Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya

nadhani tuanakoelekea CCM kitaitwa chama cha Waislamu. Hivi CHADEMA ina asilimia ngapi ya Waislamu katika safu ya viongozi wao wa kitaifa na CCM ina asilimia ngapi ya Wakristo? Jamani mambo ya kumtetea mtu hata anapokosea eti kwa kuwa ni dini yako ni mbegu mbaya sana kwa taifa letu. Ni aibu kabisa dini kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa. Believe me endapo Mramba, Yona, Chenge, Mgonja wangekuwa ni Waislam, tusingekuwa hapa tulipo. Ni aibu kabisa. Nimesikiliza bbc ya leo asubuhi, ni aibu kwa kweli.
 
Ushenzi mtupu.
Natamani nimuone huyo shehe aliyetoa yhaya matamko.
Usikute ayiyetoa haya matamko amechanganyikiwa.
Akya Mungu hili baraza lilokaa siyo baraza bali uani.
 
Haya wote tuhamieni CUF chadema haitakiwi na waislam.
NO CUF, NO upinzani tanzania,
Chama kingine chocho kitakuwa cha kikirsto.
 
Haya wote tuhamieni CUF chadema haitakiwi na waislam.
NO CUF, NO upinzani tanzania,
Chama kingine chocho kitakuwa cha kikirsto.

kama CHADEMA ni chama cha Kikristo na CUF cha kiislamu (kigezo ni asilimia kubwa ya viongozi), Je CCM siyo cha kiislamu?

Believe me, kama CCM haitavikemea vikundi hivi vya kiislamu kwa uwazi itapoteza kura za Wakristo. Tusipo acha kuingiza siasa kwenye dini, amani itapotea.
 
Mdomo ni wake, hivyo ana haki ya kusema lolote alitakalo.

Poor Mwaipopo nafikiri alisomewa albadir ndiyo sababu anazungumzaga bila kufikiri. Hivi huyu jamaa ana elimu gani vile. Au ni yule jamaa wa mihadhara ya BARUKTA enzi zile? Nafikiri amechoka. Kama anafikiri siasa ni mchezo si na yeye aingie badala ya kuwashawishi wenzake. Akamuulize Mtikila kwanza kabla ya kujitupa ndani akifikiri kuwa sheik kutamsaidia isipokuwa asitumie pesa za sadaka za waislam kwenye kampeni!!
 
Nadhani CCM wameanza kutapatapa.Hii si mara ya kwanza kwa baadhi ya viongozi wa kiislam kukubali kutumiwa kwa manufaa ya CCm.Wanajamvi mwaka 1995 CCM kwa maksudi waliwatumia maimamu wa misikiti dhidi ya Lyatonga Mrema.
 
Kuna waislamu zaidi ya milioni kumi nchini. Nani aliyewateua hawa wakina Mwaipopo kuwa wasemaji wao? Kwa nini huyu mwandishi hakusema wakina Mwaipopo wapinga....... badala ya kuwaingiza waislamu wote? Hawa ndiyo wanaoingiza udini mahali ambapo hamna! Yaani leo mawazo ya Fundi Mchundo yawe ya wamisheni wote! Uchochezi mtupu! Iko kazi.

Amandla......
 
Waislam nchini wapinga oparesheni Sangara
Geofrey Nyang'oro na Zaina Malongo


Shekhe Saidi Mwaipopo aliwataka waisalamu kutambua kuwa chama hicho, hakina msaada wowote wa maendeleo ya uislamu kutokana na chama hicho kujaa ukabila udini na ubinafisi.



Mwananchi Read News

Shekhe Saidi Mwaipopo?
Does not sound na inaelekea kapandikizwa huyu.
Mbona hajulikani maeneo hayo, hata hivyo kachanganyikiwa(kama yupo) kwa kijiingiza kwenye siasa ambazo uchambuzi kwake imekua ndoto ya mchana!
 
cheap cheap cheap cheap... huyu sheikh anataka kuingia kwenye siasa na anatafuta njia rahisi ya kukubalika CCM (hajui bila fedha CCM huwezi kupata nafasi -- labda kama anazo).

Ni wakupuuza, mwandishi alipasa kuandika "Sheikh Mwaipopo apinga operesheni Sangara" lakini kwa kuwa ameshaandika then Baraza la waislamu ni busara likamkana na kuweka bayana kwamba wao na siasa ni kama moto na petrol na watoe 'press release' kwamba yeyote atakayejaribu kulitumia baraza hilo apuuzwe na asihusishwe na uislamu. Hii ndio dawa ya magenge kama haya hasa kipindi hiki cha kuelekea 2010 ambacho warafi wengi wasio na ushawishi watajaribu kutumia njia yoyote kutafuta uhalali kwa wananchi.
 
Yaani katika watu ambao nafikiri thinking capacity ni ndogo basi wenztu waislam wanaongoza. Wanapenda sana kudeal na minors, wakati mambo makubwa wanayaona na wanapita hawasemi.

Na TZ tutaregret soon, kwa kuruhusu ujinga na upuuzi kama huu kwa watu wajinga wachache. Enzi hizo walikwua wakikusanyika wanapigwa mabomu ya machozi hawafikii hata kuogea, huyu handsome boy kaja na mambo yake ya kuwapa uhuru wa kuongea randomly wanaanza kuongea yasiyowahusu.

Jamani tusiruhusu haya mambo yatatutokea puani soon.
 
CUF at work , baada ya yale ya Mbeya sasa wamehamia kwenye makongamano.Hapa tuna amini kwamba Chadema ni wapinzani wa kweli na CUF wamekuwa wakitumika .Ushahidi tosha kabisa .Watanzania si wajinga na wataendelea na kuunga mkono Chadema.Hivi hili Mzee Jasusi Kongamano lilikuwa kwa ajili ya Chadema pekee ama maendeleo ya Waislam na maslahi katika vyama vya siasa ? Nimeshindwa kuelewa ama kwa vile sijasoma habari nzima maana nimepata kicgefu chefu kabla sijaenda mbali ?

Kwa nini usiseme CCM, NCCR au TLP at work?. Wewe unaonesha kuwa ni mdini kupita kiasi na umeshalishwa mdudu na CCM wa kuamini kuwa CUF ni wadini, CHADEMA ni wakabila hatutofika kwa style hii.
 
INGAWA madai ya wasomi wa Kiislamu ni kwamba CHADEMA inatawaliwa na Wachagga na watu wa kaskazini, ukweli ni kuwa kuna mengi mengine yasiyosemwa yanayowakera Waislamu.

Katika waraka wa siri unaozagaa miongoni mwa Waislamu (ambao pengine umepandikizwa na vyama vingine) ni kuwa viongozi wa CHADEMA wamekubaliana na viongozi wa Kikiristo nchini kuhakikisha kwamba nchi hii haiwi mwanachama wa IOC na wala Waislamu hawapewi mahakama ya Kadhi milele.

Na kwamba baadhi ya viongozi wa makanisa wamesema watawashawishi waumini wao kukichagua CHADEMA 2010!

Hili la viongozi kuwa ni watu wa Kaskazini tu ni kiini macho cha yale ambayo Waislamu wameshindwa kuyasema hadharani. Je, hivi kama mtu mwenye wa kuongoza ni Mchagga au Mbulu au Mmasai basi Wazaramo na Wanyaramba wasijiunge na chama hicho. HIli linaleta kweli?

Chadema wanapaswa kuwa makini sana hapa maana inaelekea kama vile kuna mkono wa mtu hapa.

Ni dhahiri kwamba CCM ina miezi michache tu ya kufanya uamuzi wa aidha kuwabeba au kuwatelekeza waislamu katika madai yao mbalimbali.

Hilo linaelekea linaweza likashindikana na hivyo chama tawala pengine kinahangaika kwa hivi sasa kuhakikisha kuwa kinawachafulia wengine kura zao kwa kuonesha kuwa nao pia hawana lolote watakachowafanyia waislamu pindi wakiingia madarakani.
Ingawa yapo madai kuwa vyama fulani na viongozi wao wanasema waziwazi kwamba nchi haiwezi kuongozwa na mtu yeyote kutoka makabila makubwa au tajiri hapa nchini kama vile Wahaya, Wasukuma, Wachagga, Wanyakyusa au watu wakorofi kama Wakurya na Wamasai!

Kwa Watanzania huu ni mtihani mkubwa sana. Maana kama tumeanza kutumia dini kukubali au kukataa kiongozi au chama fulani basi ni dhahiri kuwa kwa necha ya binadamu kila mtu ataanza kuvutia ngozi upande wake.

Iwe chama tawala au vile mbadala wajue kwa kuitumia dini kisiasa mambo yatakuja hatimaye kuwageukia wenyewe. Huko huko ndani ya CCM watu wataanza kupigiana kura kutokana na dini ya mtu. Na hapo kitakachofuata wote........ tunakijua isipokuwa kuna wengi hawataki kukubali ukweli wake.... na madhara yake makubwa kwa vizazi vijavyo hapa nchini.
 
Believe me, kama CCM haitavikemea vikundi hivi vya kiislamu kwa uwazi itapoteza kura za Wakristo. Tusipo acha kuingiza siasa kwenye dini, amani itapotea.
Mkuu, nadhani mhusika hapa ni Baraza la Waislamu kutoa ELIMU kwa waandishi wa habari kutochanganya habari ya mtu binafsi na tamko la Baraza au Uislamu kwa ujumla!

Elimu yenyewe wala haiitaji kuwaweka waandishi darasani bali kutoa "official Press Statement" kukemea watu hawa na kuelekeza vyombo vya habari kupuuza 'statement' za namna hii. Baraza likiendelea kukaa kimya basi watu wengi wataitumia njia hii kutafuta ushawishi maana katika kipindi hiki wengi watahusisha imani ya kiongozi wa nchi na matukio mbalimbali ili kuteka wananchi (kumbuka si Watanzania wote wana elimu ya kutofautisha pumba na mchele).
 
Katika waraka wa siri unaozagaa miongoni mwa Waislamu (ambao pengine umepandikizwa na vyama vingine) ni kuwa viongozi wa CHADEMA wamekubaliana na viongozi wa Kikiristo nchini kuhakikisha kwamba nchi hii haiwi mwanachama wa IOC na wala Waislamu hawapewi mahakama ya Kadhi milele.

Na kwamba baadhi ya viongozi wa makanisa wamesema watawashawishi waumini wao kukichagua CHADEMA 2010!


Mkuu Iga, unao huu waraka wa siri?
 
Jamani jamani, tuweke uTZ mbele. hawa watu wengine ni wa kupuuza tu. Kuna wakristo na waislamu wenye udini lakini hautakiwi kuingia katika siasa kabisa. watu kama hawa ni wa kukimbiwa, tusiangalie alisema/aliyefanya kitu ni wa dini gani tuangalie ni kitu gani na manufaa yake.

Tuache kushabikia dini jamani hatutafika na inatakiwa kila mtu aisaidie jamii kuepukana na mambo yaya. Dini zina nafasi yake misikitini na makanisani. tatizo ni kwamba viongozi wanakuwa na dini zao, sisi kama wananchi tusiangalie hilo bali tuangalie uwajibikaji wao kwetu.

Tunapoteza ladha ya Taifa
 
Yaani katika watu ambao nafikiri thinking capacity ni ndogo basi wenztu waislam wanaongoza. Wanapenda sana kudeal na minors, wakati mambo makubwa wanayaona na wanapita hawasemi.

Na TZ tutaregret soon, kwa kuruhusu ujinga na upuuzi kama huu kwa watu wajinga wachache. Enzi hizo walikwua wakikusanyika wanapigwa mabomu ya machozi hawafikii hata kuogea, huyu handsome boy kaja na mambo yake ya kuwapa uhuru wa kuongea randomly wanaanza kuongea yasiyowahusu.

Jamani tusiruhusu haya mambo yatatutokea puani soon.

Hauwatendei haki waislamu. Mwaipopo hajawahi kuwa msemaji wa waislamu wote kama vile Mchungaji Mtikila asivyo msemaji wa wakristu wote. Hii tabia yetu sisi wamisheni ya kuwahukumu waislamu wote kutokana na matendo ya wachache wao ndiyo inayoweza kutufikisha pabaya! Mbona kuna ma-lumpen kibao ambao ni wamisheni?

Vile vile ni hatari zaidi kuzuia watu kama wakina Mwaipopo kuzungumza. Kwa kufanya hivyo yutawa-legitimise kuwa maneno yao yana ukweli ndiyo maana tunamzuia. Tumwachie aseme ila tusichelee kumpinga na kumwonyesha jinsi alivyo mcha kweupe! Kwangu mimi Freedom of speech ni sacrosant na haistahili kubwana kutokana na maneno ya wapuuzi wachache.

Amandla..........
 
Baada ya Rostam kumwaga vijisenti kanisani Lutheran, iliandikwa humu JF na paparazi muwazi kuwa next ilikuwa kuwakamata baadhi ya viongozi wa kiislam. Huyu paparazi taarifa zake nyingi zimekuwa za uhakika hivyo nitashangaa kama chadema hawakulitegemea hili. Matarajio yangu ni kuwa watavuka salama kama walivyoweza kuvuka vikwazo vingine wanavyokumbana navyo toka kwa hawa mafisadi.
 
Ni lazima chadema watambue kwamba wapo katika vita ambapo maadui wao wananguvu. Nguvu za pesa na ushawishi pia.Wanaposhindwa kutumia sera kama njia ya ushindani ndipo tunawaona wanaingiza maswala ya udini na ukabila.kama hatutakemea huu uhuni wa aina hii ni dhahiri tutaweza kuligawanya taifa na yale yaliyokuwa yanasifika kwa nchi yetu yatatoweka kabisa. Ieleweke kwamba hama tawala wanaweza kitumia mbinu yoyote hatakama kukuvua nguo hadaharani ili washinde( Maana agenda yao namba moja ni kushinda kila chaguzi),Nategemea chadema wanatambua namna ya kucheza mchezo huu. Wasibweteke maana inawezekana kufa kwao kukawa rahisi zaidi.Wajipange vema,wapo katika nafasi ya kiushinda na HATIMAE HAKI ITASIMAMA TANZANIA
 
Back
Top Bottom