Hii ndiyo tunaita siasa!!....hebu tupeni vcersion yenu ya mustabali huu wa NSSF overinvestment,cause we need these 300mw at the end of the year ready for next kiangazi!!!
Kobello, kwangu mimi udhaifu mkubwa uko kwenye sheria na muundo mzima wa NSSF ilivyo sasa. Ndio maana kati ya vitu ambavyo navipigania sana ni kwamba NSSF inahitaji major overhaul ili kuweza kuweka sheria nzuri zaidi ya Social Security Funds kwa nchi nzima ambayo itaweka taratibu za mifuko ya umma na ile ya binafsi. Lakini siyo hivyo tu bali pia muundo mzima wa NSSF (na hata mashirika mengine ya umma) una loop holes nyingi ambazo zinachangia na tayari zimechangia sana katika kudhoofisha mifuko hiyo -kiutendaji na kiutawala.
Mapendekezo yaliyotolewa na CAG mwaka 2008/2009 hadi leo hayajafanyiwa kazi. Mkaguzi mkuu alisema wazi kabisa kuwa baadhi ya uwekezaji wa NSSF ambao alisema "hauna tija"
Sera yetu ya
Social Security Funds (ya mwaka 2003)sidhani kama imebadilika hadi leo ilitoa hukumu hii kuhusu masuala ya uwekezaji: (msisitizo wa mistari wangu)
2.4(b)
ix)
Investment of Social Security Funds
There has been
inadequate guidance on investment of social security fund at national level.
Ikasemwa kwenye hiyo policy guidelines kuwa :
3.12
Policy Issue: Investment of Social Security Funds
Investment of social security funds is an inseparable function of social security institutions. Sustainability of the schemes and
improvement of benefits depend on investment income.
Social security funds have often been directed to areas where there is no stimulation of economic growth. There are no clear-cut guidelines directing investments of social security funds at the national level.
Na kuhusu utawala bora ripoti hiyo iliyosainiwa na Prof. Kapuya (akiwa waziri wa kazi wakati ule) inasema:
3.13
Policy Issue: Good Governance
Good governance is the key to smooth functioning and efficiency in all social security schemes, as they are entrusted to manage funds on behalf of the contributors. T
here has been poor governance in social security services.
Sasa, haya si mambo ya leo tu; kumbuka kuwa hiyo ilikuwa ni ripoti ya sera ya 2003 na ripoti ya CAG ya 2007/2008 na mwaka iliyofuatia yote imejikuta na matatizo yale yale. Tunasubiri kuona ripoti ya 2009/2010 itakuwaje.
Katika mkutano mmoja wa kimataifa huko Ufaransa mwaka 2008 Bw. Baruti (Meneja wa Mipango na Uwekezaji) wa LAPF (Local Authority Pensions Fund) alisema hivi kuhusu mambo ya uwekezaji na mifuko ya jamii:
[FONT=Garamond, serif]The challenges facing Tanzanian social security system include uneven benefit[/FONT][FONT=Garamond, serif] packages among the existing SSIs,
inadequately regulated investment activities, limited coverage and the role of SSIs in the fight against poverty. In responding to these challenges, some of these SSIs have implemented parametric reforms in an attempt to adapt to changes brought about by the changing socio-economic environment. Consequently, the scope and depth of benefits have increased. Others have amended their respective legislation to cover sectors previously not covered by these schemes. The recent reform initiative is the formulation of Social Security (Regulatory Authority) Bill of 2008, which is expected to be enacted in 2008.
The Act will establish the regulator of social security.[/FONT]
[FONT=Garamond, serif][/FONT]
[FONT=Garamond, serif]
Huyo regulator ndiyo hii bodi iliyozinduliwa juzi na Rais. Bahati mbaya sijapata nafasi ya kuipitia sheria yake kuweza kuona ni kwa jinsi gani inajibu swali la "adequacy" katika masuala ya kusimamia uwekezaji. [/FONT] Maana tayari tatizo moja ambalo limeshaonekana ni kuwa sheria nyingi za hizo Pension Funds haziitambui bodi hiyo - hivyo zinahitaji zenyewe kufanyiwa mabadiliko kwanza!
Mabadiliko ya NSSF ni lazima kama kweli tunaitakia mema na tunawatakia mema wanachama wake. Mifano uliyotoa kwa mfano ya Rwanda, ni mizuri lakini wenzetu walifanya mabadiliko sheria yao na hata muundo wao miaka miwili au mitatu iliyopita na mabadiliko yao yanaendelea - mengi yatakuwa yanakamilika mwaka huu. Nchi kama Malaysia ambayo huwa inatolewa mfano sheria yao iko tofauti na ya kwetu katika masuala ya uwekezaji.
Kwa vile nchi nyingine zinawekeza mahali fulani haina maana na sisi tufuate tu bila ya kuangalia the legal framework or structural make up ya mifuko yao. Ninachoogopa mimi ni haya madai kuwa "nchi fulani wanafanya" basi na sisi tufanye hata kama mifumo na sheria zetu zina tofauti kubwa. Hakuna mtu ambaye anasema NSSF isiwekeze mahali popote - itakuwa haina maana kwa mfuko wa hifadhi ya jamii; baadhi yetu tunajua tatizo letu lilipo sasa hivi na kwanini kabla hatujaingia kwenye matatizo huko mbeleni ni bora kufanya mabadiliko ya msingi sasa hivi ili kwamba tupunguze risk ya kwenda vibaya huko mbele. Wengine hapa wanasema uwekezaji ni "risk" na hivyo tuwekeze tu - bila kujali risk iliyopo.
Huku ni kutokuwajibika. Tayari tumeshaona matatizo mengi kwenye sekta ya nishati; hili haliitaji mtu kushawishiwa sana. Na NSSF inataka kuwekeza kwenye nishati kwa kutumia fedha za umma. Well.. what are the chances kwamba kitu kinaweza kwenda vibaya huko mbeleni? - wapo wanaosema "nothing will go wrong" na wengine wanasema "yeah.. inaweza kwenda vibaya lakini ndiyo sababu ya risk katika investment". Wengine tupo tunasema "tufanye jitihada za kubadilisha sheria na miundo yetu mbalimbali ili kupunguza uwezekano wa kitu kwenda kombo".
Watu hawataki wanasema "tuwekeze tu kwa sababu fedha zipo". This is being irresponsible.