Ooh Poor NSSF!! - What is this?

Ooh Poor NSSF!! - What is this?

And,I think NSSF is being audted by Audit General's office,but I don't mind an independent audit.
Having said that,don't you think the same should be done to TANESCO?...and STAMICO?...and NDC?,for a social security fund NSSF doesnt have that many investments,those are just petty investments!
My point is,I would really hate to see TANESCO take over Kiwira,and suprised to see Mtei's party that was established on the basis of MArket economy,turned out to be the biggest proponent of nationalization of previously failed parastatals! PLEASE KEEP THE GOVERNMENT OUT OF THESE PROJECTS!

Mkuu,

NSSF kama muwekezaji anaweza kuuendesha huu mradi wa makaa ya mawe vizuri tu bila ya tatizo. Ila ni vema NSSF wasikae muda mrefu katika mradi huu wanaweza kufufua ukafanya kazi vizuri ukiwa unazalisha kifaida wanaweza kukaa nao miaka 5 warudishe hela zao na faida wauza kwa bei ya juu kutengeneza faida.
 
Mzee Mwanakijiji,
Nadandia treni kwa mbele?...plz man,that was a low blow!
But anywayz,option ya tatu,is that what you meant by a broken system?You seem to doubt NSSF competence on this may be because it's not made up of geologists and electrical engineers,or at least you doubt their financial capability.

Matatizo ya Tanesco hayatokani na tanesco yanatokana na wanasiasa. Ni wanasiasa waliofikisha Tanesco ilipofika.

I don't realy see why are you so negative when it comes to NSSF investing in power generation,apart from your paranoia over corruption(which here is a constant,since all those other options are susceptible to it).

with the overwhelming evidence of massive corruption scandals unaita la kwangu ni "paranoia"?

Your solutions are the solutions lying at ngeleja's desk right now with the exception of AGs involvement and formation of those lousy holdings.
Let's look at these things from the financier's point of view,are you really gonna mess with TANESCO,as a private/independent banker?..NO
Are you going to mess with GOT?...no,they had it and failed.And,if the government wanted kiwira,they could have it...just pay NSSF their money.

Tanesco wameshindwa kwa sababu ya wanasiasa; haijapewa uhuru unaostahili kama ilivyokuwa kwenye matatizo ya mashirika mengine ya umma.

And,just as a hint...President Hu Juntao is kinda reluctant with his 400m$,and the
Hunan's deal is kind crappy too,and it's mainly focused on coal production.

Simlaumu Juntao kwa kuwa reluctant; kwa sababu anataka kuwa na uhakika na fedha zake na mpango mzima. Kwenye NSSF watu wanataka tudandie tu kwa sababu ni "wazo zuri" sisi wengine tunataka kuwa reluctant. Lengo ni kwamba habari na ufahamu wa kutosha upatikane.

I THOUGHT YOU HAD SOME REAL ISH!....But nah,you are just an independent corruption watchdog blogger who loves his country and I commend you for that.

Kwenye desk la Ngeleja kuna hoja ya kuifanyia NSSF mabadiliko ya kisheria na kimuuno ili iweze kuwekeza Kiwira? Really? Whats wrong with that - kama kweli ipo hivyo.
 
Kobello.. inaonekana hujasoma unadandia treni kwa mbele tu:

a. Rudisha Kiwira serikalini - bila kuwalipa kina Mkapa; ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani kina Mkapa na Yona kwa uvunjaji wa sheria ya Maadili ya Viongozi.

Option ya kwanza:
b. Tanesco wapewe uwezo wa kuendesha, serikali ilipe madeni ya Kiwira (likiwemo la NSSF na mengine)
c. Tanesco ipate mwekezaji wa kimkakati (ambaye ni China - wapo tayari na fedha zipo dola milioni 400).
d. Umeme utakaozalishwa hakutakuwa na capacity charge wala nini kwani ni mgodi wa Tanesco.. kutakuwa na malipo ya management n.k kwenda kwa Wachina.
e. Kiwira itakuwa ni mali ya Tanesco kama ilivyo Kidatu, Hale, n.k

Option ya Pili:
b. Tanesco/Stamico wanaunda kampuni ya holding yenye hisa za wananchi na mashirika hayo na za serikali - say 50/49/1
c. Shirika hilo litasimamia miradi yote ya serikali ya umeme na uzalishaji wake na kutoa gawio kwenye faida
d. Kiwira itakuwa bado ni mali ya serikali na vile vile suala la capacity charges na mambo mengine yataangaliwa kimkataba mzuri.
e. CAG apitie mahesabu na portfolio ya makampuni hayo kuona kama yako katika mazingira ya kuweza kupewa mgodi huo
x,y

Option ya tatu
b. NSSF ifanyiwe mabadiliko ya kisheria kwanza - kuweka suala la uwekezaji wake chini ya Panel of Investment kama wanavyofanya Malaysia na sehemu nyingine
c. Iunde kampuni tanzu ya Holding ambayo itasimamia uwekezaji wake wote - kampuni iwe ya hisa za kwanza za wanachama na katika mfumo wa matching shares.
d. Shirika hilo la uwekezaji la NSSF - nje ya uongozi wa NSSF ndio itawajibika na kusimamia miradi yote ya uwekezaji ya NSSF na kusimamia ugawaji wa faida - huku wanufaika wa faida kwanza kabisa wawe ni wanachama wa shirika hilo na wanahisa wake. Litasimamia kukusanya madeni yote kwa kiwango chote kinachowezekana kisheria.
e. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali apitie mahesabu ya uwekezaji mzima wa NSSF hadi hivi sasa kuona kama kuingia kwenye uwekezaji wa Kiwira kuna faida - hasa ukizingatia maneno ya Rais Kikwete leo kwenye hotuba ya kuzindua Bodi ya Usimamizi wa Mifuko ya Pensheni

Option ya nne:
b. Serikali ibakie na umiliki wa Kiwira
c. Itangazwe tenda ya uendeshaji wa Kiwira kwa mkataba mzuri na NSSF na taasisi nyingine ndani na nje wagombanie
d. Mshindi katika uendeshaji apatikane kwa mkataba mzuri na mnono utakaopitiwa na POAC na Mdhibiti Mkuu (or whatever have you)
e. Uwe ni mkataba ambao unakuwa ni reviewable katika kila kipindi fulani ukiwa na measured goals.
f. CAG apitie hesabu za kampuni yoyote ya umma itakayotaka kuingia kwenye mradi huu.

Chagua mojayahapo.. na ninaweza kuendelea na options nyingine nyingi na bila ya shaka watu wengine wanaweza hata kumodify hizo ooptions kuwa zifae zaidi.
Nimekupata mkuu,however hiyo option ya serikali kulipa madeni ya Kiwira (likiwemo la NSSF na mengine); kwanini umeiweka kwenye option ya kwanza peke yake?Maana naona kipengele hiki;"a. Rudisha Kiwira serikalini - bila kuwalipa kina Mkapa; ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani kina Mkapa na Yona kwa uvunjaji wa sheria ya Maadili ya Viongozi." Kiko applicable in regardless to whatever option....Je hicho kipengele cha serikali kulipa hayo madeni kiko applicable in either option kama kilivyo kile cha Makapa na wenzake kufikishwa mahakamani?I said this because options zote zinaanza na kipengele "be" ikiwa na maana kuwa kipengele "aa" kiko applicable in all otpions?
Hopefully umelipata swali langu kamanda.
 
MWANAMJINI,

Acha biashara ya UDINI.

Mwanakijiji anasuburi nimkabidhi madudu ya PPF kwa maandishi na nyaraka sio kwamba hajasikia ya PPF. Kwa sasa hana data in full. Atatoa mara akizifanyia kazi, hawezi kukurupuka kwa sababu tu wewe unataka. Wengi wetu tunatumia majina ya kujificha na hatufahamiki, lakini Mwanakijiji ana fahamika hivyo kila anachoandika lazima kiwe na ushahidi kamili. Keep it up MM.

Nakuandalia nondo za PPF ili watanzania waone inavyofanywa shamba la BIBI

Jmn hv kama mnamjua na sisi tuambieni jina lake tumjue mana kwakwel me personally waga namkubali sana kwa nondo zake
 
Mdongoaji wewe umesema hapo: Nakupa ChANGAMOTO HII:

1. Tafuta mahali popote katika maandishi yangu kuhusu NSSF au katika hoja nilizoandika mahali popote ambapo panaweza kuashiria nimeshambulia dini ya Dr. Dau au hata kusema kuwa NSSF isipewe kwa sababu inaongozwa na udini?

2. Tafuta mahali popote katika maandishi yangu kuhusiana na NSSF au Dr. Dau ambapo nimewahi kudai kuwa yeye ni fisadi au hata mahali ambapo panaweza kuashiria kuwa nimeashiria hivyo.

3. Tafuta mahali popote ambapo nimegusia suala lolote la kitaifa kwa mtu yeyote aidha katika kuunga mkono au kulipinga ambapo nilitumia kigezo cha dini yangu au ya mhusika na kufanya ndio msingi wa hoja yangu aidha ya kumuunga mkono au kumpinga.

Ukipata lolote kati ya hayo kauli yako hapo juu itakuwa ni ya ukweli vinginevyo ukikosa inabidi uje na kuifuta kauli hiyo.

Katika haya sihitaji kuyajibu kwani post zako zinaonyesha hoja zimetawaliwa na ubaguzi mwanakijiji. Kwanini kuna sababu mbili naweza kukupa ambazo hazihitaji mwanasayansi wa upasuaji au PhD kufahamu unalenga wapi?

Mosi umeshindwa kutushawishi kwanini tuhofie NSSF zaidi ya PPF au PSPF, LAPF. Hoja kubwa unayoileta jamvini ni ukubwa wa uwekezaji but unasahau kama pension na financial institution inatakiwa kukua kimtaji na kiundeshaji. Hivyo basi kutokana na hilo unasema NSSF inatumika kama mrija wa serikali kukamilisha mipango yao (even though huna ushahidi yakinifu kwa haya uyasemayo).

Pili mashambulizi yako yamelenga mifuko miwili kama ukisoma post zako za nyuma a. NSSF, b. PSPF but mashambulizi katika mifuko mengine umekuwa mchache mno kama sio hakuna kabisa. What do these financial institutions have in common? Wakurugenzi wakuu wote hapa ni waislamu (NSSF ni Dr Dau, PSPF ni Dr Mmanga).

Kama nilivyosema mwanzoni haihitajiki uwe na PhD au kuwa a nuclear scientist kufahamu unalenga wapi. Mifuko mengine je iko hali gani? Vp kule CRDB kwa Dr Kimei? Tushawishi zaidi NSSF wamekosea wapi nitabidili kauli yangu kwasababu awe muislamu au mkristo kama ni fisadi ni vema akemewe na kwa faida ya shirika na tanzania kwa ujumla.
 
Nilikujibu wakati ule kuwa unatengeneza a fallacy of false dilemma, kwamba uchaguzi ulikuwa ni wa aina mbili tu. Nadhani hukunielewa naweza kurudia kwa kina juu ya fallacy hiyo.

Nimeonesha hapo juu kuwa ndio umenituhumu bila ushahidi wowote hata wa kimazingira. Unless mtu mwingine aliingia na kutumia jina lako. Na kauli yako ambapo unapinga hujanituhumu umeisindikiza na tuhuma nyingine.

Hapana.. wala haihusiani na hilo peke yake bali na mfumo mzima wa kisheria - labda ufuatilie mfululizo mzima wa makala zangu juu ya NSSF ambapo nilichambua mambo mbalimbali ya kwanini NSSF ilivyo sasa isipewe Kiwira. It is not all about the risk exposure.. it is about the system!

TAfuta ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya 2007/2008 na ya 2008/2009 itakupa mwanga kidogo.

kwani lazima miye nizungumzie kila ufisadi wa kila taasisi Tanzania? Kwanini wewe usifanye hilo au mtu mwingine? Itakuwaje mtu mwingine wa PPF naye akaja (nikifanya hivyo) na kudai kuwa kwanini Mwanakijiji haangalii ufisadi wa Wizara ya Afya; na nikifuatilia la Afya mwingine wa afya akaja juu na kusema "mbona ameacha ufisadi wa DAWASA". Mtu mmoja kasema "mwanakijiji si Mungu".. haiitaji kufikiria sana kukubali na hilo. Sina uwezo wa kufuatilia kila kitu, kumfurahisha kila mtu wakati wote. Ninachangia kidogo ninachoweza na wengine nao wachangie wanachoweza. Kwanini wewe badala ya kutetea NSSF (waache wenyewe wajitetee) usiende kufuatilia na kufunua la PPF? Kinakushinda nini ambacho unafikiri mimi nina uwezo nacho?

Siasa again mkuu toa evidence Mwanakijiji kama huna ni vema uwaache NSSF uendelee na shughuli zako tu.
 
I know TANESCO is owned by the govt,thats why it's been bankrupt...or to be conservative,running on negative returns.
TANESCO failed to run on Hydroelectricity!!,failed to run a profitable power supply chain amid huge subsidies from the government,failed to invest in coal,gas,wind,solar and other renewable sources.
TANESCO failed to pressure the government on investing in protection of our water sources leading to power rationing and heavy dependenceY on non renewable sources coupled by lousy/bogus contracts with IPPs.
TANESCO failed to maintain its infrastructure,something that few people talk about.The infrastructure is obsolete and needs overhaul!
TANESCO failed to collect debts from you know who.
Honestly,TANESCO is bogus! and I blame the government on this.But,it can be revived through investment in its infrastracture,that will attract private partnership in transmission and distribution.
Till that is done my sister,TANESCO should never be allowed wananchi's moneys to play with!...they should be included in the Ngeleja's ministry's budget as a parastatal that needs heavy investment starting next budget year....i mean,HEAVY!

Dah,

Kobello nimeshindwa kufahamu umeandika nini sijui ni mie au sijui kiinglishi mkuu unakusudia kusema nini?
 
Katika haya sihitaji kuyajibu kwani post zako zinaonyesha hoja zimetawaliwa na ubaguzi mwanakijiji. Kwanini kuna sababu mbili naweza kukupa ambazo hazihitaji mwanasayansi wa upasuaji au PhD kufahamu unalenga wapi?

Mosi umeshindwa kutushawishi kwanini tuhofie NSSF zaidi ya PPF au PSPF, LAPF. Hoja kubwa unayoileta jamvini ni ukubwa wa uwekezaji but unasahau kama pension na financial institution inatakiwa kukua kimtaji na kiundeshaji. Hivyo basi kutokana na hilo unasema NSSF inatumika kama mrija wa serikali kukamilisha mipango yao (even though huna ushahidi yakinifu kwa haya uyasemayo).

Pili mashambulizi yako yamelenga mifuko miwili kama ukisoma post zako za nyuma a. NSSF, b. PSPF but mashambulizi katika mifuko mengine umekuwa mchache mno kama sio hakuna kabisa. What do these financial institutions have in common? Wakurugenzi wakuu wote hapa ni waislamu (NSSF ni Dr Dau, PSPF ni Dr Mmanga).

Kama nilivyosema mwanzoni haihitajiki uwe na PhD au kuwa a nuclear scientist kufahamu unalenga wapi. Mifuko mengine je iko hali gani? Vp kule CRDB kwa Dr Kimei? Tushawishi zaidi NSSF wamekosea wapi nitabidili kauli yangu kwasababu awe muislamu au mkristo kama ni fisadi ni vema akemewe na kwa faida ya shirika na tanzania kwa ujumla.

Hii ni projection yako wewe mwenyewe. Haina msingi katika ukweli wowote zaidi ya hofu yako.
 
NSSF Wanataka kujikomboa wao ama wanataka kuikomboa energy ministry?
Kama msukumo wa kuinvest Kiwira ungekuwa unatona nje ya NSSF,then hapo kusingekuwa na mashaka.Ninajiuliza hivi NSSF yenyewe hai hitaji rescue?
 
Pili mashambulizi yako yamelenga mifuko miwili kama ukisoma post zako za nyuma a. NSSF, b. PSPF but mashambulizi katika mifuko mengine umekuwa mchache mno kama sio hakuna kabisa. What do these financial institutions have in common? Wakurugenzi wakuu wote hapa ni waislamu (NSSF ni Dr Dau, PSPF ni Dr Mmanga).

umewahi kunisikia au kunisoma juu ya PSPF? wapi huko au bado una project hofu zako kwangu. Hata sijui kirefu cha huo mfuko! Sijawahi kuuzungumzia wala kuufuatilia - labda kama unaushahidi wowote to the contrary.
 
Umesahau Quality Plaza? au sio wewe uliyeileta jamvini?
 
Hii ni projection yako wewe mwenyewe. Haina msingi katika ukweli wowote zaidi ya hofu yako.

Sawa Mzee mwenzangu but fumbo mfumbie mjinga mwerevu huling'amua some of us tunaweza kuunganisha matukio tukapata kukufahamu unalenga wapi.
 
NSSF Wanataka kujikomboa wao ama wanataka kuikomboa energy ministry?
Kama msukumo wa kuinvest Kiwira ungekuwa unatona nje ya NSSF,then hapo kusingekuwa na mashaka.Ninajiuliza hivi NSSF yenyewe hai hitaji rescue?

From what mkuu umesikia kwani NSSF wamefile for bankruptcy? Au BOT imewafine??
 
Siasa again mkuu toa evidence Mwanakijiji kama huna ni vema uwaache NSSF uendelee na shughuli zako tu.

Yaani NSSF waachiwe kutafuna mpunga wa walipa kodi kinyemela? Give me a break ... .... ..... when will this country follow the rule of law? JK nchi imekushinda, sijui tukwambie mara ngapi huwezi kuongoza hii nchi uliingia kwa wizi na utatoka kwa wizi.
 
Sawa Mzee mwenzangu but fumbo mfumbie mjinga mwerevu huling'amua some of us tunaweza kuunganisha matukio tukapata kukufahamu unalenga wapi.

na wakristu nao waseme ninawashambulia kina Mkapa na wengine kwa sababu ya Ukristu wao kwa sababu na wenyewe wameng'amua. Kimsingi hauna chembe hata moja ya ushahidi wa kunifikiria udini; ila ni wazi utetezi wako unaufanya kwa sababu ya dini za wahusika. Udini kumbe uko upande wako siyo kwangu. Hutetei NSSF kwa sababu ya ukweli bali kwa sababu Mkurugenzi wake ni Muislamu. Come out and admit that. Lakini hutapata chembe hata moja ya mimi kuzungumzia jambo lolote kwa misingi ya dini za wahusika. NONE WHATSOEVER..
 
Yaani NSSF waachiwe kutafuna mpunga wa walipa kodi kinyemela? Give me a break ... .... ..... when will this country follow the rule of law? JK nchi imekushinda, sijui tukwambie mara ngapi huwezi kuongoza hii nchi uliingia kwa wizi na utatoka kwa wizi.

Of course lazima NSSF isimamiwe na kuna vyombo vinawasimamia, je SSRA wameshasema kitu, BOT wameshasema kitu? Sasa mnapiga kelele za nini JF pipili ya shamba inawawashia nini nyie?

Vile vile nachoshangaa pia wachangiaji wengi wameshawatuhumu NSSF mafisadi wakati hakuna hata mmoja wenu ambaye na vithibitisho juu ya hilo kama sio chuki nini hizo? Na JK ameingia wapi hapo mkuu.
 
Back
Top Bottom