Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 15,848
- 20,697
Labda nikuulize swali mkuu,umetumia njia zote za kiungwana ili mfanyibiashara alipe kodi na halipi,what do you do,a straight answer please.Tuelewe spirit ya Rais kuhusu kodi ni kuwa wigo wa kodi upanuliwe na wawe wabunifu. Lakini pia falsafa ya Rais ni kuwa ukusanyaji wa kodi ufanyike kwa weledi na ufasaha bila kubambakiza kodi na kuwanyanyasa wafanya biashara ambao baadhi wamekimbia nchi na kufanya uchumi kusinyaa. Hivyo, watu wasipotoshe nia njema ya Rais.
Kitendo cha kuchukua mali au fedha za mfamya biashara benki ni kinyume na lengo zuri la ongeza mtaji, ongeza biahara na ongeza kodi (OMOBOK) ILi kuleta maendeleo ya dhati.
Rais yuko sahihi walipa kodi wabadilishe "mindset" zao kuhusu kodi na biashara. Wafanya biashara ni partners wao. Wabadilishe mbinu km ambavyo ukaguzi wa mahesabu walipo kuja na njia mbinu mpya.
Watoke kwenye enforcement ya kuharasss(reactive) kwenda kwenye proactive. Hii ni pamoja na kuelemisha na kujenga mitizamo chanya na endelevu ya kulipa kodi kuliko sasa. Itafika mahala kodi za nguvu zitakwama kabisa zaidi ya kuendekeza kazi. Kamishna Mkuu wa TRA ana kazi kubwa ya kubadilisha mitizamo na mbinu za utendaji wa watu wake,mifumo ya ufuatiliaji na ushirikishwaji wa jamii badala ya kukaa ofisni na kucheza na makaratasi bila kuzingatia uhalisia wa biashara vinginevyo hakuna mwekezaji atayekuja. TRA msaidie mama acheni kutumia mbinu zilezile katka mazingira mapya.
Rais Hayati Mgafuli aliwahi pia kulionya hili la kunyanyasa wafanya biashara na kupelekea Kichere kamishna mkuu wa wakati ule kumwondoa madarakani.
Kuhusu kusemea hadhara masuala ya kodi badala ya vikao vya ndani, Rais hafundishwi namna ya kusema so fa masuala ya kisera na maelekezo hutolewa hadhara ili kuweka uwazi.
Kimsingi zingatieni maelekezo ya Rais vinginevyo tunahitaji -total transformation sekta ya kodi. Hata hivyo-Wito -wafanya biashara walipe kodi
Unajua,nilitegemea Rais asisitizie juu ya umuhimu wa wafanyibiashara kulipa kodi kama sheria inavyowataka kufanya.Then nilitegemea aseme kwamba kwa mfanyi biashara yeyote ambaye hatapenda kulipa kodi kwa hiari,sheria itachukua mkondo wake,kwa kuwa zipo sheria.
Mkuu huwezi kumbembeleza mfanyibiashara asiyetaka kulipa kodi kwa hiari.Ukimbembeleza hata lipa.Lazima sheria zimbane ili alipe.