Juhudi za CHADEMA kuwasemea watanzania na kuwasaidia kujielewa na kuelewa hali zao zinaonekana kuzaa matunda. Ukweli ni kwamba watanzania wengi wanahitaji mtu anayeelewa mambo awafafanulie na kuwapa mwanga kwani kwa kawaida watawala hutumia mwanya wa watu kutoelewa mambo na kuwakandamiza wananchi.
Nimeona taratibu watu wanaanza kuwaelewa CHADEMA kuhusu umuhimu wa katiba mpya, demokrasia nzuri na uhuru wa kujieleza. Tangu CHADEMA waanze kuongoza maandamano ya wananchi nimeona wananchi wameanza kupata mwamko na kujiongeza katika uelewa wao wa mambo muhimu yanayowahusu. Mtaani kuna vuguvugu la kutaka mabadiliko na watu kwa kweli wameichoka CCM, inasubiriwa tu namna ya kuimalizia CCM ikate pumzi moja kwa moja.
Ushauri wangu kwa CHADEMA ni huu:
CHADEMA endeleeni kuwa sauti ya wanyonge. Msikatishwe tamaa na mtu, hata pale mnapoona upinzani wa serikali na wananchi kutowaelewa, msikate tamaa, endeleeni tu sio kwamba ni bure, hapana watu wanawaelewa zaidi kila siku.
Waelezeni wananchi ukweli kuwa hali ngumu ya maisha inatokana na uongozi mbovu chini ya CCM.
Zungumzieni sera mbadala. Zungumzieni matatizo ya umeme, sukari, gharama kubwa za matibabu na ugumu wa maisha unaotokana na uongozi mbovu wa CCM.
Watanzania tunawaelewa, kazeni buti tunawategemea kwa uhai wa taifa letu.
Hongera sana Mbowe, Mnyika na makamanda wengine wote!