One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

CDM msaliti ni yeyote asiyesikilizana na Mbowe na Slaa, au yoyote mwenye mtazamo tofauti,mambo ya ajabu kabisa.

CDM tuliyokuwa tunaipa sapoti ya nguvu humu circa 2006-7 sio hii ya leo iliyojaa watoto wasiojua hata kuunga sentensi mbili za kiswahili. Nasikitishwa sana na hii hali, sijui kwanini uongozi wa CDM waliacha hali ikafikia kwenye hatua hii bila wao kufanya damage control.

Sasa hivi imekuwa haiwezekaniki kujadili mada na vijana wa CDM kabla hawajaanza kutoa lugha za maudhi na kero.Yani kila akiandika sentensi mbili, anaanza wewe msaliti, wewe msaliti.yani hopeless kabisa.

Nadhani huijui Chadema au we ndo Zitto kwa ID nyingine, Chadema tuliwahitaji ma-prof na wasioweza kuunganisha sentensi. Hawa ndo watazania wanaohitaji kukombolewa!
 
Hayo ndio maelekezo yetu kwa wanachama wetu; Kupambana na adui mmoja tu - CCM.

Hii platform au tuseme "ideology" pekee ya "Kupambana na adui CCM", metrics au vipimo/mafanikio yake yanakuwaje? Politics as usual as long as ruzuku tax-money is guaranteed?
 
Ndugu wana JF,

Kwa muda mrefu na hasa siku za hivi za karibuni kumekuwa na threads nyingi sana humu ndani kuhusu Zitto na kuhusu Chama cha ACT Wazalendo. Kumekuwa na tuhuma kwamba chama cha ACT Wazalendo kinashambulia vyama vingine vya upinzani hapa nchini. Napenda kusema mambo machache sana

Chama cha ACT Wazalendo ni chama cha siasa chenye mrengo wa kushoto na kinajitanabaisha na siasa ya Ujamaa iliyoasisiwa na Azimio la Arusha. Lengo letu ni kueneza siasa zetu zenye mrengo huo.

1. Chama cha ACT Wazalendo kwa sasa ni chama cha upinzani nchini. Kimekuja kuhuisha zaidi siasa za upinzani ili kuiondoa CCM madarakani. Chama cha ACT Wazalendo hakina lengo hata kidogo kuzorotesha upinzani nchini. Tofauti zetu tulizokuwa nazo katika chama tulichokuwamo wengine tumeshazifuta, tumepiga mstari na kutazama mbele.

Ndio maana hutasikia kiongozi hata mmoja wa ACT Wazalendo akihangaika na vyama vingine vya upinzani. Hata tukichokozwa namna gani tumefanya maamuzi kwamba hatutajibizana na chama kingine chochote cha upinzani hapa nchini. Tutapambana na chama tawala ili kubomoa mfumo wa uchumi unaonyonya wengi na kufaidisha wachache. Tutapigania uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi. Tutapambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote. Hizo ndizo kazi tulizo nazo.

2. Tunasisitiza, tunayo vita moja lakini una njia nyingi za kupigana dhidi ya adui. Huko tulipokuwa tulitofautiana mbinu hizo. Sasa tumepata jukwaa la kutumia mbinu hizo. Wenzetu watumie mbinu zao pia. Hatimaye kila mmoja alenge shabaha kwa adui mmoja. Tunasema One Struggle, Many Fronts

3. Kuitana mamluki, wasaliti nk ni siasa za framing tu. Sio mara ya kwanza siasa hizi kutumika nchini katika kujaribu ku frame watu. Mwaka 1995 Mrema wa NCCR aliita CHADEMA chama cha mashushu kutoka Benki Kuu na kila mtu alimwamini. Leo Mrema yupo wapi na CHADEMA ipo wapi? Mwaka 2000 mpaka 2005 CUF ndio ilikuwa chama kikuu cha upinzani na kuidharau CHADEMA. Mwaka 2013 CHADEMA iliita CUF chama cha mashoga.

Miaka yote Mbatia amekuwa akiitwa pandikizi nk. Yote haya hayajazuia vyama hivi kufanya kazi pamoja hivi sasa. Ni vizuri sana wanasiasa kuweka akiba ya maneno. Hakuna sababu ya kutukanana na kuitana majina mabaya. Tunachohitaji ni kila mmoja kumlenga adui ili kumshinda. Tulishindwa kufanya kazi ndani ya moja, tunaweza kufanya kazi tukiwa majirani. Adui bado ni yule yule.

4. Sisi ACT Wazalendo tutachochea kuni kuwasha moto wa mapinduzi nchini kwa kuendesha siasa za masuala (issues). Tumeanza ziara yetu mkoa wa Ruvuma kwa sababu ni mkoa ambao wabunge wake wote ni CCM. Tutaweka nguvu sana maeneo hayo badala ya maeneo ambayo tayari vyama vingine vya upinzani vina nguvu. Sisi katika ACT wazalendo tunataka kuona uchumi unarudi kwa wananchi wenyewe badala ya uchumi kushikiliwa na watu wachache.


Tunataka kuona Miiko ya Uongozi inarudi ili kurejesha imani ya wananchi kwa viongozi wao. Tunataka kuona mfumo madhubuti wa uwajibikaji nchini. Hayo ndio mapambano yetu. Hayo ndio maelekezo yetu kwa wanachama wetu; Kupambana na adui mmoja tu - CCM.
Ningefurahi kuona vijana kwa wingi kuunga mkono ujamaa. ujamaa ndio sera pekee inayoweza kuleta mapinduzi ya uchumi wenye kuboresha maisha ya wananchi wote. sera ya sasa ccm kurejesha hatamu za uchumi wa taifa kwa mabwanyenye na mabepari wa kigeni ni aibu kubwa. ardhi ya wananchi vijijini imeporwa na wageni kwa kiinimacho cha vikao bandia na eti serikali inajidai kama haiwezi kuwarejeshea wananchi ardhi yao. sasa wasishamgae maana wananchi wataanza kutwaa ardhi yao wenyewe.
 
Nadhani huijui Chadema au we ndo Zitto kwa ID nyingine, Chadema tuliwahitaji ma-prof na wasioweza kuunganisha sentensi. Hawa ndo watazania wanaohitaji kukombolewa!


This i expected, sio mara ya kwanza mkikosa hoja kuanza kuropoka hovyo bila chembe ya evidence. Ndio maana kina makamba Junior wanawatungia sheria kandamizi.

Sasa kama maprofesa wapo, msioweza kuunganisha sentensi mbili kwa nini ndio muwe mbele kujadili maswala ya CHAMA, na hivyo kukitia DOA? Hamuoni kuwa mnakipa taswira mbovu chama chenu?

yani humu JF ukifungua Mada inayohusu CDM haina tofauti na kijiwe cha shule ya kata, lugha chafu, matusi, assumption za kijinga na hoja dhaifu kabisa.

Mara nyingi hoja zikionekana hazina msaada inawekwa soundtrack ya msaliti hadi inakera.JF wakifuta comments zenu mnalalamika. Binafsi naamini they are doing CDM a favour.

Kama wewe ndio sampuli ya mkombozi na mimi ndio mkobolewaji, sidhani kama nitanyanyua mguu wangu kukufuata. Onesha kuwa una "substance" ya kuwa mkombozi kabla ya kuanza kuimba ukombozi.
 
Yoyote atakaeishambia act na sisi vijana wa cama atutaeza vumilia tutashambulia tu kwani ndio sifa ya askari usisubiri idhini yoka kwa mkuu wakati unamuona adui yako alishaanza piga mengine yatafata japo mkuu hataki
Sihitajiki kukujibu, maana kwa uelewa, umri na mtazamo wako nadhani tunapishana sana.
 
sasa unategemea Zitto aje humu kumkemea mwanachama mmoja mmoja?alichofanya kuandika "msimamo" wa chama ni sahihi, sasa yule atakayefuatisha taarifa au comment kutoka kwa kina pangupabichi wenye kuficha majina yao watakuwa wanafanya makosa wao.

La msingi itakuwa kama Zitto akikutwa anatenda kinyume na alichoandika hapa. Huwezi kuongoza kundi la maelfu wa watu na wote wakafuatisha unachosema bila kutoka nje ya mstari, ukiona unaongoza watu wa aina hiyo jua kuna problem hapo.Binadamu wako na free will.
Sasa unatetea nini?...umeisoma au kupitia walau juu-juu katiba yao juu ya "KIONGOZI WA CHAMA"? Ana absolute power kwa wafuasi wake, kama ndivyo hivyo anachokisema kiongozi, wanachama wanapaswa kutii!

Ndio maana wenzenu tunasema ujamaa unaopiganiwa na ACT is illusion! Haiwezekani anchosema "kiongozi wa chama" kwa niaba ya chama kiwe chake binafsi rafiki!
 
Sasa unatetea nini?...umeisoma au kupitia walau juu-juu katiba yao juu ya "KIONGOZI WA CHAMA"? Ana absolute power kwa wafuasi wake, kama ndivyo hivyo anachokisema kiongozi, wanachama wanapaswa kutii!

Ndio maana wenzenu tunasema ujamaa unaopiganiwa na ACT is illusion! Haiwezekani anchosema "kiongozi wa chama" kwa niaba ya chama kiwe chake binafsi rafiki!

Nilichoandika na mtazamo wangu kuhusu katiba yao ni mutually exclusive. Usipigie mstari kuwa kwa kuwa nimesema posibility ya Zitto kuwa monitor au kujibu hoja moja moja ni ngumu, basi nakubaliana na vipengele vyote vya katiba yao. Hii mada haijadili katiba ya ACT.

Kwenye mada wanayojadili katiba yao, nimeweka wazi kuwa Kiongozi mkuu hatakiwi kufanya micromanagement. Nikaainisha kuwa kama walipenda format ya Labour inayotumika hapa UK, wangekopi proffersional patr ya Labour, ambayo ndio ina deal na hizi issue kama communications, social media etc. hii part ya Labour sio wanasiasa, bali wataalamu wa Social media, na kuna wataalamu wa vitu vingine pia huko ndani, ingawa kwenye Kamati kuu ya Labour wanakuwa na mwakilishi wao ndani ya Kamati, kuelezea na kushauri kutoka kwenye proffesional side.


Collectively, wanachama wanatakiwa wa-akisi kile ambacho kiongozi wao anafuatisha, kama hawakubaliani naye wanaweka wazi mitazamo yao kupitia sehemu husika kwenye vyama vyao, au wanaenda kule ambako mitazamo yao inaendana na viongozi husika na sera husika.
 
Hivi siku hizi Zitto nae kawa Mods humu JF!?

Mbona kuna maswali yangu kibao yamefutwa!?

kama siyo basi Mods mnamlinda huyu Msaliti na hii si haki kabisa!!
 
Last edited by a moderator:
Makala hii iliandikwa na Samson Mwigamba tar 9//12/2009
NAKUHURUMIA ZITTO KABWE
MHESHIMIWA Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, salaam.
Awali ya yote naomba kama nianze kwa kutangaza mgongano wa kimaslahi kama ilivyo kawaida kwa wabunge kufuatana na Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la Mwaka 2007.
Mgongano wa kimaslahi ni kwamba ninakuandikia waraka huu nikitaka kujadili machache juu ya mwenendo wa mambo ndani ya CHADEMA, mambo ambayo yanakugusa kila wakati nikitaka kujaribu, kwa faida ya wasomaji, kuangalia kulikoni na wakati huohuo nikijua kwamba wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na ambaye tumekuwa pamoja tukikubaliana kwa mambo karibu yote, wakati wote.
Mheshimiwa unajua urafiki wetu ni wa muda mrefu na kwa kweli nilikupenda kabla wewe hujanifahamu; nikakuhesabu kama rafiki kabla hujanifahamu na kwa bahati nzuri sana uliponifahamu ukakubali kuwa rafiki yangu. Nimekuunga mkono katika matukio, maamuzi na hata mitazamo yako mingi kwa muda mrefu.
Nilikuwa upande wako katika kupiga vita ufisadi na hata uliposimamishwa ubunge wakati wa hoja ya Buzwagi nilikuwa upande wako.
Nilikuwa upande wako ulipotoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga utaratibu wa kuwachagua wabunge wa Afrika Mashariki na hata katika kile ulichokiita ‘bifu' kati yako na Spika wa Bunge, lililotokana na hatua yako ya kutoka nje ya ukumbi wa bunge na maneno uliyoyatoa nje ya ukumbi huo kuhusu uwezo wa spika kusimamia kanuni za Bunge.
Nilikuwa pia upande wako uliposimama kumtetea Spika kuhusu hoja iliyotolewa na mwandishi mmoja akipinga uwepo wa Kamati ya Bunge ya Kutunga Sheria katika kanuni mpya za Bunge.
Nilikuwa upande wako pale ulipounga mkono maelezo ya kitaalam ya TANESCO kununua mitambo ya Dowans na hili unalifahamu zaidi maana tulikuwa tukiwasiliana sana na huenda mimi na Absalom Kibanda ni miongoni mwa waandishi wachache sana tuliodiriki kusema waziwazi kupitia kalamu zetu kwamba tunaunga mkono msimamo wako wa kununua mitambo ya Dowans.
Utakumbuka pia siku moja tulipishana mtazamo tulipokuwa tukichangia kwenye mtandao mmoja wa intaneti hoja ya utafiti wa taasisi moja iliyoonyesha kwamba bado Kikwete na CCM ni maarufu kuliko vyama vya upinzani kwa mbali sana.
Unakumbuka kwamba mimi nilitofautiana na wewe kwa hoja za kitaalam zinazohusu utafiti. Lakini baada ya kutoa hoja zako na mimi nikatoa hoja zangu na wewe ukazijibu nilikubaliana na wewe na hatimaye nikawa upande wako.
Lakini katika siku za karibuni nimejikuta nikiwa katika mfululizo wa matukio, mitazamo na maamuzi ya mimi kutokubaliana na wewe. Utakumbuka nilianza kutokubaliana na wewe kuhusu uamuzi wako wa kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa taifa wa CHADEMA.
Nilikutumia barua pepe ndefu sana nikipinga uamuzi huo na kukuomba kwamba ujitoe kwa hoja nyingi ambazo najua unazikumbuka vema.
Kwa bahati mbaya hukujibu ile barua pepe, lakini sikukata tamaa, nikaambiwa nipitie kwa msaidizi wako David Kafulila. Nikafanya hivyo na Kafulila akanihakikishia kwamba kila tunachoongea anakufikishia na kwamba unampa majibu ya kunipatia.

Lakini mheshimiwa unakumbuka kwamba mwishoni kabisa majibu yako yalikuwa ni kwamba hoja zangu zote ulikuwa unazikubali lakini ulishazizingatia kabla hujaamua kujitosa kwenye kugombea uenyekiti na hivyo usingejitoa. Nashukuru kwamba baadaye uliamua kujitoa japo ulikuwa umechelewa.
Mheshimiwa Zitto, nilitofautiana na wewe pia kwa kauli zako ulizokuwa unazitumia kutaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla ya kujiondoa.

Katika moja ya taarifa za habari ulinukuliwa ukisema unatofautiana na Mbowe kwa sababu wewe ni mjamaa wakati yeye ni bepari. Nikawaza na kukumbuka kwamba Agosti 13, 2006 wakati chama chenu kinazinduliwa upya ulikuwepo na ninaamini ulishiriki kikamilifu katika kufanya utafiti, kuchambua na hatimaye kuja na katiba mpya iliyowasilishwa kwenye mkutano mkuu siku hiyo na kupitishwa kuwa katiba mpya ya chama hicho.
Na kwamba maneno haya yanayosomeka kwenye utangulizi wa katiba hiyo mpya ya CHADEMA yakiwa
yametamkwa kwa kunyanyua mikono na wajumbe wa mkutano huo mkuu, basi yalikuwa ni yako pia: "Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika Agosti 13, 2006, mjini Dar es Salaam, tumeamua kuifanyia mabadiliko Katiba ya 2004 ya Chama chetu cha siasa kitanachoitwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya Nguvu na Mamlaka ya Umma na Dira na Dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea.
"Kuanzia sasa CHADEMA, kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitavyotungwa kwa mujibu wa Katiba ili kuimarisha kutetea, kudumisha, na kuendeleza Demokrasia ya kweli na hatimaye kuweza kuleta maendeleo ya kweli ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa jamii nzima ya taifa la Tanzania."
Kama na wewe ni miongoni mwa wana CHADEMA waliotamka maneno hayo siku hiyo kwamba: "Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitakavyotungwa kwa mujibu wa Katiba hii" nilitegemea uwe umeisoma katiba yenyewe na kuona kwamba ibara ya 3 ya katiba hiyo, ibara ndogo ya 3.B. kifungu cha 3.1.1 kinasema "CHADEMA ni chama cha itikadi ya Mrengo wa kati (center party)".
Hata kwa elimu ndogo tu maelezo haya yanatosha kuonyesha kwamba chama hiki kinaongozwa kwa itikadi iliyoandikwa ndani ya katiba ambayo ni Mrengo wa Kati na wala si itikadi binafsi ya Mbowe ya ubepari ama ya Zitto.
Kwa imani niliyokuwa nayo kwako na nikizingatia elimu kubwa uliyokuwa nayo, nafsi yangu ikanituma kufikiria kwamba labda ‘wamekunukuu vibaya'. Nilihudhuria mkutano wenu na waandishi wa habari uliokusudia kuzika tofauti zenu na Mbowe na kusonga mbele kama chama.
Pale ulipoulizwa swali na mwandishi mmoja kwamba utawezaje kufanya kazi na Mbowe wakati wewe ni mjamaa na yeye ni bepari; ukajibu kwa namna ambayo haikukata kiu yangu ndipo nikaamini kwamba kumbe hukunukuliwa vibaya bali ni kweli ulisema maneno hayo.
Nilipingana na wewe pia pale ulipoamua kupinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA).
Unakumbuka kwamba nilialikwa katika uchaguzi huo miongoni mwa wageni wachache wanafunzi, wanahabari, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali walioalikwa kushuhudia uchaguzi ule.
Wakati wa uchaguzi wenyewe utakumbuka mimi na wewe tulikaa meza moja na tulitenganishwa na mtu mmoja tu (Mkurugenzi wa Uenezi Taifa wa CHADEMA, Erasto Tumbo).
Nilitegemea mambo yasiyoendana na sera na kauli mbiu za chama chenu ambazo zinatangazwa hata katika jina la chama (DEMOKRASIA na MAENDELEO) ambayo yalifanyika pale ukumbini uliyaona.
Najua jioni wakati wa kutangaza matokeo hukuwepo lakini nategemea ulipata taarifa za kauli za vijana mbalimbali walizotoa pale wakitaja waziwazi majina ya watu walioharibu uchaguzi ule.
Sikutarajia kama Naibu Katibu Mkuu wa chama upinge hatua ile iliyochukuliwa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na kikao kingine chochote cha juu ya msimamizi wa uchaguzi eti kwa sababu tu rafiki yako Kafulila alikuwa anaongoza.
Hilo lilinipa taabu kubwa na naomba uniwie radhi rafiki yangu lakini nasema ukweli wa nafsi yangu kwamba nilifikia kujiuliza mara mbilimbili kama ungechaguliwa wewe kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, hali ingekuwaje?
Na mwisho nilipingana na wewe pale ulipopinga kwenye vyombo vya habari kuvuliwa wadhifa kwa David Kafulila. Kwanza ulionekana umeweka ubaguzi kwa sababu katika maneno yote uliyonukuliwa ulisisitiza juu ya Kafulila peke yake na hukumgusia kabisa Danda Juju wakati wote walivuliwa kwa sababu
zinazofanana.
Lakini kwa sababu Kafulila ni rafiki yako sana, umemwandaa kuwa mbunge na unamuunga mkono katika harakati zake, na ni mbunge mtarajiwa kwa kuwa anakubalika sana jimboni basi ukamtetea na kumsahau ‘mhanga' mwenzake. Hilo tu linafanya tutofautiane na zaidi sana tunatofautiana kwa kupinga maamuzi ya Katibu Mkuu wako nje ya vikao, maamuzi aliyoyachukua kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
Najua yote haya umeamua kuwa kimya hujayatolea kauli yako ikiwa ni pamoja na yale ya kumfadhili Kafulila kwenda Kigoma kuichafua vizuri CHADEMA. Lakini kama ni kweli, napingana na wewe na kama unaendelea kukaa kimya nitaamini kwamba ni kweli.
Sasa limeibuka la kusema kwamba unatembea na barua ya kujiuzulu nyadhifa zako zote ndani ya CHADEMA ikiwa ni pamoja na ubunge. Bado pia sijapata kauli yako, narudia kusema kwa kuendelea kunyamaza unanifanya niamini kuwa ni kweli.
Na kama ni kweli, nakuhurumia sana Zitto Kabwe. Sasa naona kile nilichokuambia wakati nikikushauri ujitoe kugombea uenyekiti kinatimia. Nilikuambia ujitoe haraka tena kimyakimya kwa kumweleza tu Katibu Mkuu aweke fomu yako pembeni lakini hukutaka kunisikia.
Lakini utakumbuka moja ya sentesi zangu ilikuonya kwamba ukingang'ania kugombea iwe umeshinda
uenyekiti ama umeshindwa utapata shida kubwa. Nilikueleza kwamba hutaaminika tena na Watanzania na kila kitu utakachofanya utaonekana kama ulikuwa ni mamluki ndani ya chama.
Ni kwa bahati kwamba umetokea kuwa na viongozi wenye busara sana kina Freeman Mbowe na kina Dk. Wilbrod Slaa wakisaidiwa na hekima na kamati ya wazee.
Hawa wakaamua kukurejesha kwenye unaibu katibu mkuu. Nilishuhudia siku ile wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA walivyoshangilia uteuzi wako na wa Dk. Slaa na Hamad Yusuph kama wakuu wa Sekretarieti ya chama.
Nilidhani sasa ungetulia na kufanya kazi ya kujenga chama chenu na kusonga mbele lakini haikuwa hivyo.
Baada ya kushauriana sana wakati ule ulipotaka kugombea uenyekiti niliamua kutafuta habari za kiuchunguzi ndani ya CHADEMA. Nimeongea na viongozi mbalimbali na maofisa wa CHADEMA makao makuu, nimeongea sana na David Kafulila na hata niliwahi kumsikiliza mama yako mzazi akiongea na watu ambao sikuwafahamu.
Nimegundua kitu kimoja tu: kwamba kama mambo haya huyafanyi kwa makusudi na kwa malengo maalumu, basi watu uliowaamini sana ndani ya CHADEMA hata kama walikuwa na nyadhifa ndogo, walikubali kutumiwa ili wakutumie wewe kuimaliza CHADEMA na wewe ukaingia mkenge.
Ukakubali kugombanishwa na viongozi wenzako wa ngazi za juu hasa Mwenyekiti Freeman Mbowe ili malengo ya watu hao yatimie. Sasa nakuonea huruma.
Nakuonea huruma kwa sababu kama ni malengo ya hao watu kukutumia kukimaliza chama hawatafanikiwa na badala yake watakumaliza wewe bure na utakuja
kushtuka ukiwa umekwisha kisiasa.
Kama ni malengo yako kwa utashi wako umeamua kutumika kukimaliza chama, nakuhurumia kwa sababu utajimaliza wewe na CHADEMA itaendelea kuimarika bila wewe wala Kafulila.
Ukitaka kujua ninachokisema, tuulize sisi waandishi tunaopata mawazo ya Watanzania moja kwa moja.
Kwa kuanzia muulize tu Edward Kinabo kwamba Jumatano iliyopita alipoandika makala ya "Simwelewi Zitto Kabwe" aliungwa mkono na wasomaji wangapi na walikuwa na mawazo gani juu yako. Hapo ndipo utakapoelewa kile ninachokisema.
Namalizia kwa ujumbe wa msomaji wangu mmoja tu kati ya wengi. Huyu aliniambia anaitwa Meshack na yuko Korogwe. Aliniambia, "Sisi tulishajua kwamba Zitto anaondoka CHADEMA na kwamba anachosubiri tu ni pensheni yake ya ubunge ambayo huwa inatolewa baada ya Bunge kuvunjwa.
Naomba Mwigamba kwa sababu unaweza kuongea na viongozi wakuu wa CHADEMA, waambie kwamba
wasije wakafanya kosa la kumvua Zitto uongozi wala kumvua uanachama.
Sisi hatutaki apate kisingizio cha kuondoka CHADEMA. Waambie wamuache tu mpaka atakapoondoka mwenyewe ili Watanzania wazidi kumfahamu," mwisho wa kunukuu.


Tafakari mwenyewe ulikofika, uamue cha kufanya. Kumbuka uamuzi wa mwisho ni wako wengine tunakueleza tu maana tumejiapiza kuzungumza ukweli hata katikati ya ugomvi.


Kama utaamua kuondoka CHADEMA ama kujivua tu nyadhifa zako. katika yote nakutakia kila heri!


Kwa hisani ya Mu-sir



Nini maana ya MSALITI?
 
Last edited by a moderator:
ACT Tanzania ndio ACT Wazalendo. Baada ya kufanya tafiti kwa wananchi ilionekana wananchi wanataka chama kitakachowarejeshea uzalendo kwa Taifa lao.

Wananchi wengi walishauri iundwe Chama Cha Wazalendo. Hivyo tukaboresha jina letu kwa mujibu wa katiba yetu na kuitwa ACT Chama cha Wazalendo

nikupongeze sana poti kwa malengo mazuri ambayo chama kimeyaweka. lakini nitahadharishe kuwa subordinates wanaweza kuwa kikwazo. mfano katika ngazi za chini kuna viongozi si kwa sababu ya sifa zao bali kwa kuwa walikuwa wa kwanza kuwa wanachama. hatima yake wako tayari hata kupindisha taratibu ili kuendeleza yaleyale tumeyokuwa tukiyapgia kelele kila siku ndani ya ccm. pia urafiki unaweza kutuponza katika kufikia malengo. kuna mtu atataka uongozi kwa kupitia migongo yenu hali ya kuwa jamii haimkubali na mtampa fursa hiyo ni hatari sana. pia viongozi toka vyama vingine lazima tuwafanyie utafiti kabla ya kuwaamini na kuwapa madaraka makbwa sana. mfano wapo ambao wamekuwa chanzo cha mifarakano katika vyama na taasisi wanazoziongoza leo hii tutawaona wakikimbilia huku. TUFANYE UTAFITI JAMII INATAKA WATU WA NAMNA GANI, LA SIVYO TUTAENDELEA KUWA MABINGWA WA MIKAKATI NA LENGO LA UZALENDO KUTOFIKIWA.
 
Kwa hiyo mnaamini kwa dhati kabisa kuwa vyama vya upinzanin vyenye sera zenye mtazamo tofauti na CDM na vile visivyokubaliana na watakavyo viiongozi wa CDM ni maadui wa CDM?unaamini huu ndio msimamo wa kiongozi yoyote mwenye weledi ndani ya CDM?au ni kelele unapiga shabiki?


Kwa hiyo na CUF circa 2005 walitakiwa wapambane na CDM sio, na NCCR Mageuzi Circa 1995-2000 walitakiwa wapambane na CDM na CUF maana ndio walikuwa wapinzani wakuu.


Vitu unavyoandika havina mantiki, havina hoja wala havina mashiko. Unaandika vitu based on paranoia.

Huwezi kumkomboa mtanzania kabla hujamweleza una nini tofauti cha kumpatia. leo hii nikikuuliza CDM itafanya nini tofauti kukuza demokrasia ndani ya Taifa mara kikiwa chama tawala utajibu nini? Naomba jibu la hili.

Fahamu tu jambo moja CDM tuna watu nyeti kila mahali.CDM ni Taasisi kubwa sana.CDM ina intelejensia yake ambayo kila kinachofanywa sirini tunakijua kupitia mfumo wetu wa usalama.

Ndiyo maana tunajua na tunasema bila kupepesa jicho kwamba ACT ni Tawi la CCM ambalo limeanzishwa mahsusi kupambana na CDM na nguvu ya Ukawa kwa ujumla.

Ndiyo maana hata wafuasi mkipiga porojo hapa namna gani mnapoteza tu muda.Tunawafahamu viongozi wa hiki Chama mpaka pesa wanayoitumia wanapata wapi.

Tulishafunga ukurasa kwamba hiki chama cha ACT hakina tofauti yoyote na CCM.Na tutatembea kila kona ya nchi kuwaambia Watanzania Ukweli kwamba wakiogope hiki chama kama Ukoma.
 
Niko kuchangia @ACT kwa mwenenendo huu walioanza nao,
"Wanasiasa Waweke HAKIBA ya MANENO"=WWHM
 
Fahamu tu jambo moja CDM tuna watu nyeti kila mahali.CDM ni Taasisi kubwa sana.CDM ina intelejensia yake ambayo kila kinachofanywa sirini tunakijua kupitia mfumo wetu wa usalama.

Ndiyo maana tunajua na tunasema bila kupepesa jicho kwamba ACT ni Tawi la CCM ambalo limeanzishwa mahsusi kupambana na CDM na nguvu ya Ukawa kwa ujumla.

Ndiyo maana hata wafuasi mkipiga porojo hapa namna gani mnapoteza tu muda.Tunawafahamu viongozi wa hiki Chama mpaka pesa wanayoitumia wanapata wapi.

Tulishafunga ukurasa kwamba hiki chama cha ACT hakina tofauti yoyote na CCM.Na tutatembea kila kona ya nchi kuwaambia Watanzania Ukweli kwamba wakiogope hiki chama kama Ukoma.


Sasa wewe mwanachama wa CDM uliyefunga ukurasa wa ACT, unafanya nini humu kwenye mada ya Zitto, ambaye ni Kiongozi wa ACT, anayehubiri sera za ACT?huoni huu ni undumilakuwili?

Wewe umekuwa nani kuwaambia watanzania kitu gani wakiogope na kitu gani wasikiogope?kwa nini usiwaachie wao hiyo kazi ya kujua kipi ni kizuri na kipi ni kibaya kwao? Hujui kuwa trait za kuwa-manipulate watu kuwalazimisha wakipende au kukichukia kitu flani zinatoka kwenye elements za udikteta?

Eneza sera za CDM, mimi binafsi naamini ni nzuri sana, na zinatosha kushawishi watanzania wengi kujiunga na CDM au kuwa nyuma yao. Lakini siamini kuwa CDM litakuwa Chaguao Pekee la watanzania. kwani hata kwenye nchi zisizo na matatizo kama TZ wananchi wao bado wanapenda vyama tofauti vya siasa.

kama ACT ni chama bomu, hakuna atakayewafuata, kama CCM haitakiwi, kura zitaonesha hilo. Unachokionesha wewe, ni kuwa ili Tanzania Demokrasia iwepo, basi CDM iachiwe iwe chama pekee cha upinzani,REALLY? ndio siasa za wapi hizi? CDM haitakiwi kupinga ujaji wa vyama vyengine vya upinzani,inatakiwa kusapoti hali hii. kwani kuna maeneo CDM haina ushawishi, vyama vya upinzani vilivyobaki vinashinda maeneo hayo na kurudisha ushawishi kwenye upinzani. Miaka nenda rudi mmeshindwa kuwa na ushawishi Zanzibar, CUF wamefanikiwa hadi kuunda serikali, sijawasikia wakisema CDM wako zanzibar kuwapunguzia kura zao hata siku moja, wanamini wana ushawishi na watashinda.

CUF inaonekana ni chama thabiti na chenye mtazamo chanya kushinda CDM kwenye demokrasia kuliko nyie.

Solace pekee iliyobaki ni kuwa wewe ni mshabiki tu, na unachoamini sio wanachoamini viongozi wako, kama wanaamini kwenye ujima wa aina hii, basi political doomsday yao inakaribia.
 
Makala hii iliandikwa na Samson Mwigamba tar 9//12/2009
NAKUHURUMIA ZITTO KABWE

Najua jioni wakati wa kutangaza matokeo hukuwepo lakini nategemea ulipata taarifa za kauli za vijana mbalimbali walizotoa pale wakitaja waziwazi majina ya watu walioharibu uchaguzi ule.
Sikutarajia kama Naibu Katibu Mkuu wa chama upinge hatua ile iliyochukuliwa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na kikao kingine chochote cha juu ya msimamizi wa uchaguzi eti kwa sababu tu rafiki yako Kafulila alikuwa anaongoza.
Hilo lilinipa taabu kubwa na naomba uniwie radhi rafiki yangu lakini nasema ukweli wa nafsi yangu kwamba nilifikia kujiuliza mara mbilimbili kama ungechaguliwa wewe kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, hali ingekuwaje?


Tafakari mwenyewe ulikofika, uamue cha kufanya. Kumbuka uamuzi wa mwisho ni wako wengine tunakueleza tu maana tumejiapiza kuzungumza ukweli hata katikati ya ugomvi.


Kama utaamua kuondoka CHADEMA ama kujivua tu nyadhifa zako. katika yote nakutakia kila heri!


Kwa hisani ya Mu-sir


Mkuu BAK asante kwa kurejea hii makala.
Kusema kweli imemwanika Mhe.Zitto.

Ila na tatizika na
Makala hii iliandikwa na Samson Mwigamba tar 9//12/2009
NAKUHURUMIA ZITTO KABWE
kwamba mtu aliyekuwa anamshauri Zitto kiasi hiki leo yuko naye pamoja kwenye jambo ambalo alikuwa anaona haiko sawa.Kweli yuko pamoja kirafiki kweli.

Kweli ni wazi kuwa safari ya kisiasa ya Mhe.Zitto ina walakini mkubwa kwa sasa-muda utatupa majibu.
 
Last edited by a moderator:
BAK,
Kama huo ndio Usaliti kuna tofauti gani kati ya Zitto na Mzee Mtei?, weka pia maelezo juu yao maana Mtei alikuwa Bepari na Nyerere Mjamaa na mwisho wao haukuwa mzuri pia, lakini hakuna aloitwa Msaliti. Hivi sii kweli kuwa viongozi wanaotofautiana Mrengo hawawezi kuwa chama kimoja na wala haitakiwi!. Kwa maana hizi ukinambia Zitto ni Msaliti wa UBEPARI nitakubaliana nawe..

Kisha mnatumia neno Msaliti kwa Watanzania lihali kila ushahidi mnaotoa ni kwa Chadema kwani Chadema inawakilisha Watanzania wote? Kwa nini mnapenda sana kuwahadaa wananchi? leo na Katiba ya wananchi wakati kumbe mmeona Uchaguzi wa ubunge kupata millioni 12 kwa mwezi kwa miaka mitano ni muhimu kuliko kuipata Katiba Mpya ambayo ndiyo mwongozo na kitu kikubwa sana kwa wananchi?.
 
Tunamjadili msaliti Zitto, usitake kubadili mjadala na kumuingiza Mtei unataka kumjadili Mtei fungua uzi wa Mtei. Wewe ndio wake wale hakuna chochote dhidi ya Zitto utakukubali kama ni usaliti lakini wanaojua maana ya usaliti wameliona hilo la usaliti wa Zitto dhidi ya CHADEMA. Hata rafiki yake Mwigamba aliliona hilo na kunwambia wazi kwamba Watanzania watamuona ni mamluki ndani ya CHADEMA kwa yale aliyotaka kuyafanya lakini wewe mtetezi wa msaliti Zitto hata hilo hukuliona.

BAK,
Kama huo ndio Usaliti kuna tofauti gani kati ya Zitto na Mzee Mtei?, weka pia maelezo juu yao maana Mtei alikuwa Bepari na Nyerere Mjamaa na mwisho wao haukuwa mzuri pia, lakini hakuna aloitwa Msaliti. Hivi sii kweli kuwa viongozi wanaotofautiana Mrengo hawawezi kuwa chama kimoja na wala haitakiwi!. Kwa maana hizi ukinambia Zitto ni Msaliti wa UBEPARI nitakubaliana nawe..

Kisha mnatumia neno Msaliti kwa Watanzania lihali kila ushahidi mnaotoa ni kwa Chadema kwani Chadema inawakilisha Watanzania wote? Kwa nini mnapenda sana kuwahadaa wananchi? leo na Katiba ya wananchi wakati kumbe mmeona Uchaguzi wa ubunge kupata millioni 12 kwa mwezi kwa miaka mitano ni muhimu kuliko kuipata Katiba Mpya ambayo ndiyo mwongozo na kitu kikubwa sana kwa wananchi?.
 
Tunamjadili msaliti Zitto, usitake kubadili mjadala na kumuingiza Mtei unataka kumjadili Mtei fungua uzi wa Mtei. Wewe ndio wake wale hakuna chochote dhidi ya Zitto utakukubali kama ni usaliti lakini wanaojua maana ya usaliti wameliona hilo la usaliti wa Zitto dhidi ya CHADEMA.
Alaa ime ku touch eeeh, Tafsiri ya neno inatumika mahala pote mkuu haichagui Zitto ikawaacha wengine..
 
Tunamjadili msaliti Zitto, usitake kubadili mjadala na kumuingiza Mtei unataka kumjadili Mtei fungua uzi wa Mtei. Wewe ndio wake wale hakuna chochote dhidi ya Zitto utakukubali kama ni usaliti lakini wanaojua maana ya usaliti wameliona hilo la usaliti wa Zitto dhidi ya CHADEMA.

Maana ya MSALITI ni nini?
 
Mkuu Chezeya michuzi weye!!! Jamaa kuona mamilioni waliyoahidiwa toka kwa Mainterahamwe akaona hakuna jinsi ya kuyatia mikononi hayo mamilioni bali ni kukaa meza moja na msaliti pamoja na kuwa anamjua fika na tabia zake za undumilakuwili.

Mkuu BAK asante kwa kurejea hii makala.
Kusema kweli imemwanika Mhe.Zitto.

Ila na tatizika na kwamba mtu aliyekuwa anamshauri Zitto kiasi hiki leo yuko naye pamoja kwenye jambo ambalo alikuwa anaona haiko sawa.Kweli yuko pamoja kirafiki kweli.

Kweli ni wazi kuwa safari ya kisiasa ya Mhe.Zitto ina walakini mkubwa kwa sasa-muda utatupa majibu.
 
This i expected, sio mara ya kwanza mkikosa hoja kuanza kuropoka hovyo bila chembe ya evidence. Ndio maana kina makamba Junior wanawatungia sheria kandamizi.

Sasa kama maprofesa wapo, msioweza kuunganisha sentensi mbili kwa nini ndio muwe mbele kujadili maswala ya CHAMA, na hivyo kukitia DOA? Hamuoni kuwa mnakipa taswira mbovu chama chenu?

yani humu JF ukifungua Mada inayohusu CDM haina tofauti na kijiwe cha shule ya kata, lugha chafu, matusi, assumption za kijinga na hoja dhaifu kabisa.

Mara nyingi hoja zikionekana hazina msaada inawekwa soundtrack ya msaliti hadi inakera.JF wakifuta comments zenu mnalalamika. Binafsi naamini they are doing CDM a favour.

Kama wewe ndio sampuli ya mkombozi na mimi ndio mkobolewaji, sidhani kama nitanyanyua mguu wangu kukufuata. Onesha kuwa una "substance" ya kuwa mkombozi kabla ya kuanza kuimba ukombozi.
Nafukir unatatizo la uelewa,tatizo lako moja tu unafikir indirectly!!!unaongozwa na falsafa za kimapokeo katika kujenga hoja mithili ya wafuasi wa Stallin waliotenda kwa kusikia!!Vyovyote mtakavyomtetea!Zitto amebreak trust kwa watu wenye fikra pevu kinyume chake ndio wanaomwamini.Zitto is opportuniste politician who dont walk on his words/speech.Anaamini wte wajinga na wepesi wa kusau!!!!Ni bingwa wa kujenga hoja zenye lengo la kuseek public empathy!!!its realy awkward to believe in him!!
 
Back
Top Bottom