Rais Samia na Dkt. Mwigulu Nchemba, hili wanalolifanya TRA huenda likaiangusha CCM 2025!

World light

JF-Expert Member
Aug 4, 2022
275
258
Ukinunua dai Risiti,
Ukiuza toa Risiti
.

"" "" "" "" "" "" "" "" "" "

TRA wamekuwa wakiwaibia wafanyakazi wa Tanzania kupitia pay as you earn [PAYE] hasa pale mfanyakazi anapopata mgogoro kazini na baadae kuumaliza mgogoro ule na mwajiri wake kisha kurejea kazini na mwajiri kwa mujibu wa Sheria kulazimika kumlipa mishahara yake yote iliyopita kwa mkupuo.

Wakati Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaingia madarakani aliikuta kodi [PAYE] ikiwa ni asilimia 12 na retention fee huko HESLB ikiwa ni asilimia 6 akaifuta kabisa hii rentetion fee huku akipunguza sana kodi hadi kufikia a single digit yaani asilimia 8 tu huku marejesho ya mwezi kwa wanufaika wa HESLB pia hakukaa kimya akiyashusha toka asilimia 15 mpaka asilimia 8 lengo ni kutaka kuwapa hawa wafanyakazi waajiriwa nafuu katika maisha yao ambayo bado ni magumu kulingana na hali ya dunia ilivyo kwa sasa.

TRA wanawatoza wafanyakazi waajirwa hawahawa kiasi cha asilimia 30 ya mishahara yao wanayopokea kwa pamoja | Mkupuo ikiwa ni baada ya kumaliza tofauti zao na waajiri wao baada ya kusimamishwa na kurejeshwa kazini, kwa lugha rahisi TRA hii inawatoza karibu maratatu zaidi ya kile alichosema Mhe Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe 01|05|2021.

Mhe Waziri Dkt Mwigulu Nchemba angalia hii kwa uharaka kwani ni kweli linaumiza sana watu wetu kwa aina ya Rais tuliyenae hili kamwe hawezi kulivumilia kwani ni yeye Kila siku anayetafuta nafuu ya maisha kwa watu wake wote anaowaongoza.

Tutafakari hili vizuri, Kweli mtu anayelipwa tupesa twake tena pengine Mwajiri wake kaamua kuachana nae ili vimsaidie kufungua kabishara ili ale na wanae kisha afe nyie mnagawana nae karibu nusu kwa nusu lazima tuwe na huruma hasa kwa hawa wanyonge tunaowaongoza.

Wasiwasi wangu ni, to Why nyie TRA mnataka kumfitinisha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na watu wake anaowaongoza kwa hekima na busara nyingi kiasi hiki!! Na Je, Rais anajua hili,Waziri wa Fedha anajua hili?

Angalia hii,

Mfano, Ikiwa mwalimu aliyekuwa na gross pay ya TZS 725,000 na Leo atalipwa malimbikizo ya mishahara yake ya miezi 10 sawa na Tsh. 7,250, 000/-.

Mfanyakazi huyu atalazimika kukatwa asilimia 30 kama PAYE sawa na Tsh. 2, 175, 000 badala ya ile aliyosema Mhe Rais ambayo ni asilimia 9/8 sawa na TZS 662, 500 tu kama malimbikizo yake ya kodi kwa miezi 10 ambayo hata hivyo hakuyasababisha yeye ila Mwajiri wake, why leo aadhibiwe yeye kwa kodi ya asilimia 30 na sio asilimia 8 aliyosema Mhe Rais tena hadharani?

Tarehe 01 | 05 | 2021 Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa Jijini Mbeya alitangaza kodi ya mshahara kwa mfanyakazi kwa Kila mwezi [PAYE] ni 8% tu, Sasa nyie TRA mmepata wapi ruhusa ya kukata mshahara wa mfanyakazi kwa 30% tofauti na maelekezo ya amiri jeshi mkuu?

Hata kama mshahara huu uko in lump-sum bado ni mshahara uleule unaotakiwa kukatwa kodi ya asilimia 8 tu kwa kuwa unabaki kuwa ni "Mshahara tu" bila kujali unalipwa kwa mwezi mmoja au kwa miezi mia kwa pamoja bado ni mshahara.

TRA kumbukeni Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alishasema yeye hataki pesa ya dhuluma kumbukeni kumtoza mtu kodi ya 30% badala ya 8% hizi ni pesa za dhuluma na zitainyima kura CCM 2025.

TRA rekebisheni maramoja huu ni wizi wa wazi kwa Wananchi kwani ni hasara kubwa kwa Chama kama usipochukuliwa kwa umakini unaostahili kwani tayari moto umewaka huko kwenye magroup ya Whatsapp na ndio Mimi tu kuwaleteeni taarifa hii Kizalendo.

Cc:
Waziri Mkuu wa JMT,
Naibu Waziri Mkuu,
Waziri wa Fedha,
Kamishna Mkuu wa TRA
 
Hii hapana warekebishe hata kama mtu analipwa kwa mkupuo bado ni mshahara ule ule hivyo kodi lazima iwe ileile ya 9% kwa kiasi kitakacholipwa.
 
Hii ni kweli nilikuwa na jamaa hapa Dar yeye alifukuzwa kazi katika taasisi moja hapa mjini baadae akaenda mahakamani akawashinda kisha akalipwa 200m ni kweli jamaa walikata kama 50M hivi za kodi
200M X 0.3 = 60m yes kodi sio 9% wamempiga zaidi ya 9% naona wanampiga VAT kwenye mshahara
 
Ukinunua dai Risiti,
Ukiuza toa Risiti
.

"" "" "" "" "" "" "" "" "" "
Why Tanzania Revenue Authority (TRA) kwa maksudi wanataka kuifitinisha Serikali hii makini ya awamu ya sita na Wananchi wake hasa hili kada la wafanyakazi waajiriwa wa Tanzania.

TRA wamekuwa wakiwaibia wafanyakazi wa Tanzania kupitia pay as you earn [PAYE] hasa pale mfanyakazi anapopata mgogoro kazini na baadae kuumaliza mgogoro ule na mwajiri wake kisha kurejea kazini na mwajiri kwa mujibu wa Sheria kulazimika kumlipa mishahara yake yote iliyopita kwa mkupuo.

Wakati Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaingia madarakani aliikuta kodi [PAYE] ikiwa ni asilimia 12 na retention fee huko HESLB ikiwa ni asilimia 6 akaifuta kabisa hii rentetion fee huku akipunguza sana kodi hadi kufikia a single digit yaani asilimia 9 tu huku marejesho ya mwezi kwa wanufaika wa HESLB pia hakukaa kimya akiyashusha toka asilimia 15 mpaka asilimia 9 lengo ni kutaka kuwapa hawa wafanyakazi waajiriwa nafuu katika maisha yao ambayo bado ni magumu kulingana na hali ya dunia ilivyo kwa sasa.

Jambo baya zaidi ni hili la TRA kuwatoza wafanyakazi waajirwa hawahawa kiasi cha asilimia 30 ya mishahara yao wanayopokea kwa pamoja | Mkupuo ikiwa ni baada ya kumaliza tofauti zao na waajiri wao baada ya kusimamishwa na kurejeshwa kazini, kwa lugha rahisi TRA hii inawatoza karibu maratatu zaidi ya kile alichosema Mhe Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe 01|05|2021.

Mhe Waziri Dkt Mwigulu Nchemba angalia hii kwa uharaka kwani ni kweli linaumiza sana watu wetu kwa aina ya Rais tuliyenae hili kamwe hawezi kulivumilia kwani ni yeye Kila siku anayetafuta nafuu ya maisha kwa watu wake wote anaowaongoza.

Tutafakari hili vizuri, Kweli mtu anayelipwa tupesa twake tena pengine Mwajiri wake kaamua kuachana nae ili vimsaidie kufungua kabishara ili ale na wanae kisha afe nyie mnagawana nae karibu nusu kwa nusu lazima tuwe na huruma hasa kwa hawa wanyonge tunaowaongoza.

Wasiwasi wangu ni, to Why nyie TRA mnataka kumfitinisha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na watu wake anaowaongoza kwa hekima na busara nyingi kiasi hiki!! Na Je, Rais anajua hili,Waziri wa Fedha anajua hili?

Angalia hii,

Mfano, Ikiwa mwalimu aliyekuwa na gross pay ya TZS 725,000 na Leo atalipwa malimbikizo ya mishahara yake ya miezi 10 sawa na Tsh. 7,250, 000/-.

Mfanyakazi huyu atalazimika kukatwa asilimia 30 kama PAYE sawa na Tsh. 2, 175, 000 badala ya ile aliyosema Mhe Rais ambayo ni asilimia 9 sawa na TZS 662, 500 tu kama malimbikizo yake ya kodi kwa miezi 10 ambayo hata hivyo hakuyasababisha yeye ila Mwajiri wake, why leo aadhibiwe yeye kwa kodi ya asilimia 30 na sio asilimia 9 aliyosema Mhe Rais tena hadharani?

Tarehe 01 | 05 | 2021 Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa Jijini Mbeya alitangaza kodi ya mshahara kwa mfanyakazi kwa Kila mwezi [PAYE] ni 9% tu, Sasa nyie TRA mmepata wapi ruhusa ya kukata mshahara wa mfanyakazi kwa 30% tofauti na maelekezo ya amiri jeshi mkuu?

Hata kama mshahara huu uko in lampsam bado ni mshahara uleule unaotakiwa kukatwa kodi ya asilimia 9 tu kwa kuwa unabaki kuwa ni "Mshahara tu" bila kujali unalipwa kwa mwezi mmoja au kwa miezi mia kwa pamoja bado ni mshahara.

TRA kumbukeni Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alishasema yeye hataki pesa ya dhuluma kumbukeni kumtoza mtu kodi ya 30% badala ya 9% hizi ni pesa za dhuluma na zitainyima kura CCM 2025.

TRA rekebisheni maramoja huu ni wizi wa wazi kwa Wananchi kwani ni hasara kubwa kwa Chama kama usipochukuliwa kwa umakini unaostahili kwani tayari moto umewaka huko kwenye magroup ya whatsapp na ndio Mimi tu kuwaleteeni taarifa hii Kizalendo.

Kidumu chama cha Mapinduzi.

Cc:
Waziri Mkuu wa JMT,
Naibu Waziri Mkuu,
Waziri wa Fedha,
Kamishna Mkuu wa TRA
Hii haikubaliki na yeyote
 
Back
Top Bottom