System?...what do you mean its about the system? Plz Mwanakijiji if you can shortly explain to us who dont see the problem with the existing Social Security System.And if you can come up with an idea on how kiwira can better be revived for power generation.
Why don't you give us solutions?
Too many complaints!....thats so 90s!!
Kobello.. inaonekana hujasoma unadandia treni kwa mbele tu:
a. Rudisha Kiwira serikalini - bila kuwalipa kina Mkapa; ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani kina Mkapa na Yona kwa uvunjaji wa sheria ya Maadili ya Viongozi.
Option ya kwanza:
b. Tanesco wapewe uwezo wa kuendesha, serikali ilipe madeni ya Kiwira (likiwemo la NSSF na mengine)
c. Tanesco ipate mwekezaji wa kimkakati (ambaye ni China - wapo tayari na fedha zipo dola milioni 400).
d. Umeme utakaozalishwa hakutakuwa na capacity charge wala nini kwani ni mgodi wa Tanesco.. kutakuwa na malipo ya management n.k kwenda kwa Wachina.
e. Kiwira itakuwa ni mali ya Tanesco kama ilivyo Kidatu, Hale, n.k
Option ya Pili:
b. Tanesco/Stamico wanaunda kampuni ya holding yenye hisa za wananchi na mashirika hayo na za serikali - say 50/49/1
c. Shirika hilo litasimamia miradi yote ya serikali ya umeme na uzalishaji wake na kutoa gawio kwenye faida
d. Kiwira itakuwa bado ni mali ya serikali na vile vile suala la capacity charges na mambo mengine yataangaliwa kimkataba mzuri.
e. CAG apitie mahesabu na portfolio ya makampuni hayo kuona kama yako katika mazingira ya kuweza kupewa mgodi huo
x,y
Option ya tatu
b. NSSF ifanyiwe mabadiliko ya kisheria kwanza - kuweka suala la uwekezaji wake chini ya Panel of Investment kama wanavyofanya Malaysia na sehemu nyingine
c. Iunde kampuni tanzu ya Holding ambayo itasimamia uwekezaji wake wote - kampuni iwe ya hisa za kwanza za wanachama na katika mfumo wa matching shares.
d. Shirika hilo la uwekezaji la NSSF - nje ya uongozi wa NSSF ndio itawajibika na kusimamia miradi yote ya uwekezaji ya NSSF na kusimamia ugawaji wa faida - huku wanufaika wa faida kwanza kabisa wawe ni wanachama wa shirika hilo na wanahisa wake. Litasimamia kukusanya madeni yote kwa kiwango chote kinachowezekana kisheria.
e. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali apitie mahesabu ya uwekezaji mzima wa NSSF hadi hivi sasa kuona kama kuingia kwenye uwekezaji wa Kiwira kuna faida - hasa ukizingatia maneno ya Rais Kikwete leo kwenye hotuba ya kuzindua Bodi ya Usimamizi wa Mifuko ya Pensheni
Option ya nne:
b. Serikali ibakie na umiliki wa Kiwira
c. Itangazwe tenda ya uendeshaji wa Kiwira kwa mkataba mzuri na NSSF na taasisi nyingine ndani na nje wagombanie
d. Mshindi katika uendeshaji apatikane kwa mkataba mzuri na mnono utakaopitiwa na POAC na Mdhibiti Mkuu (or whatever have you)
e. Uwe ni mkataba ambao unakuwa ni reviewable katika kila kipindi fulani ukiwa na measured goals.
f. CAG apitie hesabu za kampuni yoyote ya umma itakayotaka kuingia kwenye mradi huu.
Chagua mojayahapo.. na ninaweza kuendelea na options nyingine nyingi na bila ya shaka watu wengine wanaweza hata kumodify hizo ooptions kuwa zifae zaidi.