Operation Jicho la Paka na dakika za Mwisho(with Wolf rules )

Riwaya:Oparation Jicho la paka

Sehemu ya kumi

Na Bahati Mwamba

Akaitazama fulana yake na hapo akili yake ikamwambia ya kuwa yaeza kuwa walipewa fulana feki za kuzuia risasi na kisha akajiwazia ya kuwa huo ulikuwa ni mchezo waliochezewa tangu wakiwa nyumbani Tanzania.

“kwanini wametufanyia hivi!!”akajiwazia Luteni kanali Mwinyi Kisoda huku akigeuka nyuma ili atoke ndani ya jengo lile,mara akasikia hatua za mtu zikinyata kusogelea jengo lile na yeye akawahi kuruka juu na kuipiga taa ikavunjika na pale ndani kukawa giza.

Akiwa amesimama kwa kutulia na huku akijaribu kusikiliza hatua za mtu aliehisi akiingia,macho yakapata kuona kitu kilichomstua.

Akiwa bado anatafakari kile alichokiona,mara mlangoni vikajaa vivuli vya watu wawili na moja kwa moja vivuli vile ambavyo kiuhalisia ni watu vikaanza kushambulia kwa kasi kuelekea pale walipohisi Komando Mwinyi Kisoda atakuwako ila kitu ambacho hawakujua ni kuwa tayari waliemlenga alikuwa yupo kona nyingine na amezikwepa risasi na haijampata hata moja.

Komando Mwinyi Kisoda alikuwa amesimama huku kisu chake kikiwa mkononi na kwa kasi ya ajabu akakirusha kuwaendea watu wale waliokuwa wanapiga risasi hovyo na kikatua kifuani kwa mmoja wapo na mwingine wakati anajaribu kurudi nyuma guu la Luteni Kanali Mwinyi Kisoda lilikuwa limeshatua kifuani kwake na kumtupa nyuma kwa nguvu kama gunia la viazi vitamu.

Mwinyi Kisoda hakuwa na muda wa kusubiri haraka akarudi pale alipoona kitu mfano wa kitaa kidogo kikaacho kwenye saa aina ya Ago.

Kifaa kile alipojaribu kukishika,akakutana na uso wa komando zaza.

“hii miwani ndio iliotuuza”akajisemea kwa uchungu baada ya kugundua kile ni kifaa kilichokuwa kinarusha mawasiliano sehemu flani kwa njia ya mawimbi.

Haraka na yeye akavua mawani yake na kuyatupa kisha akafanya haraka kutoka mle ndani huku akisikia sauti za mbwa kwa mbali na vishindo vya watu vikija kwa kasi eneo lile.

Mbio zake zilikuwa ni kuelekea usawa ambao alikubaliana na Luteni Haji Makame ashushe chopa na lengo lake la kwenda huko ilikuwa ni kuhakikisha kama na Luteni nae ameuwawa ama la na kama alivyopata taarifa ya kuwa chopa imepigwa bomu basi ahakikishe kisha ajue atacheza vipi peke yake ili ajinasue katikati ya waasi wa kundi la LRA .
*****

Dakika kumi badae alikua amesimama huku akishuhudia namna chopa yao ilivyokuwa imeharibiwa kwa bomu.

Akapiga hatua kwa umakini ili aweze kufika karibu zaidi na kilichokuwa kinampeleka pale ni kutafuta kiboksi cheusi ambacho huwa ni muhimu sana kwa uharibifu ama kwa ajali ya usafiri wa anga.

“wako makini sana na wanajua wanachokifanya”alijisemea baada ya kukikosa na hiyo ilithibitisha ya kuwa tayari kimeondolewa pale.

Wazo pekee ililokuwa limesalia kichwani mwake ni wapi ulipo mwili wa Luteni Haji Makame,mana kwa vile yeye ndie alietoa taarifa ya kushambuliwa kwa chopa hiyo ilimaanisha hakuwa ndani ya chopa.

Ni kama akili yake ilihisi kitu na haraka akageuka na ndivyo ilikuwa alichokihisi kuwapo nyuma yake kilikuwapo .

Alishuhudia jibwa kubwa lenye kimo cha ndama likiwa limesimama kimya likimtizama katika mkao wa kushambulia.

“spy dog”akajisemea baada ya kuona aina ya mbwa ambao huwa wamefundishwa kufuatilia nyayo za adui kimya kimya bila kupiga kelele na wakimpata hushambulia kwa kutoa mlio flani ambao hutoa taarifa kwa wahusika.

Luteni Kanali Mwinyi Kisoda alianza kupiga hesabu namna ya kumtoka mbwa yule.

Akajitikisa kidogo kwa lengo la kumhadaa mbwa yule nae mbwa akahadaika kwa kuruka ili amdake lakini hakujua hila aliopangiwa.

Komando Mwinyi Kisoda akainama kidogo kisha akatumia kisu chake kutoa shambulio la kustukiza lililoenda kutua shingoni mwa mbwa yule na mbwa yule bila kutoa kelele akaanguka chini kimya kimya na hakuwa walau na neno la mwisho kwa Luteni Kanali aliekuwa ameshachomoa kisu chake na kukitia kwenye ala.

Wakati anataka kutoka eneo lile mara akahisi kitu cha baridi kimepenya kwenye paja la mguu wake wa kulia,hakutaka kujiululiza mara mbili ya kuwa tayari alikuwa ameshambuliwa kwa risasi na mdunguaji.

Kwa kasi akaruka juu kisha akiwa juu akajigeuza kwa kasi na kutaka kujirusha kwa mtindo maarufu kwa makomando wakati wakitaka kujiokoa kwa haraka lakini ni kama alikuwa anajitekenya peke yake kabla azima yake haijatimia akapigwa risasi ya bega na kumfanya aende chini kama mzigo ambao haujafungwa vyema.

Mwinyi Kisoda hakutaka kukamatwa na waasi wale hivyo kwa kutumia mkono wa kulia akachomoa bomu dogo la kurusha kwa mkono alilokuwa amelisunda mfukoni,wakati akitaka kutoa safety pini risasi ya mdunguaji makini ikampiga katikati ya kiganja cha mkono hivyo kufanya azima yake isitimie na akabaki chini akigagaa kwa tabu.

Kundi kubwa la waasi likamzingira huku silaha zao zikiwa tayari kufanya kazi yake endapo angelitaka kuleta ujanja wa aina yoyote.

Komando alikuwa mikononi mwa waasi.

Itaendelea

Leo fupi mtanisamehe
 
Na imekuwa fupi kweli ila Shukran sana mkuu!!
 
shukrani sana
 
Sipo njema kiafya nina wiki ya tatu sasa ila nikikaa vyema tutaendelea usiwe na shaka
Pole sana mkuu!
Ni maombi yangu utapona na utarudi katika hali ya kawaida na utaendelea na majukumu yako kama kawaida!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom