUFI KUBWA!, kuanzia kichwa cha habari mpaka ujumbe wenyewe naona kusudio ake ni kuamsha hisia za wananchi walio wengi kuwa
"Ze Comedy + Manji = kutaka Kumsakama Mengi! "
...Kwa mawazo yangu 'kikundi' kinatengeneza movie/comedy scripts zao, kisha wanazipeleka kwenye vituo kwa mfano; EATV, au TBC ,Channel 10, au DTV hata TVZ... huko wanafanya majadiliano na 'wahariri' wa vipindi, kama hizo scripts zitauzika na kama kutakuwa na possibilities ya kuingia mkataba na kituo, penye maslahi nao mazuri ndipo wanapofunga mkataba, haijalishi hicho kituo ni cha Mengi, Manji au cha serikali...
Ulezi/udhamini wa kikundi ni tofauti na umiliki wa kikundi, ndio maana siamini kwamba Ze Comedy wamekosea kuomba udhamini kwa Manji. Hebu jiulize roughly inawagharimu kiasi gani kila week kutengeneza episode moja ya Ze Comedy? Movie production sio lele mama kama unavyoweza fikiria... panahitajika transport, locations, costumes, achilia mbali film crews etc etc etc...
hayo ni mawazo yangu tu, maybe am wrong!
Hauko wrong hata kidogo, uko very right.
Kama tunataka quality katika kazi za hawa jamaa inabidi tuweke siasa pembeni na tuwaache wafanye maamuzi yao kibiashara. Si sahihi kuanza kuwaponda kabla hatujajua hata contents za mkataba wao na Manji, hii ni dalili ya skeptism tu!
Kwa Tanzania kila kitu kinagusa siasa kama tunapenda au la na huo ndio ukweli wa mambo. Manji ana akili yake alipoamua kuwa mlezi wa Ze comedy. Kishajua atawatumia vipi ili kutaka kile anachokitaka lakini bahati mbaya hawa jamaa wa Ze comedy kutokana na uwezo wao mdogo wa kuchanganua mambo hawakuliona hilo. Tusubiri labda wanaweza wakashtuka na kuwaambia Watanzania baada ya muda kwamba Manji si mlezi wao tena kwa sababu anawaingilia katika maamuzi yao ya kupanga vichekesho vyao au vinginevyo vichekesho hivyo vitaegemea upande mmoja zaidi na Watanzania watawashtukia.
hawa vijana njaa inawasumbua, lakini hawamjui manji, atawatumia kutafuta umaarufu, akishaupata anawaacha njia panda, kama alivyowaacha yanga wakati ule. waha waajemi hawana jema na watu wetu, kwao watu wetu ni madaraja ya kuwavusha kutimiza malengo yao. after all nani angewahamu akina ze comedy kama siyo EATV?
Ze comedy ni kikundi cha burudani! Tujaribu kuweka siasa pembeni wakati mwingine.
Pamoja na kuwa hatujui mapato yao ni kiasi gani, lakini hawakustahili kujiambatanisha na Manji. Hata hawa kama wana mipango mizuri wanaweza kabisa kuwa na maisha mazuri tu bongo pamoja na kuwa yanaweza yasiwe katika kiwango cha middle class americans. Vichekesho vinastahili viwe huru, na kama uhuru wa kuandaa vipindi vyao unaingilia na mtu au kikundi cha watu basi wanapoteza kundi kubwa la wapenzi wao.