Inawezekana pengine anauwezo wa kupata taarifa nyingi zaidi (za kifisadi) za NSSF kuliko zile za PPF (or PSPF, GEPF, LAPF etc) lakini hili halitakuwa na maana kuwa huko hakuna ufisadi. Kama kuna ufisadi NSSF au kwengineko ni lazima ufunuliwe bila kuangalia kiongozi wake ni wa imani gani.
Tusije tukafika mahala tunashindwa kuwawajibisha viongozi tuliowachagua/tuliowapa dhamana kwa kuogopa eti watu wa dini yake watadhani ni kwa sababu ya dini yake. Tunayaona haya yanaaza kujitokeza sana katika siku za karibuni. Watawala kwa ujanja ujanja wanajaribu kujibanza kwenye kivuli cha udini. Tanzania ni yetu sote.
Kama anapata taarifa za kifisadi (kama zipo maana so far tunapewa taarifa za tuhuma, majarida ya magazeti, taarifa za vikao) za NSSF kwanini asisubiri na za PPF, PSPF, na LAPF ndipo azungumzie mustakabali mzima wa pension fund sector na uchumi wa Tanzania.
Na taarifa za kifisadi zipo hapa JF kuna wadau wa PPF walianzisha thread sijui imepotelea wapi but ukichungulia yaliyokuwa yakizungumziwa humo ndani na hao whistleblowers ni ya kutisha kushinda hata ya Dau (kama kweli kama mnavyodai ni fisadi). Hatudanganyiki!!!!