Operation Jicho la Paka na dakika za Mwisho(with Wolf rules )

Riwaya:Operesheni Jicho la Paka
Sehemu ya kumi na moja

Mwinyi Kisoda hakutaka kukamatwa na waasi wale hivyo kwa kutumia mkono wa kulia akachomoa bomu dogo la kurusha kwa mkono alilokuwa amelisunda mfukoni,wakati akitaka kutoa safety pini risasi ya mdunguaji makini ikampiga katikati ya kiganja cha mkono hivyo kufanya azima yake isitimie na akabaki chini akigagaa kwa tabu.

Kundi kubwa la waasi likamzingira huku silaha zao zikiwa tayari kufanya kazi yake endapo angelitaka kuleta ujanja wa aina yoyote.

Komando alikuwa mikononi mwa waasi.

*****
Baada ya dakika kumi mlango wa CDF ukasukumwa na akaingia mtu mwenye umri wa kustaafu yani yapata miaka hamsini na mbili hivi, lakini mwili wake ulikuwa unamwonekano wa chini ya umri huo.

Mtu yule akapiga saluti kwa mkuu wake wa kazi ambae alikuwa ni mkuu wa majeshi Jeneral Tasi kinoga.

Baada ya salamu hizo za nidhamu jeshini,ukapita ukimya kidogo kisha Jeneral akauvunja kwa swali.

“Kanali, Classified document unazo?!”

Kanali akatazama chini kidogo kisha akasema

“ya mwaka gani mkuu!!”

Jeneral akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akasema

“kikosi chako kilikuwa kinashugulikia ya mwaka gani na ipi tuliokubaliana isitoke?”

Kanali akawaza kidogo kisha akasema

“1997 ndio hadi sasa ni Classified na bado ipo mikononi mwangu”

“vijana wangapi wa Military Intelligence service wanajua usiri wa nyaraka hizo?!”akauliza Jeneral

“wanajua watu wawili tu! Waliokuwa chini ya MIS(military intelligence service)”akajibu Kanali

“wako wapi vijana hao”aliuliza Jeneral

“Baada ya kunikabidhi nyaraka hizo mmoja nikampeleka Sudani na Mwingine nikampeleka kikosi cha anga Zanzibar”akajibu kanali.

“unawaamini hao vijana?!”akasema Jeneral.

“Naweza kusema hivyo japo naamini binadamu aweza badilika japo sina hakika kama mabadiliko hayo yatakuwa kwao!”akajibu kanali.

“Sasa inabidi uelewe ya kuwa nyaraka hiyo kuna watu wanahitaji kuipata ili mambo yao yakae sawa,unaeza usione tofauti sasa ila wakiipata hata leo,tutaishi katika tabu kubwa sana”akanyamaza kidogo Jeneral kisha akamtazama Kanali Zwange kama anamsikiliza na aliporidhika na umakini aliopewa na Kanali akaendelea,

“Nyaraka hiyo hata rais hajui ilipo na inamuumiza kichwa hasa baada ya leo Meja jeneral Kambi kibeyo kujiua kule visiwani mana ndie alikuwa mkombozi endapo mambo yangeliharibika”akanyamaza tena kisha akajikuna kidevu chake kilichokuwa kimeotesha ndevui chache nyeupe.

“hakuna namna inabidi uitunze kama mboni yako na ukubali kufa kuliko kuitoa ilipo,najua ni mimi na wewe tunaojua ilipo lakini inabidi uijue wewe peke yako Kanali kuanzia sasa”akasema huku akinyanyuka na kumsogelea karibu zaidi Kanali Zwange aliekuwa amesimama muda wote wa maongezi yao.

Kanali akazidi kushangaa kauli ile ya kamanda wake.

“hakuna namna tunaweza kufanya zaidi ya wewe kuomba kustaafu kisha utokomee na nyaraka hiyo”Jeneral alisema kwa sauti ndogo lakini ilijaa vyema kwenye ngome za masikio ya Kanali Zwange.

“lakini Jeneral kati yangu mimi kustafu na waziri Makoye kutenguliwa uwaziri kipi bora?”aliuliza Kanali.

Jeneral akavuta pumzi nyingi kisha akazishusha kwa wakati mmoja na kisha akasema.

“hakuna namna bora ya kuweza kutengua uteuzi wake na hilo rais amelikataa wakati nikiwa nae ahsubuh ya leo na alisema ni hatari sana kwa kumtoa pale alipo maana akiwa nje ndio huweza kufanya mengi tofauti na sasa ambapo anaweza kufanya taratibu sana”alifafanua kwa kirefu Jeneral.

“kwa hiyo natakiwa kufanya nini Jeneral”aliuliza kanali Zwange.

“inabidi ustafu na usiwepo kabisa katika mfumo wowote wa ndani ya nchi hii,namanisha tutafuta kila kitu kinachokuhusu na kisha tutaweka mtu mwingine mwenye jina sawa na wewe na mtu huyo ndie atakuwa kanali mpya na ataendelea kuongoza MIS na tayari nishampa taarifa”alisema Jeneral huku akichukua faili moja kubwa na kuliweka juu ya meza.

“stahiki zako zote nimeziweka humo nenda kayaanze maisha mapya na hakikisha hata mimi sijui ulipo ili iwe salama zaidi huko uendako na njia ya kuwasiliana na wewe nadhani unaijua!”

*****

Kanali Zwange baada ya kutoka ofisini kwa CDF moja kwa moja alielekea kwenye ofisi zake na huko akakuta vijana wa military Intelligence wakiendelea na majukumu yao bila wasiwasi,hakuwajali akawapita na kuelekea kwenye ofisi yake na huko hakukaa sana akatoka akiwa amebeba mkoba wake na kupanda gari kisha akatokomea kuelekea mjini na huko akaelekea zilipo ofisi za Bank moja kubwa na akakaa kwa muda wa nusu saa na alipotoka hakuwa na mkoba wake na alikuwa mikono mitupu na akapanda gari kisha akaelekea Mwenge yalipo makazi yake na uzuri ni kuwa hakuwa akiishi na mwanamke,na hii ni baada ya kuwa ametalakiana na mkewe ambae alikuwa na uraia wa chini Nigeria hivyo kufanya familia yake iwe huko na yeye akabaki peke yake na kuwa na michepuko tu huku akili yake akiwa ameiweka zaidi kwenye kazi yake.

“walifanya makosa sana kwenye mkataba ule,ona sasa wanaishi kama wakimbizi dah…”alijiwazia Kanali huku akiweka vitu vyake sawa na kupangua hiki na kile na alipokamilisha alichokihitaji akaamua kuondoka ndani ya nyumba ile bila kufunga maana alijua kuna mtu kama yeye atakuja kuishi nyumba ile na yeye akaamua kufunga safari kwenda anakokujua.

****

Vipigo mfululizo vilikuwa vimemdhoofisha Luteni kanali Mwinyi Kisoda na hadi wakati huo majeraha yake ya risasi alizopigwa hayakuwa walau yamefanyiwa utaratibu wa aina yoyote.

Mbali ya kuwa dhoofu lakini macho yake bado yalikuwa imara kumtazama mtu wa umri wake akiwa amesimama mbele yake huku akiwa amevaa mawani ya kumziba macho hivyo kufanya wanaetazamana asijue kama anatazamwa yeye.

Mtu yule akaletewa kiti na mtu mwingine aliekuwa ameziba sura yake mfano wa wale wapiganaji wa kikundi cha Alshabab.

“Mangazeni Nkunda huwa siingiliki kirahisi hivyo Luteni Kanali!!”alisema mtu yule aliejiita Mangazeni Nkunda na ndie alikuwa mkuu wa kikosi cha wapiganaji wa LRA.

“Africa hakuna kisiwa cha amani kama mnavyojinasibu huko Tanzania,ona sasa mmeanza kulana wenyewe kwa wenyewe”alisema Mangazeni Nkunda kisha akaendelea

“ngozi nyeusi tumeumbwa na tamaa ya kila kitu na ndio mana tinatumiwa na watu weupe kujiua wenyewe na ndivyo ilivyo..”akanyamaza kidogo kisha akaendelea

“….Maisha yangu nataka pesa tu na ili niendelee kuzipata nimepewa jukumu moja tu kuhakikisha unanambia ni wapi zilipo classified document!”

Swali lile likamfanya luteni kanali Mwinyi Kisoda atumbue macho Kama mwizi wa maziwa kwenye susu .

Alitumbua macho kwa sababu hakuwa akijua lolote kuhusu nyaraka alizosihitaji kiongozi yule wa waasi na pia ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia kuhusu nyaraka za siri kuhitajika.

“najua unajua ya kuwa siko kwenye kitengo cha Military intelligence na wala siko Usalama wa Taifa,mimi niulize mission ngapi nimefanikisha ama nimefeli nitakujibu utakavyo”alisema Luteni kanali Mwinyi Kisoda.

Mangazeni Nkunda alicheka kwa jibu lile kisha akasimama na kupiga Makofi ya kumpongeza Luteni kanali,japo makofi yale yalitafsiriwa kama ni dharau na Luteni kanali mwenyewe.

“Luteni kanali Mwinyi Kisoda nimeyapenda majibu yako ila ukweli ni kuwa hata nikikuuliza yanayokuhusu utakataa kunijibu,na kwa kuwa Luteni Haji Makame hajapatikana na ni rafiki yako basi lazima aliwahi kukudokeza zilipo classified information about the 1997 mission”

Habari hiyo ilimsisimua Mwinyi Kisoda na ilikua ni ngeni ila alifarijika kusikia ya kuwa Haji bado yupo mzima,lakini alishindwa kuelewa kwanini yeye ahusishwe na nyaraka hizo ambazo zinaonekana ni muhimu sana japo hakuwa akizijua mwanzo.

“kiukweli habari hizi nazisikia kwako leo”alisema kiunyonge Mwinyi Kisoda.

“naona natumia diplomasia sana ndugu na hivyo kukufanya inijibu utakavyo”akasema Mangazeni Nkunda huku akivua koti la baridi na kumkabidhi mfuasi wake mmoja na kisha akachukua fimbo ndogo mfano wa mpini wa moko na bila kujiuliza akaanza kumshambulia nayo Luteni kanali sehemu mbalimbali za Mwili wake na alipositisha kupiga tayari Mwinyi kisoda alikuwa amepasuka hapa na pale na kufanya avuje damu mwili mzima huku akitweta kwa maumivu.

“nakuuliza tena ziko wapi ama uliambiwa nini na Luteni Haji Makame ambae ni rafiki yako?!”safari hii alizungumza huku akivua fulana yake na kuitupa chini

Luteni kanali Mwinyi kisoda hakuwa na cha kujibu na hata angelikuwa nacho bado asingeliweza kutoa jibu.

Kukaa kimya kwa Mwinyi kisoda kukazidi kumpandisha gadhabu Mangazeni nkunda na akaamua kuagiza zana za kazi ambazo zingelimsaidia kumbana Komando yule ili aseme ukweli.

“makomando kama nyinyi huwa tunadawa yenu ya mateso yalioboreshwa na utautapika ukweli”akasema Mangazeni huku akipokea kitorori kidogo kilichokuwa na vifaa mbali mbali na akachagua kitaulo kidogo na kwenda nacho hadi karibu na alipofungwa Luteni kanali Mwinyi kisoda na kisha akamziba nacho usoni na ili kumnyima hewa kisha mtu mwingine akaja na kuanza kumwaga maji juu yake na hivyo kumfanya Luteni Kanali Mwinyi Kisoda atapetape kwa kukosa hewa.

Zoezi lile lilidumu kwa zaidi ya nusu saa kwa kujirudia rudia lakini hakuna alichokisema Mwinyi kisoda kwa kiongozi yule wa waasi.

Mangazeni Nkunda akaamua kubadili mbinu ya kumwadhibu Mwinyi,akachukua waya mfupi wenye unene sawa na mdenge wa tairi ya baiskeli aina ya sport na ulikuwa umewekwa ndani ya moto hivyo kuufanya uwe mwekundu kutazama.

Akautazama kwa madaha kisha akamsogelea Luteni kanali Mwinyi na bila huruma akaudidimiza upande wa kulia wa kifua kipana cha komando Mwinyi kisoda.

Komando Mwinyi kisoda akapiga kelele za uchungu hasa alipohisi waya ule wa moto ukizama na kutoka kifuani kwake na kisha kurudishwa tena na Mangazeni aliposikia kilio cha Mwinyi akazidisha ukatili kwa kuchezesha waya ule uliokuwa umezama kifuani mwa komando Mwinyi ..

Itaendelea

Nb:Nipo kimya kwa Muda Kidogo kwa sababu nasumbuliwa na maradhi yakifua,kifua kinabana na ninakosa pumzi ila sio Athma ama Tb,bado naedelea na tiba za matababibu kulingana na ushauri wao
Hivyo niwaombe muwe wavumilivu tu nami nipatapo nguvu nitaweka riwaya.

Ila wale ambao hawataweza kusubiri,tuwasiliane kwa namba hii 0758573660 na utalipia Tsh 3000/=

Ahsanteni
 
Ugua pole mkuu.
Na shukran kwa muendelezo.
 
mmh...jamani jamani ..kudo... wahi tiba ndugu yangu isije ikawa kinataka kubana kama kilivyombana Marehemu Ibra Washokera..... .... ohoooh...
 
Back
Top Bottom