Sehemu ya kumi na tatu
Wakati wanaanza kuikamata barabara ya uzalendo,ndipo dereva wa gari lililokuwa limetangulia alipoona kuna pikipiki inakuja kwa kasi upande wao huku kukiwa na mtu alievalia mavazi ya kijeshi bila kofia ngumu kichwani.
Mtu yule alizidi kikaribia gari lile na alipofikia karibu kwa wepesi wa aina yake akaipisha kidogo ile gari,na niyeye tu aliejua aliekifanya kwenye gari lile na kwa kuwa alikuwa kasi haikuchukua walau sekunde akalipita gari la pili na kwenda kufanya kile alichokifanya kwenye gari la kwanza na kisha akaruka juu na kutua chini kwa mtindo wa aina yake na hakuumia hata kidogo na aliiacha pikipiki yake ikienda kugonga magari mengine yaliokuwa nyuma kisha yeye akaepa na kutua upande wa pili wa barabara na haikupoita hata dakika moja gari la kwanza na la tatu yakalipuka kwa kishindo na dereva wa gari la pili akayumba kukwepesha gari lake na akajikuta anagonga kingo ya barabara na gari likapaa na kuanguka huku tairi zikiwa juu zinazunguka.
Dereva wa pikipiki hakutaka watu ama polisi wamkute pale,haraka akachomoa bastola yake na kukimbia kwa kasi ya na kulifikia gari lile na akaenda upande wa dereva akaachia risasi mbili zikatua kichwani kwa dereva na kumwacha maiti kisha akapita upande wa pili akakutana na mtu akijaribu kutoka ndani ya gari lile nae akamchapa risasi ya mgongo kisha akinama na kuchomoa funguo kutoka kwa mtu yule ambae alimpiga risasi na haraka akapita upande wa nyuma na akapiga risasi moja ilioenda kuvunja kufuli na kufungua mlango,risasi zake tatu zikaenda na uhai wa watu ambao hakuwahitaji na aliwakuta huko nyuma wakiwa wamweka mtu aliemhitaji katikati yao.
Alipohakikisha kaua wote akamsaidia kutoka mtu aliemhitaji kisha akamfungua na pingu za miguu na mikono na alipotaka kumkokota watoke,kagundua mwenzie hana nguvu kabisa,akachomeka bastola yake kiunoni na akamweka begani kisha akakimbia nae kuelekea barabarani na punde ikaja range nyeusi ikasimama na haraka akashuka mwanamke aliekuwa amevaa mavazi ya jeshi la Uganda na akamsaidia kufungua milango na kumwingiza waliemwokoa kisha yule mwanamke akaukamata usukani na kuondoa gari kwa kasi sana huku nyuma wakiacha kelele za magari ya polisi na zimamoto yakifika pale.
****
Unajisikiaje kamanda”aliuliza mtu aliekuwa amekaa karibu na Mwinyi Kisoda.
“Haji nipo hovyo sana,na wamenitesa sana wajinga hawa”alijibu Mwinyi.
Gari walilokuwamo likaenda kuegesha kwenye maegesho ndani ya nyumba ya kawaida iliokuwa imezungushiwa ukuta.
Mwanamke aliekuwa dereva,akawa wa kwanza kushuka na kuja kuwafungulia mlango na akatoka Luteni Haji Makame,na kisha akafuatia Luteni Kanali Mwinyi Kisoda.
Licha ya kuonekana hana nguvu sana,lakini alikataa kusaidiwa kutembea na akatembea mwenyewe kwa tabu na akaingia ndani na yule mwanamke akamwomba aongoze moja kwa moja hadi kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa na vifaa tiba na alipofika huko Luteni Haji na yule mwanamke wakaanza kumpa tiba kwenye majeraha mbali mbali mwilini.
“Huyu mwanamke ni nani Haji”aliuliza Mwinyi.
Haji na yule mwanamke wakaangaliana kisha Haji akajibu.
“Afisa wa Jeshi la Uganda anaitwa Cathy ni tabibu kambi ya Enungu,tulikutana miaka kadhaa nyuma huko Sudani”
“ok sawa ndo mana mmeanza kufanana sasa”akatania Mwinyi na kufanya wote waangue kicheko pale ndani.
Baada ya saa tatu kupita tayari Mwinyi Kisoda alianza kurudiwa na nguvu zake na akanyanyuka na kwenda kukaa sebuleni ambako aliwakuta Haji na Cathy wakitizama runinga.
“Vipi kamanda ungelipumzika kwanza…”alisema Haji Makame baada ya kumuona Mwinyi akikaa kwenye sofa.
“mapumziko yanatosha Haji ngoja niungane nanyi hapa mana naona nikilala nitamuota yule mshenzi Nkunda”alijibu huku akitoa sonyo la hasira.
“Yule kafanya kazi yake,tatizo lipo tulikotoka Kamanda na si mimi ama wewe aliegundua hilo”alisema Haji Makame.
“Kwani wewe uliwezaje kutoka kule”aliuliza Mwinyi.
“wakati nikiwa nimeshusha Chopa, nikawa nimetulia nikisubiri amri yako,hapo ndipo nikaamua kutazama kushoto kwangu na nikakutana na mawani moja ikiwa kmesalia mle na nilipoishika nikakutana na chip ndogo na hapo nikajua kuna kitu hakipo sawa nikashuka nayo chini ili niiharibu lakini wakati nafika chini tu nikakutana na watu watatu,sikutaka kuwa mzembe nikapambana na kukimbia,sikufika mbali nikaona chopa ikiwaka moto ndipo nikakutaarifu kisha mikavua bulg na kuzitupa mana sikuziamini tena,na nikaanza kuja uelekeo mliokuwako na nilifika hadi kwenye yale majengo mawili na huko nikafanikiwa kukuona ukifukuzwa na waleywapiganaji,nikataka kukusaidia ila ukawakimbia na ukarudi nilikotoka nami nikarudi na nikafanikiwa kuona ukitekwa nami nikafanya jitihada nikateka mmoja ndie akanambia wanakuleta entebe kwenye nyumba zao,nikachomoka na kuja hadi huku nikampata Cathy na tukafanikiwa kukuokoa”alimaliza kusema Haji Makame.
Luteni Kanali Mwinyi Kisoda akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akasema.
“sasa tunarudije nyumbani mana kuendelea kukaa hapa nikujirudisha tena mikononi mwa LRA ambao naamini hadi sasa wanatutafuta”
“ni kweli na hakuna njia nyingine,lazima twende ubalozi kama raia wema tu kisha tutarudishwa nyumbani na huko tutajua cha kufanya ila mimi sintorudi jeshini tena”alisema Haji Makame huku akimwomba Cathy awapishe wazungumze faragha wao wawili.
Baada ya Kubaki wenyewe Mwinyi akasema
“afu wale wajinga walikuwa wanaulizia nyaraka namba 08 ya 97,sijui wajua lolote”
Haji Makame akakaa kimya kisha akajibu
“wakati nipo kitengo niliwahi kuiona na niliihifadhi mimi chini ya usimamizi wa Kanali Zwange ila nyaraka ile ni janga kama ikiwafikia watu”
“basi inapaswa tutoke hapa Uganda,mwite Cathy atupeleke ubalozi sasa hivi”akasema Mwinyi huku akisimama na kwenda maliwatoni kubadilisha mavazi nae Haji alifanya hivyo.
Dakika kumi baadae walikuwa nje ya uzio wa nyumba ya Cathy wakielekea Kampala huku wote wakiwa kimya kabisa.
***
Bada ya mwendo wa saa mbili na nusu hivi,tayari walikuwa wanaingia Kampala na ndipo Mwinyi akauvunja ukimya.
“Luteni,naona tusiende pamoja wewe baki huku utakuja kwa njia zako,wacha mimi nitangulie,mana kama tulisetiwa nyumbani,hadi sasa wananijua mimi si wewe hivyo baki hapa Uganda”
“Umenena vyema kamanda”kwa mara ya kwanza Cathy aliingilia maongezi yao kisha akaendelea.
“japo sijajua kwa kina ilikuwaje,ila inavyoonekana ni mkondo mkubwa mnauingia hivyo kwenda pamoja ni kama kujimaliza wenyewe”alisema tena.
“hapana shaka we tangulia,mi nafanya niwezalo kesho ama leo hii nitafika Tanzania”alisema Haji Makame.
“ukifika nenda nyumbani kwangu,ukikuta geti limefungwa kwa kufuli jipya ujue nipo na usalama upo ila ukikuta kufuli la kale,jua kabisa sipo na sipo salama,fanya jitihada za kunitafuta”alisema Mwinyi kisoda huku akionekana dhahiri kuingiwa na woga moyoni mwake.
• * *
Gari yao ilisimama hatua kadhaa kutoka kwenye lango la kuingilia ubalozini na Mwinyi Kisoda akashuka kisha lile gari likaondoka kwa kasi kurudi lilikotoka.
Luteni kanali Mwinyi Kisoda akapiga hatua hadi mapokezi,akaeleza shida yake kisha akapelekwa kwenye ofisi ya kushugulikia dharura na huko akakaribishwa na kijana nadhifu,ambae hakuwa mnene wala mwembaba na hakuwa mrefu wala mfupi ila alikuwa na urefu wa kawaida sana na kwa haraka Mwinyi akatupia jicho mezani kwake na akaliona jina Habibu B Anga,kibao kilisoma hivyo.
Habibu akaomba atoke nje na atarudi kumsikiliza alikaa huko nje kwa dakika kama tano kisha akarudi na kuendelea kumsikiliza mgeni wake,kisha akamwambia atamsaidia mana kuna ndege inaenda dar jioni hiyo.
****
Baada ya nusu saa Luteni kanali alikuwa juu ya anga,wakielekea dar es laam kwa ndege ya shirika la Afya duniani.
Tofauti na alivyotegemea ndege ile kutua JNIA,yenyewe ikaenda kutua uwanja wa Karume Zanzibar na kisha wakaja wanajeshi kama kumi hivi wakamweka chini ya ulinzi na kutoka nae na kuelekea asikokujua.
Nb:nunua moja upate moja bure kwa Tsh 3000/= wasiliana nami 0758573660